VIDEO: Kijana Omar Ramadhani, amuombea Rais Magufuli viwanja vya Sabasaba

OGTV

JF-Expert Member
May 22, 2016
353
167
Rais Magufuli apiga picha na mtanzania baada ya kuvutiwa na dua zake, mtanzania huyo akamuombea kwa dua takatifu.

View attachment 364450
CmXqTndXYAAKvpk.jpg

Kijana Omar Ramadhan akimsalimia kwa furaha Rais Magufuli kwenye viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar


Kila mtu huwa na hisia tofauti juu ya jambo fulani katika Maisha yake. Na kila mtu huwa na uwezo tofauti katika kukabiliana na hisia, wakati mwingine unaweza kujikuta umefanya jambo ambalo hukulitegemea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli alijikuta akiwapa wakati mgumu walinzi wake baada ya kuwashtukiza, pale alipomwambia Kijana Omary Abdallah Ramadhani Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam aje kupiga picha na Rais baada ya kijana huyo kusikika kwa mbali akimuombea dua.

Tukio hili lilitokea siku rais Magufuli alipokuwa akitembelea Maonesho ya Sabasaba jijini Dar Es Salaam Julai Mosi 2016.
 
RAIS MAGUFULI APIGA PICHA NA MTANZANIA BAADA YA KUVUTIWA NA DUA ZAKE, MTANZANIA HUYO AKAMUOMBEA KWA DUA TAKATIFU.

SAMAHANI KWA KUKOSEA ILA VIDEO HIYO HAPO.
 
Hahahaha Lowasa akiiona hii roho itamuuma sana naye atakwenda sababa kuangalia kama atapewa dua...
 
Back
Top Bottom