Vigezo vya mtu kuingia Advance

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Wizara imetoa muongozo kwa ajili ya kuwaongoza wamiliki wa shule zote, yaani za serikali na zisizokuwa za serikali utakaoanza kutumika katika mwaka 2018/2019.

Katika taarifa iliyotolewa na Kaimu katibu mkuu wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu hapo machi 20, imetoa muongozo wa vigezo vitakavyozingatiwa katika udahili mpya wa wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka huu.

Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo.
  1. Ufaulu wa masomo yasiyopungua 3 katika kiwango cha ‘credit’, yaani A,B au C katika masomo yasiyo ya dini kwenye matokeo ya kidato cha nne(4).
  2. Jumla ya alama za ufaulu katika masomo 7 zisizidi 25.
  3. Jumla ya alama za ufaulu kwenye masomo ya tahasusi ziwe 3 hadi 11 kwa shule zisizokuwa za serikali(yaani AAA-CDD),ambapo shule za serikali jumla ya alama za ufaulu zitakuwa 3 hadi 10(yaani AAA-CCD).
  4. Alama ‘F’ isiwe katika somo la tahasusi.
  5. Mwanafunzi atakayedahiliwa asiwe na umri zaidi ya miaka 20.
  6. Wanafunzi watahiliwa kwa ushindani kulingana na nafasi zilizopo katika shule husika kama masharti ya usajili yalivyoelekeza.
  7. Wanafunzi wenye sifa watadahiliwa kwenye tahasusi zilizoidhinishwa na mikondo iliyosajiliwa na wizara ya elimu, sayansi na teknolojia katika shule husika.
  8. Wanafunzi wenye sifa linganishi(ambao matokeo ya mitihani yao siyo ya baraza la mitihani la Tanzania) wataomba udahili kwa kutumia matokeo ambayo yamehakikiwa na kukubaliwa na baraza la mitihani la Tanzania kwamba alama alizopata mwanafunzi zinalingana na alama zinazotamkwa katika muongozo huo kwa ajili ya udahili.

Pia soma Jua Kuhusu Vitu unavyoweza kusoma Chuo Kikuu kutokana na ufaulu wako
 
Back
Top Bottom