Vifo Krissmass | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo Krissmass

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 27, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU Kadhaa amefariki kwa nyakati tofauti katika sikuuu ya Noel kwa sababu tofauti tofauti jijini Dar es Salam.
  Tukio la kwanza lilitokea eneo la barabaraya Sam Nujoma, ambapo mtu mmoja amefariki dunia papohapo ka kugongwa na gari.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ajali hiyo ilitokea juzi, majira ya saa 10.15 jioni, katika eneo la Mlimani City.

  Gari aina ya Suzuki lililokuwa likitokea Mwenge kuelekea Ubungo liligonga pikipiki yenye namba za usajili T. 922 BMB aina ya Honda iliyokuwa ikiendeshwa na Emmanuel Mwaikasu (38) waligongana na kupoteza mwelekeo na na kwenda kmgonga mtembea kwa miguu aliyekwua akipita eneo hilo.

  Tukio la pili lilihusisha vijana wawili waliokuwa wakigombana kutokana na sababu za kimapenzi na kupelekea mmoja kufariki kwa kumtia kisu cha mbavu mwenzake.

  Ilidaiwa kuwa vijana haow anaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30, waishio maeneo ya Mbande walikwua wakigomabani mwaname ambpo ilidaiwa mmoja akti ya vijana hao alimkuta mpoenzi wake huyo akiwa na kijana huyo.

  Hivyo katika pulukushani za ugomvi imepelekea mmoja kufariki dunia muda mchache baada ya kufikishwa zahanati kwa kujeruhiwa na mwenzake huyo.

  Katika tukio lingine, Dominic Kivubo (41) amekutwa akiwa amejinyonga katika shamba la kiwanda cha matofali huko Pugu.

  Tukio hiloo lilidaiwa kuwa, lilitokea wakati wa sikuuu ya krissmas majira ya saa 12.asubuhi, kwa kukutwa akiwa amejinyonga kwenye mti wa msonabari kwa kutumia kamba ya katani.
   
 2. E

  Exav Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Poleni sana wote mlioondokewa na wapendwa. Roho za waliotangulia mbele ya haki zilazwe pema peponi...
   
Loading...