Vigezo na masharti ya kupata kibali cha TBS na TFDA uzalishaji/uuzaji wa chakula

DR.POLITICS

Member
Dec 16, 2015
69
42
Habari wadau JF,

Nimefikiria kuanzisha mradi wa kusaga, kukoboa na kupack unga na mchele ili niweze kuuza kwa watumiaji wa maeneo yote. Nilitembelea Supermarket moja nikaona namna vifungashio vilivyoandikwa na kujaribu kuongea na wahusika wakaniambia ili niweze kuwapelekea bidhaa yangu ni lazima iwe imethibitishwa na TBS na imekaguliwa na TFDA.

Je ni vigezo gani vinahitajika ili niweze kufikia ngazi hii?
 
Habari wadau JF, nimefikiria kuanzisha mradi wa kusaga, kukoboa na kupack unga na mchele ili niweze kuuza kwa watumiaji wa maeneo yote. Nilitembelea Supermarket moja nikaona namna vifungashio vilivyoandikwa na kujaribu kuongea na wahusika wakaniambia ili niweze kuwapelekea bidhaa yangu ni lazima iwe imethibitishwa na TBS na imekaguliwa na TFDA,. Je ni vigezo gani vinahitajika ili niweze kufikia ngazi hii?
Ukipata majibu uni tag mkuu
 
Kwa upande wa TFDA unatakiwa ufike ofisi zao na uombe waje kutembelea na kukaguwa hapo unapoandalia hivyo vyakula. Yaani, watakagua unapohifadhi mpunga kabla ya kuukoboa, na nafaka kabla ya kuzisaga. Kisha watakagua pia mahali unaposagia na kukoboa, mwisho kabisa pale ambapo unafanyia packaging.

Baada ya ukaguzi huo wataandika ripoti yao na utafahamu kama watakupa lesini kwamba eneo lako limekaguliwa na limekidhi viwango vya usafi vinavyohitajika.

Hizo bidhaa zako zote zipo kwenye kundi la nafaka na vyakula vitokanavyo na nafaka. Kusajili bidhaa hizo na TFDA ni dola za marekani 320, ukaguzi wa TFDA gharama yake ni Tsh 100,000, kusajili label ya bidhaa na TFDA ni Tsh 50,000.

Taarifa zangu zinaweza zikawa zimepitwa na wakati, nashauri ufike ofisi ya TFDA kwa uhakika.
 
Wahusishe Afisa Afya, SIDO au Unatakiwa kuandika barua kwa TBS na TBS watakuja kiwandani kwako kukagua ili waangalie mazingira na ubora wa bidhaa unazozalisha ( ikihitajika sample watachkukua ) then wakiridhika unapewa hiyo CERTIFICATE. Taratibu zao zote wameziweka kwenye website yao ya www.tbs.go.tz na www.tfda.go.tz tembelea ujisomee
 
Shukran mkuu
 
UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI (SMEs) KUWEZESHWA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’

1.0 UTANGULIZI

Serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha wenyewe zithibitishwe ubora. Katika utaratibu huu, wapo wajasiriamali ambao husamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo.

Ili kupata msamaha huu, vigezo vifuatavyo huzingatiwa:

• Mjasiriamali hutakiwa kuwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya SIDO iliyo karibu. Ni vema kuhakikisha kuwa barua inafafanua vizuri na kwa kina shughuli zinazofanywa.

• Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA.

• Mjasiriamali hupaswa kuwa na leseni ya biashara.

• Wajasiriamali waliokwishapata leseni ya kutumia alama ya ubora hupaswa kutunza rekodi za uzalishaji na mauzo ambazo watatakiwa kuzionesha kwa wakaguzi wa TBS pindi zinapohitajika.

2.0 HATUA ZA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’

2.1 HATUA YA KWANZA – MAOMBI

• Maombi ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa hufanywa na mwombaji kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS kwa maandishi.

• Majibu hutolewa yakielezea taratibu na gharama zote.

• Majibu huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji huijaza na kuirudisha TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:

? Mtiririko wa uzalishaji wa bidhaa husika;
? Mfumo wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora;
? Orodha ya malighafi anazotumia na mahali zinakotoka kwa kila bidhaa;
? Ramani inayoelekeza jinsi ya kufika kiwandani kwako;

Baada ya hapo tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali hupangwa.

2.2 HATUA YA PILI – UKAGUZI WA AWALI

• Ukaguzi wa awali hufanywa na wakaguzi wa TBS wakati kiwanda kikiwa katika uzalishaji.

• Sampuli huchukuliwa na kupimwa ili kuona kama zinakidhi matakwa ya kiwango husika.

• Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili kurekebishwa.

2.3 HATUA YA TATU – UPIMAJI

• Sampuli zilizochukuliwa hupimwa katika maabara za TBS kwa kufuata kiwango husika.

• Baada ya kazi ya upimaji kumalizika, ripoti ya maabara hutolewa kwa mwombaji.

2.4 HATUA YA NNE – UTOAJI WA LESENI

• Maamuzi kuhusu kutoa au kutotoa leseni ya kutumia alama ya ubora hutegemea tu ripoti ya ukaguzi wa awali wa kiwanda pamoja na ripoti ya maabara.

• Kimsingi ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba mazingira ya uzalishaji kiwandani, mfumo wa uzalishaji na bidhaa iliyopimwa havina matatizo.

• Ikiwa sivyo basi mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena na kuleta sampuli nyingine.

3.0 MUDA WA LESENI (VALIDITY OF LICENCE) YA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’

Leseni ya kutumia alama ya ubora ya ‘tbs’ hudumu kwa mwaka mmoja na huhuishwa (renewal) baada ya kuhakikisha kwamba taratibu zilizokubalika (Scheme of Inspection and Test, SIT) zinafuatwa
 
Habari wadau JF,

Nimefikiria kuanzisha mradi wa kusaga, kukoboa na kupack unga na mchele ili niweze kuuza kwa watumiaji wa maeneo yote. Nilitembelea Supermarket moja nikaona namna vifungashio vilivyoandikwa na kujaribu kuongea na wahusika wakaniambia ili niweze kuwapelekea bidhaa yangu ni lazima iwe imethibitishwa na TBS na imekaguliwa na TFDA.

Je ni vigezo gani vinahitajika ili niweze kufikia ngazi hii?
Anza mtaani kuuzia wakina mangi ukifanikiwa na ukiwa na pesa ya kutosha na unamashine au umeingia mkataba na mwenye machine nenda TBS then mamulaka ya ukakuzi wa chakula jaza form zao na peleka na product yako utapita kirahisi. Afu supermarket watu wananunua vitu kutokana na matangazo au popular product name na supermarket wanataka product zilizofata sheria ilikuepuka msala kwao
 
Je hatukokuwa na usumbufu wowote nikianza tu kuwauzia kina mangi?
 
Haitakua na usumbufu cha msingi wewe update faida na wao wapate faida. Pia inabidi uwashawishi kua product yako nikiwango na mteja akinunua anaweza kufanya Wateja wengine wakanunue product yako hivyo utakua umeanza kukamata soko.
 
Biashara ina changamoto kubwa sana kama mtaji wako mdogo na wakopaji wengi sana na sio waaminifu.

Pia wateja wengine wananunua bidhaa ya unga kwa jina hata kikiwa kibovu. Niliyaona wakati nilikuwa na duka jumla.
 
UTARATIBU WA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WA KATI (SMEs) KUWEZESHWA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
1.0 UTANGULIZI

Serikali hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha wenyewe zithibitishwe ubora. Katika utaratibu huu, wapo wajasiriamali ambao husamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo.

Ili kupata msamaha huu, vigezo vifuatavyo huzingatiwa:

• Mjasiriamali hutakiwa kuwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya SIDO iliyo karibu. Ni vema kuhakikisha kuwa barua inafafanua vizuri na kwa kina shughuli zinazofanywa.

• Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA.

• Mjasiriamali hupaswa kuwa na leseni ya biashara.

• Wajasiriamali waliokwishapata leseni ya kutumia alama ya ubora hupaswa kutunza rekodi za uzalishaji na mauzo ambazo watatakiwa kuzionesha kwa wakaguzi wa TBS pindi zinapohitajika.

2.0 HATUA ZA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’

2.1 HATUA YA KWANZA – MAOMBI

• Maombi ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa hufanywa na mwombaji kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS kwa maandishi.

• Majibu hutolewa yakielezea taratibu na gharama zote.

• Majibu huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji huijaza na kuirudisha TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:

? Mtiririko wa uzalishaji wa bidhaa husika;
? Mfumo wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora;
? Orodha ya malighafi anazotumia na mahali zinakotoka kwa kila bidhaa;
? Ramani inayoelekeza jinsi ya kufika kiwandani kwako;

Baada ya hapo tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali hupangwa.

2.2 HATUA YA PILI – UKAGUZI WA AWALI

• Ukaguzi wa awali hufanywa na wakaguzi wa TBS wakati kiwanda kikiwa katika uzalishaji.

• Sampuli huchukuliwa na kupimwa ili kuona kama zinakidhi matakwa ya kiwango husika.

• Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili kurekebishwa.

2.3 HATUA YA TATU – UPIMAJI

• Sampuli zilizochukuliwa hupimwa katika maabara za TBS kwa kufuata kiwango husika.

• Baada ya kazi ya upimaji kumalizika, ripoti ya maabara hutolewa kwa mwombaji.

2.4 HATUA YA NNE – UTOAJI WA LESENI

• Maamuzi kuhusu kutoa au kutotoa leseni ya kutumia alama ya ubora hutegemea tu ripoti ya ukaguzi wa awali wa kiwanda pamoja na ripoti ya maabara.

• Kimsingi ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba mazingira ya uzalishaji kiwandani, mfumo wa uzalishaji na bidhaa iliyopimwa havina matatizo.

• Ikiwa sivyo basi mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena na kuleta sampuli nyingine.

3.0 MUDA WA LESENI (VALIDITY OF LICENCE) YA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’

Leseni ya kutumia alama ya ubora ya ‘tbs’ hudumu kwa mwaka mmoja na huhuishwa (renewal) baada ya kuhakikisha kwamba taratibu zilizokubalika (Scheme of Inspection and Test, SIT) zinafuatwa.

Back
Top Bottom