Wanasayansi wa JF, Msaada wenu please!
Nataka kufungua studio yangu ya video na photo production. Ninunue vifaa gani kwa kazi hii?
Naombeni mnisaidie jamani.
1. Kompyuta nzuri kwa kazi hii ni yenye sifa zipi?
2. Kamera nzuri ni ipi?
3. Na hiyo printer iwe vipi?
Note: mimi ni mjasiliamali naetaka kutoka kwa njia hii nahitaji vifaa na technology ambayo ni affordable.
1. Computer nzuri - Kazi za video production na photo editing zinahitaji kompyuta nzuri ambayo inaweza kufungwa software za editing na zikafanya kazi vizuri, software hizi huwa na minimal requirements za hardwares i.e RAM na PROCESSOR. Kama unapanga kununua desktop used basi jiandae ya bei kuanzia laki 3 na nusu na kuendelea na kama ni mpya jiandae ya kuanzia milioni 1 kwenda juu. Ukihitaji nitakupeleka dukani.
2. Camera nzuri - Utahitaji kamera nzuri inayoweza kuchukuwa picha kwenye high definition, picha au video nzuri. Kuna kamera jua likiwa linawaka huwezi kupata picha nzuri kumbe kuna zingine hata ukipiga kuli-face jua la saa nane mchana bado picha itatoka safi, zipo baadhi ya kamera zinafanya editing zenyewe yaani ukishapiga picha unaweza kufanya baadhi ya editing kama vile kupunguza ukubwa wa picha, kui-crop picha, kuongeza effects nk. Sikushauri camera used kwa kazi hii lakini kamera mpya ya kuanzia laki 2 na nusu mpaka milioni 1 na nusu inafaa kwa kazi hii.
3. Printer nzuri - Utahitaji ku-print picha zako. Unahitaji kupata printer ambayo ni multifunctional inayoweza kuprint karatasi za kawaida, karatasi za picha, photocopy, na pia iwe ina print cd/dvd covers directly. Unahitaji printer ya kuanzia laki 3 na nusu na kuendelea.