Vifaru, ndege za kivita na makombora: Fahamu silaha zilizotumwa Ukraine

Vifaru, ndege za kivita na makombora: Fahamu silaha zilizotumwa Ukraine

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Tangu uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine Februari 2022, mataifa ya magharibi yametenga zaidi ya $250bn, (£205bn) za kijeshi, kibinadamu na misaada mingine ya kifedha kwa Ukraine.

Hebu tuangazie aina ya vifaa vya kijeshi ambavyo vimepewa Ukraine.

Ukraine imekuwa ikitumia makombora ya ATACMS yaliyotengenezwa na Marekani ambayo yana masafa ya takriban maili 190 (300km).

Mnamo Novemba, Rais wa zamani Joe Biden aliondoa marufuku hiyo, na kuruhusu ATACMS kutumika kushambulia Urusi.

Uingereza na Ufaransa zimeipatia Ukraine makombora ya Storm Shadow au Scalp, ambayo yana upeo wa juu wa maili 155 (250km), na ambayo Ukraine imeripotiwa kurusha katika eneo la Urusi.

Mwishoni mwa Julai mwaka jana, Rais Volodymyr Zelensky alisema jeshi la anga la Ukraine limepokea kundi la ndege za kivita za F-16 kutoka Magharibi. Amesema mengi zaidi yalihitajika.

Nchi za NATO, zikiwemo Ubelgiji, Denmark, Uholanzi na Norway, zimeahidi kuipatia Ukraine ndege 65 au zaidi zilizotengenezwa na Marekani, ambazo zilikuwa zimepanga kuzistaafisha kutoka kwa vikosi vyao vya anga.

Mapema mwaka wa 2023, mataifa ya Magharibi yalikubali kutuma vifaru nchini Ukraine. Ilitarajiwa wangewezesha vikosi vyake kuvunja safu za ulinzi za Urusi katika makabiliano.

Uingereza ilitoa Vifaru 14 aina ya Challenger 2s. Mataifa ya Ulaya yametuma zaidi ya vifaru 200 vya Ujerumani Leopard 1 na Leopard 2, kulingana na takwimu kutoka Taasisi ya Kiel.

Marekani ilituma vifaru vyake 31 vya M1 Abrams, ambavyo vinafikiriwa kuwa vya kisasa zaidi duniani.
 
Back
Top Bottom