Vietnam War katika kumbukumbu

ikiendelea niite maana umenikumbusha movie yangu pendwa rambo |||
 
Vietnam war katika kumbukumbu
Sehemu ya pili (2)

Huu ni mwendelezo wa makala hii fupi kuhusu historia ya vita vya Vietnam.
Kwanza kabisa napenda kuwaomba radhi ndugu wasomaji na wapenzi wote wa jukwaa letu pendwa pamoja na Wana JF wote maana wengi wenu mmeonesha kutopendezwa kabisa na utaratibu wa kuletewa habari fupi fupi na ahadi za miendelezo ya masimulizi.
Lakini kwa ufupi hii hutokana na mtindo wa maisha yetu na hatuwezi kukwepa jambo hili kutokana na ufinyu wa muda wa ziada wa ku-share mambo kwa pamoja hapa JF kuwa ni mdogo mno. (Tusamehane wakuu)

Katika sehemu hii ya pili ya masimulizi haya tutayaangazia masuala mbali mbali yaliyojitojeza katika vita vya Vietnam. Vita iliyobeba historia kubwa sana huku ikihusisha mataifa kadhaa tokea Asia, na Marekani ambapo nje ya Marekani kuonekana kama mshiriki mkuu katika vita hivyo lakini ndani yake kulikuwapo na mataifa mengine kama vile Laos, Cambodia, uchina na nchi nyingine za ulaya wakiwa washirika wakuu wa Marekani.
Twende pamoja. Mnamo mwezi January 1973, umoja wa mataifa ukishirikiana na Amerika ya kaskazini walihitimisha makubaliano ya mwisho ya amani na kukomesha vita vya wazi kati ya mataifa mawili.
Vita kati ya Vietnam ya kusini na Vietnam ya kaskazini (tunakumbuka Marekani ni kama aliununua ugomvi katika vita hivi, na kumuunga mkono aliekuwa mtawala wa Vietnam ya kusini na huu ni utaratibu wa Marekani kukuza mambo na vita kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine kama vile Iraq,Syria,na kwingineko) na katika vita hivi vya Vietnam waliopaswa kuwa wenyeji wa vita ni wa-vietnam wenyewe, ila kwasababu ya Marekani kuitaji kupambana dhidi ya kuangamiza nguvu za usoviet, na itikadi za kikomunisti ndipo ikiingia vitani na kuiunga mkono Vietnam ya kusini dhidi ya iliyokuwa Jamuhuri ya Vietnam ya kaskazini iliyokuwa na makazi yake makuu huko Hanoi
"Wanajeshi wa Marekani wakisaidia majerui wao katika uwanja wa vita"


Tukirudi nyumba kidogo tunaona ijapokuwa kulifanyika makubaliano ya kumalizia vita yaliofanywa mwaka 1973 lakini vita viliendelea mpaka mwezi April 30, 1975 huku majeshi ya (DRV) yalipoitwaa Saigon iliyokuwa ngome ya Vietnam ya kusini yenye kuungwa mkono na Marekani na washirika wake na kisha kuibadilisha jina na kutoka Saigon na kuita Ho Chi Minh city, jina la kiongozi wao ambaye wakati huo alikwisha kufa kutokana na maradhi ya kawaida tu na sio kuuwawa na Wamarekani.
Bwana Ho Chi Minh
Tunaendelea. Kumbuka pia makala hii imeandikwa kwa mtindo wa mbele nyumba, nyuma rudi mbele hivyo basi tuzingatie katika usomaji wetu.
Wakati vita baridi (cold war) vikiimarika duniani kote , Marekani ilijipanga vyema kukabiliana na washirika wowote wale watakao jitokeza na kuungana na umoja wa kisoviet na hapo ndipo aliekuwa Rais wa Marekani wakati huo bwana Dwingh Eisenhower aliahidi msaada wa hali na mali kwa bwana Dien na Vietnam ya kusini ili kupambana na kuuangusha utawala wa Vietnam ya kaskazini ya kina Ho Chi Minh.
Marekani kama ilivyo kawaida yake ilitoa mafunzo na vifaa vya vita kwa wapiganaji wa Vietnam ya kusini pamoja na kuongezewa maajenti wa CIA ili kutoa mafunzo na kuweka mikakati sawa.
Baada ya kupata msaada na nguvu ya kutosha, jeshi la Dien lilivamia huko Viet Minh, upande wa kaskazini na kuwakamata waviet Cong au unaweza kuwaita Vietnamese Communist ambapo waliwakamata mateka watu laki moja (100,000) kisha kuwatesa na kuwaua kikatili ikiwa ni pamoja na kuwanyonga.
Baada ya hapo kibao kiligeuka, pale ambapo ndani ya mwaka 1957 waviet-cong na wapinzani wengine wa Dien walipoungana na kuanzisha mashambuluzi dhidi ya viongozi wa serikali na hadi ilipifikia mwaka 1959 wa Viet Cong wameanza kuwa na jeshi kubwa sana, kama ulishawahi kufuatilia movie za kivietnam kama vile ile ya PLATOON, utakuwa unajua mziki wa waviet-cong huwa hawaishi wanakuja kama nyuki na kauli mbiu yao ni kusonga mbele tu pia katika movie ya FULL METAL JACKET ya mwaka 1987 kuna mziki mkubwa ndani yake, hivyo kutokana na vita hivi Wamarekani wametoa makumi ya ma movie kuhusu vita vya Vietnam, kaitafute movie nyingine iitwayo GOOD MORNING VIETNAM hii ni ya mwaka 1987 pia, kuna nyingine inaitwa AIR AMERICA ya 1990 na nyingine nyingi sana, wazee wa WAR BUS nadhani mtakuwa mnanielewa hapa.

Tukirudi katika mwendelezo wetu tunaona kuwa baada ya kuungana kwa wapinzani wa bwana Dien na mwaka 1960 huku muungano huo ukiwaleta pamoja waviet-cong wenye misimamo ya kikomunisti na wale wasio upande wowote, hao wote waliungana na kuwa kitu kimoja na hapo ndipo maneno ya muasisi wao mzee Ho chi Minh yalipotimia pale aliposema "wa-vietnam watafufuka, wataungana na kuwa mtu mmoja" note (hapa usije ukafananisha muungano huu na muungano wa vyema upinzani(ukawa) vya Tanzania, bali huu ulikuwa muungano wa vita na damu) dhidi ya Dien na Marekani.
Vita viliendelea zaidi na zaidi huku askari wa Marekani wakiongeza bidii katika mapigano bila kufumba macho, maana waviet-cong waliokuwa hawatabiriki hata kidogo.

"Askari wa Marekani ndani ya Vietnam"
Tujikumbushe kidogo jambo moja muhimu kabla hatujasonga mbele zaidi. Unajua baada ya kufa kwa kiongozi wa mwanzo kabisa wa Vietnam ya kaskazini, Bwana Ho Chi Minh, ambaye alifikwa na umauti kwa maradhi ya kawaida tu, lakini hiyo haikufanya mapambano yapoe ama kuisha bali vita viliendelea kupamba moto na hadi kufika idadi ya maraisi Watano (5) wa Marekani waliohudumu kipindi vita vikiendelea. ambapo mwanzilishi akiwa ni Rais Dwight Eisenhower alieanza kuongoza Marekani tangu mwaka 1853 na mwaka 1955 akavipokea rasmi vita vya Vietnam hadi pale alipomaliza muhula wake mwaka 1961 na kukabidhiwa bwana John F Kennedy kuwa Rais. John Kennedy ambaye alijitahidi kuongeza nguvu zaidi katika vita huku akituma zaidi vikosi 400 vya special force na maajenti wengi zaidi wa CIA , lakini safari yake haikuwa ndefu sana baada ya kufanyiwa mauaji ya kutisha ndani ya nchi yake mwenyewe, ambapo alipigwa risasi huko Dallas akiwa katika gari la waziPichani juu, ikionyesha gari la bwana Kennedy na mwili wake ukiwa chini kwenye seat ya nyuma.
pichani juu ni bunduki iliyotumika katika kuutoa uhai wa Rais John F Kennedy.
Ndani ya mwaka 1963 baada ya Kennedy kufa aliingia madalakani bwana Lyndon .B. Johnson alipokea madalaka na kuendelea na vita hivyo hadi pale mwaka 1969 alipomwachia Rais Richard Nixon ambaye pia aliongoza kwa kipindi cha miaka mitano huku vita vikiendelea na kisha mwaka 1974 akamkabidhi madalaka Rais mpya Bwana Gerald Ford ambaye alimaliza muda wake mwaka 1977 ambapo Rais Ford alimaliza muda wake huku vita vikiwa vimeisha miaka miwili iliopita. ambapo kwa ujumla vita hivyo vilichukua miaka 19 na miezi mitano (5) wiki nne (4) na siku moja (1).

Kwa kumalizia, maana bado mambo ni mengi sana kama vita yenyewe ilivyochukua muda mwingi kuisha.
Katika vita vya Vietnam Marekani na washirika wake walitumia ndege nyingi pamoja na maelfu ya helicopter, na siraha nyingine nyingi za kielectroniki.



(katika sehemu ya tatu na ya mwisho, tutaona ni aina gani ya siraha zilizotumika katika vita, sehemu za kumbukumbu, siku ya maadhimisho na ni nani alieshinda vita)
Asanteni.
La Nuit.
 
Saaaafi tunasubiri episode 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…