Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wakuu
Wananchi wa Arusha walifunga barabara kwa mawe wakipinga hali mbovu ya miundombinu, huku wakimtaka kiongozi wa TARURA, Vickey Chisoma, aseme ukweli kuhusu changamoto hiyo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Tukio hilo limeibua taharuki baada ya wananchi kugomea polisi waliokuwa wakijaribu kufungua barabara, wakisisitiza kuwa hawataondoka hadi suluhisho la kudumu lipatikane. Wakiwa na hasira, baadhi yao walipaza sauti wakisema, “Nakubeba, tuondoke wote,” wakimaanisha kuwa viongozi wa TARURA wanapaswa kuwajibika ipasavyo.
Wananchi wa mtaa wa Nado Kati, kata ya Muriet, mkoani Arusha, wameandamana na kufunga barabara inayotokea East Africa kuelekea Nadosoito, wakilalamikia ubovu wa miundombinu hiyo. Wanasema barabara hiyo imekuwa kikwazo kikubwa hasa wakati wa mvua, ikisababisha mafuriko yanayowazuia kufanya shughuli zao za kiuchumi na watoto kushindwa kwenda shule.
Wananchi hao pia wamemlalamikia mkandarasi wa mradi huo kwa kuchelewa kufanya ukarabati wa barabara, wakidai kuwa kazi yake haiwaletei matokeo yanayotarajiwa, huku wakimuomba kiongozi aliyewaita wananchi wajinga aombe msamaha na alitii hilo kiongozi huyo.
Ofisa kutoka TARURA, Vikey Chisoma, alifika katika eneo hilo na kueleza kuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi ndiye aliyekwamisha mchakato wa ukarabati. Hata hivyo, wananchi hawakuridhishwa na maelezo yake, wakimuita muongo na kushinikiza hatua za haraka zichukuliwe ili barabara hiyo iweze kurekebishwa ipasavyo.