Vigezo vya kumpa mtu uprofesa wana jf!

kwanza kabisa uprofessor sio daraja la elimu ( ninaposema sio daraja la elimu namaanisha kuwa hausomewi), ila ni ngazi ya utumishi hata kwenye academic institution, ngazi ya kwanza huwa ni tutorial assistant, inafuatia assistant lecturer, lecturer, seniior lecturer, associate professor na mwisho kabisa ni full professor. Sasa katika vyuo vyetu vikuu kuna waraka unaitwa "up the ladder", waraka huu unaeleza ni jinsi gani mtu anaweza kupanda ngazi moja kwenda nyingine, lakini kwa ufupi tu ni kuwa kuwa professor ( boith associate and full) ni lazima kwanza muhusika awe na degree tatu yaani bachelor, masters na phd,na kupanda ngazi moja kwenda nyinge ni lazima muhusika kwanza awe ametimiza miaka mitatu katika post yake ya awali, mfano ili uwe associate professor kigezo cha kwanza ni lazima uwe senior lecturer kwa miaka mitatu, kigezo cha pili ni teaching points ( sina kumbukumbu ni point ngapi zinahitajika) na tatu ni pint kutokana na publication kama nakumbuka vizuri ni point kama 5.5 au 6 hivi na hizi ni kutokana na publication kutoka katika peer reviewed journal! Ukitimiza vigezo hivi vyote ndipo baraza la utumishi la chuo husika hutangaza kumpandisha muhusika kutoka level moja kwenda nyingine!

umesema kweli.

Ila uprofesa ni award ambayo mtu anatunukiwa na sio cheti cha kusomea kama ilivyo phd na masters.
 
Back
Top Bottom