Video: Maisha ya Ughaibuni na Pigabox

Duh! Hivi hawa jamaa wanakuwaga na elimu gani mpaka wakafanye kazi za wasiosoma?
 
kama anayeifanya karidhikanayo,na ni kazi halali,wewe kinakuuma nini?PILIPILI USIOILA..........
 
Ukifanya kazi huku...hata iwe kazi gani...unalipwa na unaishi maisha yako vzr...ndo tofauti na huko unaweza kuwa hata maneja branch lkn madeni kibao na utapeli utapeli tu...ndo tofauti kubwa sana hiyo..na huku km akili yako ni nzuri unakua na displin na maisha na hela unayoipata
 
Si bora wabebe box kuliko kuwa mapunda! Afu wanapataga mi-dollar mingii!
 

Waambie hao
Tatizo wabongo tuna dharau sana hatutaki kufanya kazi wenzetu wanapiga kazi na fursa ni nyingi na hakuna rushwa huyo mbeba mabox ukienda kwake anamaisha bomba sawa tu na huyo tajiri aliyeko bongo na pengine akiwa bongo hana mbele wala nyuma rushwa kibao.
 
Ni kweli shansarie..kitu nlichogundu na kinacho nifurahisha ni kwamba kwanza huku unajifunza kupata kipato kwa kufanya kazi...hakuna rushwa hakuna nini..hakuna kujuana..na ukifanya kazi unapata kipato unakula, unapata hela ya kulipia morgage..unaiendesha familia vzr..unapanga mipango yako vzr...stress ni kazi tu...kuna notion ambazo wabongo wanakua nazo si za kweli kabisa...ila kweli ukija na usistadu na ubrazamen wa kibongo bongo maana sisi wabongo showoff nyingi kweli maisha utayaona magumu
 
kama anayeifanya karidhikanayo,na ni kazi halali,wewe kinakuuma nini?PILIPILI USIOILA..........

We vipi?acha kukurupuka,nani kasema inaniuma? Hata akiamua kuzibua vyoo ni kazi yake halali vyote sawa lakini hilo haliwezi kunizuia mimi kuhoji.
 
Hata wenyeji wanazifanya hizo kazi na wengi wao wamesoma sana. Usishangae dereva wa taxi ana PhD!

Mkuu kwa hiyo anakuwa na Phd ya mambo ya udereva wa tax au anaamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha/ajira?
 
Mkuu kwa hiyo anakuwa na Phd ya mambo ya udereva wa tax au anaamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha/ajira?
Huko kazi yeyote inaheshimiwa sana, na mshahara anaoupata huwezi ukalinganisha na pesa za madafu. Huoni jamaa kwenye video anasema kuwa watu wa nyumbani wakiona western union pesa zinakuja ni kazi hizi? Watu wananunua nyumba ughaibuni na kujenga nyumbani kwa kazi hizo.
 

Kweli kabisa ngoja nikabebe mabox yangu mie as long as mwanangu anasoma shule ya maana aka sina tabu hao wanaotunanga acha waendelee kuuza kahawa vibarazani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…