Vidokezo vya kuishi na Watu vizuri

Vidokezo vya kuishi na Watu vizuri

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,422
1.Usimwamini mtu uliyemjua ukubwani.

2.Anayejifanya ANAKUPENDA SANA chunguza upendo huo kwa makini

3.Anayekuletea HABARI fulani kasema hivi fikiria YEYE alisema nini?

4.Usitegemee mtu akatunza SIRI YAKO iliyokushinda WEWE binafsi kuitunza.

5.Muombe MUNGU sana ili akupe MACHO YA ROHONI umjue MWEMA na m'baya wako.

6.Kumjua ADUI ni kwa UWEZA wa MUNGU tu.

7.Anayekupenda kwa DHATI utamwona wakati uwapo na SHIDA.

8.Hakuna anayefurahia MAFANIKIO yako ZAIDI ya WAZAZI wako na MUNGU tu. Ukikutana na mtu wa namna hiyo ujue ni mzazi wako.

9.Mthamini na kumjali kila ALIYECHANGIA WEWE KUFIKA HAPO ULIPO. Uwe na baraka tele zitakazo kupa AMANI na UTULIVU
 
ujumbe mzuri lakini sioni kama unaendana na heading. labda ungesema ukinunua nyama hakikisha watoto wa jirani hawajui hapo ningekuelewa
 
Nazjaz, miungu ikubariki kwa andiko hili jema...
 
Last edited by a moderator:
1.Usimwamini mtu uliyemjua ukubwani.
Hii ni sentensi tata. Watu wengi nakutana nao ukubwani, na imani kwa mtu yategemea na jambo husika...kama utekelezaji wake wahitaji imani ya mtu mwingine au la. kwahiyo binafsi naona huu ni muono wako ambao kwangu si sahihi.

2.Anayejifanya ANAKUPENDA SANA chunguza upendo huo kwa makini
Ukisema "anayejifanya" unamaanisha ulishapima na kujua kuwa si mkweli, basi ni vyema kuachana naye...kwani kuendelea kukubali kupendwa naye yadhihirisha udhaifu wa maamuzi yako. Sahihi kuchunguza mapenzi yote kwa makini.

3.Anayekuletea HABARI fulani kasema hivi fikiria YEYE alisema nini?
usiishi kwa kujihisi katika kila jambo. Ingekuwa hivi basi hata vyombo vya habari tungevijengea fikra mbovu kuwa kama vyatupa habari fulani kuhusu jambo au mtu fulani...navyo vimepewa nini au kutusema nini kabla ya kutoa habari husika??? Sahihi ni kupima habari husika, kama ina mashiko-sawa, haina mashiko-weka kapuni.

4.Usitegemee mtu akatunza SIRI YAKO iliyokushinda WEWE binafsi kuitunza.
si sahihi kwani siri yako(binafsi) ni tu ikiwa nawe binafsi. Ukimwambia mtu kitu ulichoweka siri basi siri hugeuka kuwa taarifa na haiwi na sifa ya siri yena. Siri binafsi ibaki kuwa binafsi...ukimwambia mtu, hiyo sio siri tena.

5.Muombe MUNGU sana ili akupe MACHO YA ROHONI umjue MWEMA na m'baya wako.
Muombe Mungu akujalie utashi wa kupembua yaliyofaa na kuepuka yasiyofaa. "macho rohoni" si sahihi.

6.Kumjua ADUI ni kwa UWEZA wa MUNGU tu.
Kumtambua adui, ni kwa utashi na tafsiri binafsi tuliojaliwa na Mungu(kwa wenye imani tu)

7.Anayekupenda kwa DHATI utamwona wakati uwapo na SHIDA.
Si sahihi. Wapo waliozaliwa na kukua katika raha(hawajui shida). Sahihi ni, rafiki wa dhati utamjua wakati wa uhitaji.

8.Hakuna anayefurahia MAFANIKIO yako ZAIDI ya WAZAZI wako na MUNGU tu. Ukikutana na mtu wa namna hiyo ujue ni mzazi wako.
Hapana, kwa maana halisi ya mzazi ni yule aliyekuzaa na si vinginevyo. Hizo nyingine ni tafsiri ambazo kwangu binafsi si sahihi. Huwezi kuniambia mtoto mdogo(jirani labda) anipongezae na kufurahia mafanikio yangu ni mzazi wangu-sio sahihi.

9.Mthamini na kumjali kila ALIYECHANGIA WEWE KUFIKA HAPO ULIPO. Uwe na baraka tele zitakazo kupa AMANI na UTULIVU
kama tu nina iman, vinginevyo ni kazi bure
 
Kutafuta kanuni za kuishi na binadamu mim naona ni kujipa tabu zaidi. Bora kutafuta kanuni ya kuishi na pesa.

Ishi upendavyo na si watakavyo.
 
Sikubaliani na # 1 & 2, naona kama umebugi step. Unataka kujua kwanini.......

#1 - Ulishawahi kusikia ndugu wa tumbo moja au mapacha wanachukiana, eti huyu nae mlijuana ukubwani
#2 - Ulishawahi sikia true love, unconditional love.... mapenzi ya aina hii haihitaji sababu.
 
Mkuu sijajua source ya hii thread yako,ila naomba nikukosoe hapo kwenye namba 8.

Hapo nadhani mkuu umetumia tu kukariri au mazoea kusema hivyo,maana ukiacha MUNGU na WAZAZI bado kuna watu wengi sana wanaofurahia mafanikio yetu.
 
Hapo 8 & 9, Mkuu umetoboa mule mule...yan umeongea madini matupu.

Pia utagundua kama uliwahi kua na dem/mpenz mkapendana sana mkiwa below 20 ( teenage years) ni ngumu sanaa kusahauliana hata kama mli split. Iko hvyo kwangu. Trust me.
 
Mkuu sijajua source ya hii thread yako,ila naomba nikukosoe hapo kwenye namba 8.

Hapo nadhani mkuu umetumia tu kukariri au mazoea kusema hivyo,maana ukiacha MUNGU na WAZAZI bado kuna watu wengi sana wanaofurahia mafanikio yetu.

kama wanapenda bas jua bado we haujafanikiwa. ukifanikiwa utaona maadui zako. ukitaka kuwaona vizuri, uwe juu halafu udrop.
 
Hii thread yako imejaa kasoro na makosa,
pengine utuambie, ni fikira zako ama umesoma mtandaoni?
 
Back
Top Bottom