Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,194
Kesi ya Kikatiba ya Sheria ya Ndoa Imeanza kusikilizwa Tarehe 9 Machi
Kesi ya kikatiba namba 5. ya mwaka 2016, inayopinga vipengele vya sheria ya ndoa imeanza kusikilizwa leo March 9 kwa upande wa mleta maombi kuwasilisha kwa maandishi maelezoya upande wake mahakamani. Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji likiongozwa na Jaji Kiongozi Shaban Lila, jaji Sakiet Kihiyo na Jaji Munisi. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Tar 15 mwezi wa 3 kwa upande wa serikali kuleta maelezo yao.
Kesi hiyo ya Kikatiba ilifunguliwa na Rebeca Gyumi, mwanaharakati wa haki za binadamu hasa haki za mtoto wakike, na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la MsichanaInitiative linalofanya kazi ya kutetea haki ya mtoto wa kike kupata elimu,kupitia kwa wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocates.
Vipengele vinavyopingwa ni kifungu cha 13 na 17 vya sheria yandoa (CAP 29 R.E 2002) kwa kutoa mwaya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka15 kwa ridhaa ya wazazi. Ambayo ni kinyume na Ibara ya 13,12na 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria, kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.
Vifungu vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 vyapingwa mahakamani
Kesi hiyo ya Kikatiba iliyosajiliwa na kupewa namba 5 ya mwaka 2016 imefunguliwa na Rebeca Gyumi, mwanaharakati wa haki za binadamu hasa haki za mtoto wa kike, na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Msichana Initiative linalofanya kazi ya kutetea haki ya mtoto wa kike kupata elimu,kupitia kwa wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocates.
Vipengele vinavyopingwa ni kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa (CAP 29 R.E 2002) kwa kutoa mwaya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi. Ambayo ni kinyume na Ibara ya 13,12 na 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria, kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.
Vifungu hivi vya sheria vimeweka umri tofauti kati ya mtoto wa kike na wa kiume na hivyo kupingana na Ibara ya 13 (1) (2) ya Katiba inayotoa haki ya usawa mbele ya sheria, na kwamba ni kosa kuwa na sheria zinazobagua. Wakati mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi, umri wa mtoto wa kiume kuoa ni miaka 18.
Kifungu cha 17 kinachotoa ruhusa kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi, kinaminya utu na haki ya mtu kujieleza kama zilivyoainishwa kwenye Ibara ya 12 na 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Masuala ya ndoa si kama mikataba ya biashara, pande zinazoingia kwenye ndoa lazima zikubaliane na si kulazimishwa. Na tumeona hata matukio ambapo wazazi walikatiza mtoto wa kike masomo ili aolewe.
Shauri hili linaiomba mahakama kuu kuvifuta vifungu hivi na kupandisha umri wa chini wa kuoa/kuolewa kwa mwanaume na mwanamke kuwa miaka 18.
Ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike zaidi ya kuwa suala la ukiukwaji wa haki za binadamu, pia ni suala la kiafya, elimu na kisaikolojia. Msichana kujifungua katika umri mdogo ni chanzo cha matatizo kama Fistula na vifo vingi vya wajawazito. Ingawa huwezi peleka shauri mahakamani kudai haki ya kupata elimu Kikatiba, lakini haki hii ni muhimu sana kuzingatiwa na kuhakikisha hakuna mianya inayoweza kutumiwa kuzima ndoto za watoto kubaki shuleni na kusoma.
Takwimu za ndoa za utotoni duniani zinaonesha Tanzania kuwa moja ya nchi zenye viwango vikubwa vya ndoa katika umri mdogo. Kwa wastani watoto wakike wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Kwa mwezi wa 1 tu 2016 tumeshasikia kesi za watoto wa kike kuolewa au kutaka kuozwa wakiwa chini ya miaka 15.
Pamoja na kuwa utoaji wa elimu kwa jamii, vikundi vya dini na kupinga mila na desturi ni muhimu kutokomeza ndoa za utotoni, uwepo wa sheria inayomlinda mtoto wa kike na wa kiume ikiendana na utekelezaji wa sheria hizi ni muhimu zaidi ili kutokomeza kabisa tatizo hili la ndoa za utotoni.