Vifo mfululizo vyatikisa mji wa Moshi

Vifo mfululizo vyatikisa mji wa Moshi

Kwa nini mabalaa iwe kwa walioshangilia kifo cha mwendazake tu

Unajua kinachotokea Mwanza na Sengerema kulikopita mbio za Mwenge juzi?

Au kwa sababu serikali bado haijaridhia kutoa takwimu za siku kwa mahali?

Pumzikeni kwa amani Engineer wa madaraja bila kukusahau ewe jiwe pale Geita.

Usisahau wanaokufa wasiokuwa na majina ni wengi zaidi.
 
Usukuma sasa hivi ni itikadi?

Au sijakuelewa!

Hata Bashiri, pole pole, wajaliwa, walamila, na wengi wengine ni wasukuma kiitikadi.

Yes usukuma ni itikadi kwa maana kamili na wala si mpya. Au na wewe mmoja wao?
 
Hata Bashiri, pole pole, wajaliwa, walamila, na wengi wengine ni wasukuma kiitikadi.

Yes usukuma ni itikadi wala si mpya. Au na wewe mmoja wao?
Duh huu wehu ni mpya

Hii ni kwasababu wasukuma hawashangilii vifo vinavyotokea moshi, kama mlivyoshangilia vilipokua vinatokea mwanza?

Hii akili ya wapi hii?

so unataka wasukuma wawatengenezee itikadi na nyinyi?
 
Duh huu wehu ni mpya

Hii ni kwasababu wasukuma hawashangilii vifo vinavyotokea moshi, kama mlivyoshangilia vilipokua vinatokea mwanza?

Hii akili ya wapi hii?

so unataka wasukuma wawatengenezee itikadi na nyinyi?

Ukiambiwa corona hipo utakuwa wakwanza kupinga
 
Duh huu wehu ni mpya

Hii ni kwasababu wasukuma hawashangilii vifo vinavyotokea moshi, kama mlivyoshangilia vilipokua vinatokea mwanza?

Hii akili ya wapi hii?

so unataka wasukuma wawatengenezee itikadi na nyinyi?

Unayasoma wapi hayo ya wasukuma na shangiliaji? Au ni kuota ndoto chighafla tu?

Au ni jitihada tu za kurukia treni kwa mbele?
 
Una akili?

Wewe ndo una akili maana hata ujui icho kifaa unachotumia wamekuzindulia wasukuma au wanasayansi.ukiumwa unakwenda kwao,ukitaka kumtumia pesa mchepuko,umeme,spika,nguo nzuri.
Kama una akili naomba kaishi na nyani
 
Wewe ndo una akili maana hata ujui icho kifaa unachotumia wamekuzindulia wasukuma au wanasayansi.ukiumwa unakwenda kwao,ukitaka kumtumia pesa mchepuko,umeme,spika,nguo nzuri.
Kama una akili naomba kaishi na nyani
Duh! Unaelewa ulichoandika?
 
Waliokutuma wameamua wakudhalilishe bila wewe kujua.
Uliyetumwa ni wewe ndiyo maana hata ulipoambiwa uonyeshe unaposoma usukuma kama kabila au shangilizi umeshindwa kupaona.

Wacha kudandia litereni kwa mbele!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
COVID-19

View attachment 1848567Mji wa Moshi unazizima, ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mfululizo wa vifo vya watu wenye umaarufu waliofariki ndani ya wiki moja, katika hospitali za mkoa wa Kilimanjaro.

Watu wanane mashuhuri katika mji wa Moshi wamefariki dunia kutokana na maradhi ambayo hayakuwekwa wazi, huku vifo vyao vikiwa gumzo katika mitandao ya kijamii kutokana na vifo hivyo kufuatana.

Familia ya wafanyabiashara inayofahamika ‘The Big Family’ imepoteza wanachama wake watatu ndani ya siku saba, ambao ni mfanyabiashara Stanley Shayo anayemiliki kampuni ya Tanganyika Tours na baa ya Kwetu Longe.

Mwenyekiti wa bodi ya The Big Family, Christopher Shayo jana alithibitisha kuondokewa na wanafamilia watatu ndani ya wiki moja na kwamba jana asubuhi alifariki Soren Kaale, aliyewahi kuwa meneja mkuu wa Moshi Timber Utilization.

“Ni kweli zimekuwa siku mbaya kwetu. Leo hii (jana) tumempoteza Soren Kaale na ndio nimetoka KCMC muda huu. Juzi hapa tumempoteza Stanley Shayo tena tumempoteza katikati ya majonzi ya kumpoteza Boniface Ngowi,” alisema.

Mbali na hao, lakini juzi asubuhi zilisambaa taarifa ya kufariki kwa diwani wa kata ya Kileo Wilaya ya Mwanga, Salim Zuberi aliyefariki katika hospitali ya St Joseph na kifo chake kulithibitishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga, Zefrin Lubuva.

“Tumempoteza kiongozi wetu. Niwaombe wananchi wa kata ya Kileo wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu, lakini niendelee kuwasisitizia wachukue tahadhari dhidi ya virusi vya corona kwa vile eneo letu ni la mpakani,” alisema.

Wiki hii pia wakazi wa mji huo walitikiswa na kifo cha mmiliki wa duka kubwa la dawa za binadamu la Pharm Source lililopo jirani na Nyumbani Hoteli, Doreen Njau au Ashura Mshana na kifo chake kilitikisa mitandao ya kijamii nchini.

Mbali na mfanyabiashara huyo, lakini kifo cha Ofisa Afya katika kituo cha Forodha cha Holili, Edward Ocheing nacho kiliibua mshtuko, hasa ikizingatiwa kifo chake kilitokana na kujisikia tu vibaya na hakuchukua muda mrefu alifariki dunia.

Jana mji wa Moshi uligubikwa na taarifa za simanzi za kifo cha aliyewahi kuwa mkuu wa Idara ya Mazingira ya Manispaa ya Moshi, Danford Kamenya aliyehamishiwa Jijini Mwanza kikazi ambako ndipo umauti ulipomkuta jana.

Mbali na msiba huo, jana hiyo hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alimpoteza ndugu yake aitwaye Charles Mbowe, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema alilithibitishia gazeti hili juu ya kufariki kwa Charles na kwamba alikuwa amelazwa KCMC kwa muda wa wiki moja sasa akipatiwa matibabu kabla ya umauti kumkuta jana asubuhi.

Taarifa zaidi zilidai kuwa Mbowe ambaye alikuwa katika shughuli za chama alilazimika kusitisha na kuanza taratibu za mazishi ya Charles.

Mwananchi.
 
Back
Top Bottom