Kupitisha sheria ya ndoa kuwa miaka 9 ni aina fulani ya upungufu wa akili

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
290,261
746,258
Hatimaye bunge la Iraq limepitisha rasmi sheria ya ndoa kuwa miaka 9.. Kwamba mtoto wa kike akifikisha miaka tisa basi ni ruhusa kuolewa
Ndoa ninini!? Wengine watakwambia ni ndoano.. Lakini ndoa ni mapatano/makubaliano ya kuishi pamoja watu wa jinsia mbili tofauti kama mke na mume kwa muktadha wa kujenga familia na kuzaa watoto .. Na ni lazima ziwepo hisia na natamanio ya upendo na kupendana.. Na kikubwa kuliko yote.. Wote wawe na uwezo wa kufanya ngono
Baada ya hapo ndio yanafuata majukumu mengine ya kifamilia

Ndoa inahitaji upevu na ukomavu wa akili lakini pia upevu na ukomavu wa mwili..
Je mtoto wa miaka tisa kakomaa kimwili?
Je mtoto wa miaka tisa keshapevuka kiakili
Je mtoto wa miaka tisa keshavunja ungo kiasi cha via vyake vya uzazi kuruhusu kuingiliwa kingono?
Je mtoto wa miaka tisa anajua maana ya ndoa na majukumu yake yote?

Ndoa ni tendo la hiari katika ulazima wake.. Ndio ma a na siku ya kufunga harusi wahusika huulizwa kama wamekubali.. Mtoto wa miaka tisa ambaye hajajua vema hata kufua chupi na kujiswafi unawezaje kumbembesha jukumu zito kama hilo?
Huo ni ubakwaji
Huko ni kubemendwa
Huo ni utumwa wa kingono
Huko ni kuvunja haki za msingi za binadamu na za mtoto wa kike
Huko ni kufisha na kuua kabisa ndoto zao maishani maana ndoa ni gereza kwa wasiojua maana ya ndoa
Iraq kwenye hili imekengeuka haki na ustawi wa uumbaji na furaha na afya ya akili na mwili kwa mtoto wa kike! IKEMEWE..!
 
Waarabu hawajawahi kuwa na akili. Hata huku Afrika mashariki kuna watu wanatenda upumbavu wa kuoa watoto 7-9 wakiamini ni suna sababu mtume Muhamad alifanya hivyo.
Je Mtume alioa katika mazingira gani?
Je watu wa wakati huo tunaweza kuwalinganisha na wa kileo?
 
Back
Top Bottom