Stay Tuned,Kumbe Kifurushi hichi ni TAMBAZI sio jipu na kila mtu anaogopa kumvisha paka kengele ila mimi najitoa kwa ajili ya watu wengine,malalamiko kibao mpaka staff nao wanalalamika sasa ngoja nikupe maajabu yaliyonitokea!
Niliingia Hospitali saa 5:30 usiku siku ya tarehe 3/1/2015 nikapokelewa vizuri na mgonjwa wangu akahudumiwa na daktari,baadae akanishauri kuwa tunahisi ni tetanus hivyo ni vizuri mgonjwa alazwe ili kesho aonane na specialist,nikalipa bill zangu za awali za matibabu kama orodha ifuatayo:-
1.SELFT REFERAL PARTIENTS
casuality by pass fee & without appointment)............................ Tsh 20,000/=
2.RBG................................................. Tsh 2,500/=
3.B/S(Haematology)........................... . Tsh 2,000/=
4.Cannula,syringe na Gause................. Tsh 2,100/=
5.Oframax,ATS,Metris.......................... Tsh 11,000/=
6.Card ya Matibabu ya CRDB................ Tsh 2,000/=
TOTAL Tsh 39,600/=
Baada ya Huduma hii kupatiwa na kulipwa nikashauliwa ni bora mgonjwa alazwe ili apate uangalizi wa karibu kwani Tetanus ni ugonjwa hatari,ili specialist aonane nae asubuhi na hii ilikuwa kama saa 9 :11 usiku,ndipo ikadaiwa nilipe kifurushi cha 150,000/=kama Malipo ya awali,(deposit package)kwa wagonjwa wa kawaida(general) wanaolazwa,na asubuhi yake tarehe hiyo hiyo saa 4 asubuhi akaja daktari round akamdischarge(akamruhusu)kuwa hana tetanus na hakupewa dawa yeyote zaidi ya drip(ambayo ililipwa awali kabla ya kumlaza) wakati naenda kufanya clearance naambiwa HELA YAKO IMETOSHA!..Niko na Maongezi na Uongozi Baada ya Ofisi ya Mahusiano,Malipo Kushindwa Kujibu Hoja zangu nilizowapelekea ila nina clip za sauti za kila niliyeongea nae toka naingia hospitali saa 5:30 usiku na majibu yao,na hoja tulizofanya nitaziupload tuzisikie na tushauriane ili tujue Tambazi(jipu kubwa la ndani) Tutalimalizaje!na kila unaemkuta analalamika !
-