VIDEO: Waziri wa Magufuli ampigia salute G. Lema bungeni

Lazima nikiri kuwa nimeanza kumpenda huyu Waziri wa Viwanda kwa ufanyaji wake wa kazi.

Ni mtu ambaye anaweka Taifa mbele. Akiambiwa jambo la maana analikubali hapohapo hata kama limetoka kwa upinzani. Natamani viongozi wengi wangelikuwa kama huyu jamaa.

Kitendo alichomfanyia Lema ni nadra sana Watawala kufanya hivyo. Heshima sana kwako Mheshimiwa Waziri wa viwanda na biashara. Maadamu ndiyo kitendo ambacho Rais Magufuli anakisisitiza kila siku basi naamini Rais na serikali yake itafanikiwa kujenga misingi mizuri sana ya kiuchumi.
 
Lazima nikiri kuwa nimeanza kumpenda huyu Waziri wa Viwanda kwa ufanyaji wake wa kazi.

Ni mtu ambaye anaweka Taifa mbele. Akiambiwa jambo la maana analikubali hapohapo hata kama limetoka kwa upinzani. Natamani viongozi wengi wangelikuwa kama huyu jamaa.

Kitendo alichomfanyia Lema ni nadra sana Watawala kufanya hivyo. Heshima sana kwako Mheshimiwa Waziri wa viwanda na biashara. Maadamu ndiyo kitendo ambacho Rais Magufuli anakisisitiza kila siku basi naamini Rais na serikali yake itafanikiwa kujenga misingi mizuri sana ya kiuchumi.
MCHANGO WA LEMA NI WA MAANA SSANA ILA SIJAJUA MAGUFULI KAMFANYIA NINI?
 
Ingekuwa kwenu UKAWA mngemwita msaliti
Usikariri ukawa tu, jaaribu kuchangia kilichoongelewa... kwa sasa naweza sema JPM amewasafisha baadhi ya wananyinyiem kwa kuwa awali nilikuwa nawaona wote akili sawa .. kumbe wapo ambao bado hawajawa vibaya kama wengine walio wengi.
 
Tujifunze kukubaliana kwenye issues za msingi za kitaifa. Uzalendo si chama chako kushinda bali Tanzania kuwa taifa bora. Tatizo umeingia ugonjwa wa kupiga siasa kwenye kila kitu ...kizuri au kibaya lazima zitafutwe political mileage ...hatuwezi kuendelea namna hii .
 
Mkuu kati ya Mawaziri waadilifu katika serikali ya awamu hii ni huyu.Kuhusu mambo ya usaliti ni kwasababu watu sasa siasa wamefanya kama ushabiki wa Simba na Yanga.Si CDM wala CCM,kitu ambacho ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu,wewe mwenyewe ni mmojawapo.

umeona eh! shabiki nambari moja
 
Huyu Lema kuna watu wanamuona hamnazo sababu ya vijembe na attitude yake, lakini ni moja ya wabunge wa upinzani ambaye akichangia kama unazingatia uzito wa hoja zake unaweza kupata mambo ya msingi sana. Lakini pia huu ndio upinzani wa kweli, unakosoa serikali na kutoa mawazo mbaadala.
 
Ni vizuri kuona wapo watu wana~fight back maana hii nchi sasa hivi inapelekwa kiholela watu wanashangilia kwa kua wanajua Mafuguli yupo juu ya kiti.

Ukweli ni kua inaenda pabaya mno, hakuna mjinga atataka kuja ku~invest Tanzania sasa hivi kwa jinsi ambavyo serikali inaingilia sekta binafsi ovyo, kwanza wanakaa kupangia bei watu which is plain nonsense, na kila siku nalaumu humu kua ile kauli ya Rais ati "kamata kwanza alafu tutafix errors baadaye" ilikua ni mbaya, sasa leo hii sukari zimekamatwa kila kona, watu wanatoa tu amri bila kufikiria, ilimradi kaona ghala tu lina sukari nyingi anasema imefichwa, anaita askari fasta, no questioning wala kufanya uchunguzi. Mwisho wa siku tunaona matokeo yake, sasa hivi serikali inabidi itoe pesa kurudisha sukari za watu walipozitoa baada ya kugundua kua zilikua ziko pale kihalali. Tena ingekua ni mimi ningefungua kesi kabisa mahakamani kudai fidia, sukari wangerudisha na wangelipa milioni mia kadhaa juu yake kunipotezea muda.

Rais anaweza kua na nia nzuri, lakini vitu vinatakiwa vifanywe polepole baada ya kufikiria na kujaribu kupima na kujua effect zake huko mbele ni zipi, na kuhakikisha kila step inafuata sheria, kujaribu kua juu ya sheria ni kosa moja kubwa sana, mtu anayekuja kukunyang'anya mali zako hana hata karatasi kutoka mahakamani kua karuhusiwa, ukimpiga risasi akulaumu nani? Maana wewe unafata sheria, unajilinda, yeye kaja hajafata sheria yoyote. Hawa wakuu wa wilaya, mikoa, sijui wametolewa wapi, bora wapangwe upya, hata kusoma na kuandika tu shida, kila mtu anakaa kutoa order tu ovyo na kualika waandishi wa habari aonekane anafanya kazi, yaani kalala kaota fulani ni mwizi, anamrukia fasta! hehehe duh! hivi kweli sisi watanzania ni stupid kiasi hicho?

TCRA ovyo, TAKUKURU ovyo, kila sekta ovyo, hadi hawa nao BASATA ovyo ati nao wanatafuta kiki siku hizi kila msanii anafungiwa tu, hehehe! Kila nikifikiria kuregister kampuni yangu bongo moyo unagoma unanambia niiache tu huku ilipo hata tax nalipa ndogo kuliko ambayo nitalipa huko na serikali ya watu hainiingilii, ningependa sana kuona Tanzania inaongozwa na watu smart na sio waliopo sasa hivi wazee wa kiki.
 
Back
Top Bottom