ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,321
- 50,541
Upepo wa mabadiliko mengi ya kisiasa na ki utawala duniani yameonekana. Yameathiri viongozi wetu baadhi. Kila sehemu ya ardhi ni kama kuna nguvu fulani naturally inashindana na nguvu fulani. Tupo kipindi kibaya sana. Mpito mgumu usio na uhakika wa kufika mahali fulani. Serikal inapoingia Mategemeo ya wengi ni kuona agenda mbalimbali kipindi cha kampeni hasa zile muhimu zinajadiliwa positive way. Tupo tunadai katiba mpya hii ndiyo Inagusa maisha ya wengi . mpaka Sasa bado kama taifa hatuelewei Nani atatuvusha katika hili. Maugomvi na kutoelewana kutatupoteza. Tupo Zama ambazo unaweza usiamini. Umaskiji kuongezeka, madawa ya kulevya kuongezeka matumizi Kwa watu wapya, ushoga kuongezeka. Hii ni kutokana na ROHO fulani asiye Penda maendeleo kuwepo MIOYONI.. Ni kama kila mtu anatafakari nini kinafuata kesho. Maisha hayapo live tena Kwa baadhi ya watu. Natangaza kuliombea taifa na Naomba mniunge mkono ntafanya maombi kila siku Kwa siku saba. Nitamwomba MUNGU afungue Fahamu za watu wengi. Wanasiasa nitawaombea muwe na fikra ya agenda za kututengenezea taifa lenye mshikamano sisi vijana wa kesho. MUNGU ameumba Galaxy, ameumba anga LA ajabu lenye nguvu za ajabu hawezi kushindwa kubadilisha akili za watanzania. MUNGU hashindwi kumwaga hekima Kwa Viongozi wake. Pande zote naziombea. Tunapenda kuona mazungumzo yenye tija kila Kona. Nchi Nzima Kusiwe na tofauti. Lengo letu liwe moja na hasa mambo muhimu. Taifa la kuombewa. ROHO za kisasi zitaharibu utulivu. Tujaribu na upande wa maombi. Tuombee Hali ya hewa