The Bourne
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 1,077
- 1,322
VIDOKEZO MUHIMU VYA AFYA NA USALAMA.
[HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] Hisani ya kumaliza mwaka 2017.
[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
1. Pokea simu kwa kutumia sikio la kushoto. Zungumza na simu mara chache na kwa muda mfupi, tumia zaidi ujumbe mfupi kwa mawasiliano yasiyo ya lazima. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000. Tenga majira ya kutumia simu yako, mara zingine izime kabisa na pumzika.
2. Usinywe dawa (vidonge) kwa kutumia maji baridi. Na usinywe dawa (vidonge) kama hujaelekezwa na daktari. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku, ukiweza usinywe maji baridi kamwe kwenye maisha yako.
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni. Usile chakula na kunywa maji kwa wakati huo huo. Usile chakula kingi kwa wakati mmoja. Usile chakula harakaharaka. Na kwa wasiojua, kula si jambo la ratiba ya lazima, kama mathalani husikii njaa, tafuta matunda na vimiminika vyenye afya, vitumie kisha lala. Usiende mezani kula JUST because watu wote wanakula.
4. Unapokuwa na hasira kunywa maji haraka, kisha ukiweza, ondoka eneo hilo na rudi baadaye. Unapochokozwa au kutukanwa, ondoka eneo hilo haraka, siyo WOGA, ni ushujaa. Je, unafahamu kuwa wachokozwaji wengi sana wako MAGEREZANI au makaburini kwa sababu tu walitaka kuoneshana umwamba na wachokozaji?
5. Muda bora wa kulala ni kuanzia saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri. Panga ratiba zako saa hizo uwe kitandani. Lala saa 8 kwa siku. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku kula chakula laini. Lala kwenye godoro imara na lisilo na "mashimo" au mibonyeo.
6. Unapotembea barabarani kwa mguu, usitembee upande sawasawa na uelekeo wa vyombo vya moto. Zinapotokea dharura au ajali za ghafla, wanaookoka mara nyingi huwa ni watembea kwa mguu wanaotembea uelekeo wa kupishana na vyombo vya moto. Mtu anayeiona gari ikipoteza mwelekeo ndiye hupata muda wa kufikiri afanye nini kuliko yule ambaye anastukia amegongwa na gari ikitokea nyuma yake.
7. Unapofanya kazi, kila baada ya saa 1, pata muda wa kusimama na kunyoosha viungo, tafuta maziwa FRESH na kunywa maji ya kutosha. Usifanye kazi NON Stop kwa sababu unajiua. Hakuna TUZO ya mfanyakazi bora ambaye hakuwa ananyoosha mgongo na kuuweka mwili wake salama. Kazi yako inakupenda lakini mwili wako ndiyo unatunza uhai wako.
8. Watoto wako au mtu mwingine (nyumbani na ofisini) wanapokuuliza kitu, mwangalie usoni, acha kuangalia simu, mjibu mhusika huku akiona kuwa unajua unachomueleza. Wanafamilia wengi sana, na hasa watoto hujenga ukatili na kutojali kwa kadri wanavyoumizwa na kukosekana kwa hali ya kujali kutoka kwa wazazi.
9. Unapovamiwa na watu wenye silaha wakitaka kukupora mali zako, usishindane nao, tii maelekezo yao. Hujui watu hao ni kina nani, wana silaha gani na uwezo gani. Sekunde moja tu ya kufanya lolote inaweza kukukuta ahera. Watu wa namna hiyo huhitaji mali kuliko uhai wako, waachie mali kisha linda uhai na omba msaada kwa raia wema baada ya tukio.
10. Kamwe usishike simu yako ukishakaa kwenye usukani wa gari. Sekunde moja tu ya kutizama simu = vifo vya makumi ya watu walioko ndani na nje ya gari. Kama ni lazima uzungumze, pokea simu kwa kutumia vipokeleo (earphones) ambavyo viko automatiki masikioni (unaweza kuvibonyeza kwa mkono wa kushoto na ukazungumza huku akili na macho yako vikiwa barabarani).
Compiled from Security and Health Websites.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].