Kuna msemo unaosema kuwa, ukijibishana na kichaa na wewe unakuwa ni kichaa. Kwa maana nyingine, ukijibishana na "mpiga porojo" na wewe unakuwa ni "mpiga porojo".
Kwa viongozi wa CHADEMA kama wanavyopenda wananchi waamini, Nape Nnauye ni "mpiga porojo" lakini katika "porojo hizo", wanatumia nguvu kubwa katika kuzijibu. Kwa sisi tunaoangalia kwa mbali tunaachwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu zaidi ya kurudi kwenye usemi wa mwanzo na kuwa na hitimisho kuwa basi hata viongozi wa CHADEMA nao ni "wapiga porojo" (manzi ga nyanza) na kama sivyo, basi inawezekana maneno ya Nape Nnauye yakawa yamebeba ukweli ndani yake mpaka kufikia kujibiwa kwa nguvu na viongozi wa chama kinachotaka watu wakiamini kama ni makini katika utendaji wake (damage limitation).
Kama hivyo vyote vipo, basi siasa za Tanzania zina kansa ambayo inatakiwa "amputation" ndani ya fikra za wananchi kwa sababu nchi haiwezi kujengwa kwa porojo za kisiasa kama hizi bali kwa fikra malidhawa na zenye maono ya kukabiliana na changamoto za karne hii ya sayansi na tekinologia.