Vifaa Muhimu Vya kuwa navyo Jikoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
1.Sufuria



Ili uweze kupika kitu cha kwanza unachohitaji ni sufuria. Sufuria ni chombo ambacho kinatumika kila siku katika mapishi mbalimbali hivyo ni vyemaa ukanunua sufuria bora ambazo ninadumu muda mrefu, nzito haziunguzi kwa urahisi na ziwe za kuvutia. Hakikisha unazisugua vizuri na kutakata baada ya kumaliza kuzitumia, haipendezi kuwa na sufuria nyeusi kwa masizi, labda uwe unatumia jiko la kuni.

2. Vikaangio (frying pan)




Vitatumika unapotaka kukaanga kwa kutumia mafuta, kupika mayai au hata kupikia vyakula vingine. Ni vyema ukawa nazo zaidi ya moja, kwa kuanzia 2 moja kubwa na nyingine ndogo.

3. Miko




Ya saizi na aina mbalimbali. Miko itakusaidia unapopika ugali, wali, mayai scramble, na mboga mbali mbali. Tafuta miko imara na iliyo laini yenye umbo la kuvutia.

4. Vijiko vya kupikia




Hivi ni vijiko vikubwa maalumu kwa kupikia vitu mbalimbali na kupakulia kutoka kwenye sufuria. Vijiko hivi vinatumika jikoni na sio kwenye meza ya chakula. Vipo vya plastic ngumu na vya alminium, na huwa vinakuwa seti ya vijiko sita ( cha kupakulia supu, cha kupakulia tambi, cha kutolea vitu kama chipsi, ndizi n.k kwenye mafuta, cha kupakulia wali, cha kukaangia chapatti, na cha kukaaagia maandazi)

5. Kikwauzo (Grater)




Hivi vipo vya aina nyingi tofauti tofauti ila ni vya muhimu sana katika mapishi. Kitakusaidia kukwaruza nyanya, karoti na vitu vingine vingi katika mapishi yako. Tafuta ambacho ni imara na chenye meno tofauti tofauti ili kiweze kukusaidia katika mapishi tofauti tofauti.

6. Peeler




Hiki ni kifaa kinachotumika kumenya karoti, viazi, tango n.k na pia huweza kutumika kukatia kachumbari na ni nzuri sana kukatia kabichi, ni rahisi na hutumia muda mfupi sana. Ni kifaa ambacho ni lazima kiwepo kwenye jiko lolote.

7. Whisk




Kama unavyokiona hapo pichani, sijajua kwa Kiswahili kinaitwaje, kifaa hiki hutumika kupigapiga mayai na pia kuchanganya unga wa kupikia chapati za mayai. Ni rahisi kutumia na hufanya ung wako uwe laini bila mabonge bonge kwa muda mfupi.

8. Kinu kidogo


Tafuta kinu ambacho ni laini kwa ndani ili unaposaga vitu mbalimbali viweze kusagika kwa urahisi bila kupotea kwenye kinu. Kinu hiki kitakuwezesha kusaga vitunguu saumu, tangawizi, na vitu vingine vidogo vidogo.

9. Ubao wa Kukatia




Zama za kukata kata nyama, mboga na vitunguu kwenye mikono zimepita, usihatarishe vidole vyako tena. Tafuta kibao cha kukatia na uwe unakitumia hicho, ni rahisi na pia ni salama kwa afya yako. Vipo vya aina mbali mbali chagua kile ukipendacho na ukitumie.

10. Visu




Wekeza kwenye visu imara na vizuri vya aina na ukubwa tofauti tofauti. Kisu ni kifaa ambacho ni muhimu sana jikoni, ni vyema ukawa na visu vya kazi mbalimbali mfano kukatika mboga na nyama laini, kukatia nyama ngumu na yenye mifupa, kidogo cha kukatika matunda n.k.

11. Kichujio ( Colander)




Hiki hutumika kuoshea mboga za majani kama mchicha n.k kwa mtu anayetumia maji yanayotiririka bombani, pia hutumika kuchuja tambi baada ya kuiva. Ni kifaa kizuri kuwa nacho jikoni kwako.

12. Vitambaa vya Jikoni




Tafuta vitambaa vizuri na vya pamba kwa ajili ya kufutia meza/ jiko na vingine kwa ajili ya kufutia vyombo. Haipendezi kuwa na vitambaa vya jikoni vya kanga iliyochakaa kisha ikachanwa, nunua vitambaa vizuri ili kupendezesha jiko lako na ni rahisi kuvisafisha na kugundua kama ni vichafu. Tofautisha rangi kati ya vile vya vyombo na vya kufutia meza.

13. Ndoo ya Uchafu




Unapopika utahitaji kutupa uchafu kama maganda na mwingine sasa ni vyema ukawa na ndoo ya kuwekea uchafu jikoni kwako ambayo itakuwa inamwagwa mara kwa mara. Weka mfuko wa plastiki ndani ya ndoo ili iwe rahisi kuisafisha baada ya kumwaga uchafu.

14. Brender / Food Processor



Hii ni vyema ukawa nayo na itakusaidia katika mambo mengi. Unaweza ukawa na brender pekee na kama uwezo unaruhusu unaweza ukanunua food processor kabisa. Brender itakusaidia kutengeneza juice za aina mbalimbali na ukinunua yenye 2 in 1 utapata na kifaa cha kusagia karanga. Kama una motto mdogo food processor itakuwezesha kumtengenezea vyakula mbali mbali.

16. Toaster




Hutumika kukaushia mikate ili iweze kuwa na ladha nzuri, sio cha lazima sana ila ni kizuri kuwa nacho kama mfuko utaruhusu.
Kwa uchache hivi ni vifaa vya muhimu kwa maandalizi ya chakula.



womenofchrist
 
Back
Top Bottom