VIDEO: Mwili wa Kawawa ukipakiwa ndani ya gari

Hivi hii ni mila yetu au Muhimbili kukosa organization?

Au kukosa organization ndiyo mila yetu?

Mbona naona kama ilikuwa shaghalabaghala tu?

Kama huu ulikuwa ni muda wa familia, basi waandishi wa habari wangeheshimu hilo na kutopiga picha hizi.

Kama hii ilikuwa ni katika muda wa kumuaga Kawawa publicly, bsi kungekuwa na organization yenye heshima zaidi.

I mean this is goddamn Kawawa for atoms sake, where is the dignity? Hamna hata viaskari njaa vya uongo na kweli ku control watu? Hamna hata kijia cha utepe kuenzi umuhimu wa huyu bwana?
 
sinkala-albums-sinkala-picture813-flag4.gif
 
Kiukweli sikupendezwa na utaratibu huo, ni kama mabo yalifanywa vululuvuluu tu!! Mzee ni mtu na heshima zake kwa tz sasa huu utaratibu gani!!!!

R.I.P Mzee K!!
 
Ndugu zangu waislam napenda kuwahuswia pamoja na kuihuswia Nafsi yangu katika kumcha Allah na kufata maamrisho yake na kuacha yale aliyokataza.

Nikirejea katika Quran imeweka wazi kabisa kuwa sisi ni Umma Bora sana na sababu za sisi kuwa Umma bora ni tatu tu. 1. Tunaamrishana mambo mema 2. Tunakatazana mambo mabaya 3. Tunamuamini na kumtwii Allah Subuhanau wataala.

Nawahuswia Muweke Husia.

Ni lazima mjue mambo muhimu kwa maiti wa kiislam. Mola amesema bayana Mtu anapofariki tu tunatakiwa haraka sana kumzika.

Kumbukeni Shart za maiti wa kiislam ni
1. Kumfunika (kumsitiri) pale anapofariki tu
2. Kuoshwa
3. Kuvikwa Sanda.
4. Kulipa madeni yake na kupokea zile anazodai ( kuwakabidhi wadeni/ wadaiwa kwa mtu maalum katika familia)
5. Kumswalia.
6. Kuzika.

Hakuna kipengele katika Dini kinachosema kuwa kuna issue ya Kuaga maiti. Huo ni UKRISTO MTUPU na tutaangamia kwa mambo haya ya kuiga ukristo.

Hakuna mambo ya kuchanganyika wanaume na wanawake katika misiba hususan kuaga au hata kwenda kuzika.

Mungu atunusuru sana na mambo haya ya kinaswala.

Nawahusia muweke Usia msije fanyiwa mambo kinyume.

Dr Hamza Yousuf Al nammani
Doha
 
HIvi naomba kuuliza, Kwnye Qurhan kuna kipengele chochote kilicho jua siku za mbele ? labda kutaja kuhusu technology ya Ndege za Abiria, magari ya petroli , umeme ,simu , computers ,friji au chochote cha technolgia kilicho siku za sasa? Asante
 
Hizi dini bado zina mambo ya kizamanizamani sana. Kwa mfano zote haziruhusu matumizi ya condom kwa kinga ya magonjwa mbali mbali au uzazi wa majira. Hadi hii leo zote hazina mapadri au masheikh Wanawake. Wengine huwatenga waumini wao eti kwa kuachwa ndani ya ndoa na hawaruhusiwi kuoa tena. Sasa jamani kijana/binti wa miaka 25 ambaye ameachana na mwenziye kweli viongozi wa dini wanategemea mtu kama huyu atakaa miaka yote ya uhali wake iliyobakia bila kula tunda kweli!? Sasa kama haruhusiwi kuoa/kuolewa huku si kukaribisha uzinzi kwa mfuasi kama huyu?

Kawawa alikuwa ni miongoni mwa Watanzania walioshika nyadhifa mbali mbali za juu sana ndani ya nchi yetu. Kuagwa na Watanzania wenzake ambao tulithamini sana mchango wake kwa Taifa letu ukilinganisha na hawa waroho tuliowapata kuanzia awamu ya pili hadi hii leo kuna ubaya gani? Hivi mwili wake ukiwekwa mahali bila kufunuliwa ili Watanzania tumuage kwa mara ya mwisho kuna dhambi gani hapo?

Kuna mambo mengine katika hizi dini yamepitwa na wakati sana.

Friday Jan 01, 2010

01_10_jjqxh9.jpg

PRESIDENT Jakaya Kikwete and First Lady, Mama Salma Kikwete pay last respects to the body of Former Vice President, Prime Minister and veteran politician, Mr Rashid Mfaume Kawawa at Karimjee Hall in Dar es Salaam today in the afternoon.
 
Hivi hii ni mila yetu au Muhimbili kukosa organization?

Au kukosa organization ndiyo mila yetu?

Mbona naona kama ilikuwa shaghalabaghala tu?

Kama huu ulikuwa ni muda wa familia, basi waandishi wa habari wangeheshimu hilo na kutopiga picha hizi.

Kama hii ilikuwa ni katika muda wa kumuaga Kawawa publicly, bsi kungekuwa na organization yenye heshima zaidi.

I mean this is goddamn Kawawa for atoms sake, where is the dignity? Hamna hata viaskari njaa vya uongo na kweli ku control watu? Hamna hata kijia cha utepe kuenzi umuhimu wa huyu bwana?

Je una habari jinsi ilivyokuwa wakati wa kumpokea Sokoine pale Morogoro hospital baada ya ajali. Je, baada ya kuthibitisha kifo cha Sokoine una hakika kwamba haikuwa hivihiv wakati wa kumpandisha kwenye ndege ya jeshi kuupeleka Dar.
 
Back
Top Bottom