Nyaraka Muhimu za Kuambatisha
Unapoomba leseni ya biashara, utatakiwa:
- Kuwasilisha TIN (Taxpayer Identification Number) kutoka TRA ili kuthibitisha kuwa umejiandikisha kama mlipa kodi.
- Kama ni kampuni, jumuisha cheti cha usajili wa kampuni.
- Onyesha mkataba wa pango kama biashara ipo eneo la kupanga.
- Ambatanisha Tax Clearance Certificate kutoka TRA kama uthibitisho wa kutimiza wajibu wa ulipaji kodi.
- Kwa huduma za kitaalamu kama mawasiliano, chakula, mafuta au dawa — toa vyeti vya mamlaka husika: TCRA, TBS, EWURA, TMDA n.k.
- Kwa taaluma maalum kama udaktari, uhandisi, sheria, jumuisha hati ya kitaalamu (Professional Certificates).
MAKUNDI YA LESENI ZA BIASHARA
Leseni zimegawanywa katika makundi mawili kulingana na aina na ukubwa wa biashara:
Kundi A
Hili linajumuisha biashara kubwa zenye mtaji mkubwa kama: wauzaji wa bidhaa nje ya nchi, huduma za mawasiliano, bandari, vilabu vya usiku, bima, huduma za utalii, benki, maduka ya kubadilishana fedha n.k.
Hutolewa na: BRELA (Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni)
Kundi B
Hili linajumuisha biashara ndogo na za kati kama: migahawa, hoteli, vyama vya ushirika, wakala wa bima, viwanda vidogo, udalali, ushauri wa kitaalamu, na uuzaji wa bidhaa jumla na rejareja.
Hutolewa na: Afisa Biashara wa Halmashauri za Serikali za Mitaa
Kupata leseni si kazi ngumu — kinachotakiwa ni maandalizi sahihi, nyaraka kamili, na kuelewa mahitaji ya mamlaka husika.
TUNAKUSAIDIA HATUA KWA HATUA
Mimi na timu yangu tupo tayari kukusaidia kila hatua — kutoka kujaza fomu, kuandaa nyaraka, hadi kufuatilia mpaka upate leseni yako halali kwa haraka na kwa usahihi.
📞 Wasiliana nasi sasa hivi: wa.me/+255693880325Au piga simu moja kwa moja: +255 693 880 325