VIDEO:Mpangilio wa malazi kwa kutumia kontena

oel200e

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
276
118
Habari, nimetengeneza video hii kuonesha japo kwa Ufupi, namna ya kutengeneza malazi kwa kutumia kontena (shipping container) la futi 40.Kwa hapa nimetumia wakazi kama ni wanafunzi.
Hii hapa;
 
Habari, nimetengeneza video hii kuonesha japo kwa Ufupi, namna ya kutengeneza malazi kwa kutumia kontena (shipping container) la futi 40.Kwa hapa nimetumia wakazi kama ni wanafunzi.
Hii hapa;

vp unaweza kutengeneza kwa nyumba ya kuishi mtu (yaan nyumba ya kifamilia) siyo bweni kama hilo na vp kuhusu joto kama inawezekena weka mfno video
 
Inawezekana kabisa...kuhusu joto hakuna Shaka kwa sababu kwanza kuna kuta za ndani nyembamba (insulator) kwa ajili ya kupunguza joto...lakini Pia kuna almost 40% ya uwazi wa madirisha na mlango...kama haitoshi, aina ya madirisha na mlango ni louvre ambayo huzuia mwanga na kuruhusu upepo muda wote
 
kwa Tanzania utaliweka wapi hilo Container wakati wenzako viwanja vinauzwa?
km ni Mabwepande bora jenga nyumba ya kudumu hata ya tope iwe na madirisha yenye hewa na tembe zetu hazina joto kabisa
ukiangali hizo Clip inaonesha hata hizo nyingine si za Nchi zetu za afrika zenye ardhi tosha
 
Inawezekana kabisa...kuhusu joto hakuna Shaka kwa sababu kwanza kuna kuta za ndani nyembamba (insulator) kwa ajili ya kupunguza joto...lakini Pia kuna almost 40% ya uwazi wa madirisha na mlango...kama haitoshi, aina ya madirisha na mlango ni louvre ambayo huzuia mwanga na kuruhusu upepo muda wote
tengeneza mfano ulete kwa video araf useme bei gani
 
Kazi nzuri mkuu ume design na umetumia nafasi ya ndani vizuri - pia umeweka madirisha makubwa ambayo yatasaidia mzunguko wa hewa na kusaidia kupunguza joto na kuingiza mwangaza, choo umekiwaka pahali pazuri pia na presentation yako ni nzuri sana - keep it up na jitahidi
 
tengeneza mfano ulete kwa video araf useme bei gani

hivi na wewe unadanganyika na kazi za ku-copy na ku=paste
hayo Macontainer na ya kwetu ninachozungumzia ardhi ya kwetu ni kubwa achana na Macontainer
Nimemaanisha mleta Mada hawezi kuja na la ziada zaidi ya hizo clip za YouTube
 
sijakuelewa aisee hata punj8e !
ebu changanua maneno yako vizuri copy- paste hayo makontena ya kwenu araf
ardhi ya kwetu kubwa then niachane na makontena
sijakuelewa
 
sijakuelewa aisee hata punj8e !
ebu changanua maneno yako vizuri copy- paste hayo makontena ya kwenu araf
ardhi ya kwetu kubwa then niachane na makontena
sijakuelewa
mm nimejibu post #1 ya mleta Mada kuwa si yeye aliyeitengeneza ila amecopu YoiTube
ww unataka nikuletee ya nyumba nzima tena nitengeneze clup ndio nikasema hiz habari waachieni wazungui waliokosa ardhi hebu fuatilia mtiririko wa post wala si nyingi utajua nilimjibu nani?
 
Mkuu una hakika kwamba nimecopy clip ya YouTube?...em fuatilia hiyo channel uone kama jina la account kama it's not belong in Tanzania (done by Studio Tanzania). Hakuna maajabu katika design wala utengenezaji wa video hii, haya mambo yanasomwa hapa tanzania kama tu nchi zingine.
Tuache dharau, Architecture ipo hapa tanzania na ni elimu ya miaka takribani mitano hapo chuo kikuu Ardhi.Tupo watanzania wengi wenye uwezo wa kufanya vizuri tu kama hao unaowaona kwamba ndio Wanajua zaidi.

Kuhusu suala la Ardhi, unafikiri watu wangapi hapa Dar es salaam wanamiliki Ardhi?, kwa takwimu ya miaka mitatu tu iliyopita inaonesha Dar ni jiji la Tatu kwa ukuaji Afrika , ni wazi haiwezekani kila mtu kumiliki Ardhi ya kutosha kwa vipato vya sasa.Labda nje ya jiji la Dar, lakini je wangapi wanaishi nje ya jiji hili na kuwa na uwezo wa kuja mjini kila siku kufanya kazi, au kielimu?..
Umewaza ujenzi wa nyumba pia?....kwa sasa ghrama ya nyumba hapa dar inaenda kwa rate ya laki 7 na hamsini elfu, (inaendelea kukua) je unadhani watu wa kipato cha chini watajenga lini??...je umewafukiria vijana ambao wanaanza maisha tu na wangependa kujishikiza sehemu ya gharama nafuu mpaka watakajiwezesha?..mfano hii ni proposal nime-design kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo wanaohangaika na hostels...je na wao pia wanataka viwanja wajenge kipindi cha masomo yao??

Kontena moja ni million 7 (futi 40 urefu) matengenezo ya ndani hayazidi mil 4....wapi hapa Dar utajenga kwa mil 10?.alafu hiyo nyumba iwe na uwezo wa kuhamishwa kwa wakati..mfano bomoa bomoa za kupisha shughuli nyingine za ki uchumi.

Suala la msingi ni kwamba, ni wakati umefika tukubali kwamba kila makazi yanategemea na kipato cha mtu, lakini suala la kuishi sehemu nzuri ni haki ya kila mtu bila kujali rika wala kipato chake.
 
Idea nzuri mkuu.ila kwa joto la Dar, AC ni must.

AC si lazima mkuu, kwa bahati mbaya makazi yetu mengi yamefanyiwa design kiholela lakini kiukweli kuishi bila AC inawezekana.

Ukiangalia vizuri utaona kwamba, kiwango cha maeneo ya wazi (yaani madirisha na Milango) katika design ni almost 40-50% ya kuta za kontena.kulingana na uwelekeo wa jua na aina ya kuta ndogo za ndani (insulators) na uelekeo wa upepo inawezekana kabisa kukaa bila AC.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom