DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Idadi ya vifo kutokana na maandamano yenye vurugu nchini Nepal imeongezeka na kufikia watu 31, huku juhudi zikiendelea kuunda serikali ya mpito kufuatia kuondolewa kwa Waziri Mkuu KP Sharma Oli.
Kwa mujibu wa Idara ya Tiba ya Uchunguzi wa Maiti katika Hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu cha Tribhuvan, miili 25 kati ya waliouawa imetambuliwa, huku miili sita, ukiwemo wa mwanamke mmoja bado haijafahamika.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Nepal walifyatua risasi kwa wafungwa waliokuwa wakijaribu kutoroka katika Wilaya ya Ramechhap, Mkoa wa Bagmati, na kuua wawili pamoja na kuwajeruhi zaidi ya kumi na wawili.
Maandamano hayo na jaribio la kutoroka yamezidisha hali ya taharuki nchini humo, wakati viongozi wakiendelea na mazungumzo ya kisiasa ya kuunda serikali ya mpito.
Chanzo: Global Tv