Mhabarishaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2010
- 1,007
- 601
Tarehe 2.8.2014, Askofu Mkuu Zachary Kakobe aliongoza maandamano ya kusherehekea miaka 25 ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (1989-2014). Maandamano hayo yaliyojulikana kama "Matembezi ya Shukrani" yamekuwa gumzo kubwa katika Jiji la Dar-es-Salaam kutokana na umati mkubwa wa waumini wa Kanisa hili kutoka kote nchini walioshiriki maandamano hayo, na zaidi sana kutokana na kuonekana hadharani kwa Kakobe ambaye alizushiwa kwamba alitoroka nchini na eti "aliliuza Kanisa lake".
Last edited by a moderator: