Video: Je, Bunge la Afrika Mashariki linatumia lugha ipi kwa mawasiliano?

BENNICK

JF-Expert Member
May 2, 2013
633
864
Nilikuwa nikipita huku na kule nikakutana na kipande hiki cha video, mmoja wa wagombea wa Bunge la Africa mashariki akiomba kura. Jamaa kamix kiingereza na kutimka fasta. Nikajiuliza maswali mawili.
1.Lugha rasmi inayotumika kwenye bunge la Afrika mashariki ni ipi?
2.kama lugha inayotumika kwenye hilo bunge ni English, baadhi ya wabunge wetu wataweza kutuwakilisha ipasavyo.?
 
Attachments

  • VID-20170409-WA0001.mp4
    417.8 KB · Views: 28
..inabidi uende kwenye RECORDS kuona wabunge waTz wanashiriki kwa kiasi gani ktk mijadala ya Bunge la Afrika Mashariki.

..inawezekana tuliwatuma kwenye bunge hilo wanadhuria vikao lakini hawachangii au kushiriki ktk mijadala.
 
Lugha rasmi ya Bunge la EAC ni English ingawa nasikia tutaanza kutumia na lugha ya kiswahili. Ukiangalia hiyo video unapata mawazo mengi na kujiuliza kama huko CCM kuna wabunge wanao ipenda Tanzania. Na swali jingine unajiuliza kama wana akili sawa ktk vichwa vyao.
 
Binafsi yangu naona kunashida kwenye lugha ya malkia hasa kwa hawa what so called engineeers!!
Yaan hawa jamaa sijui tuwapeleke kwa Ras Simba??
Huyu ni mmoja tu wapo wengi sana kwakweli hawa jamaa hakuna namna unaweza kusema wanajua kingereza.
To make story short hawa jamaa hawajui kuongea kingereza at all.
 
We communicate using drawings and math!!!
 
Pengine BUSARA itumike wabunge Wetu wa ccm wa mwambie mwenyekiti WA chadema wanamtaka nani na nani wawe wabunge wa bunge la Africa mashariki nadhani itakuwa simple uchaguzi kama mbowe kaleta watu wake sisi hatuwataki tumpe muongozo mlete fulani na fulani simple
 
Lugha rasmi ya Bunge la EAC ni English ingawa nasikia tutaanza kutumia na lugha ya kiswahili. Ukiangalia hiyo video unapata mawazo mengi na kujiuliza kama huko CCM kuna wabunge wanao ipenda Tanzania. Na swali jingine unajiuliza kama wana akili sawa ktk vichwa vyao.

..waTz hatuelezani ukweli kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiingereza.

..tunadanganya wananchi eti Kiswahili kimeruhusiwa OAU/AU. Sasa ukiangalia matangazo ya ajira AU wanaeleza kuwa lugha rasmi ni English, French, and Portuguese.

..Kiswahili kinasikika AU siku Raisi wa Tz akihutubia( most likely mara 1 kwa mwaka) na baada ya hapo hakuna mtu ana habari na Kiswahili huko AU.

..Hata SADC na EAC hawatumii Kiswahili ktk shughuli za kiofisi.

..Tunaweza kulazimisha wabunge (SADC & EAC)wetu wazungumze Kiswahili, lakini idadi yao haizidi 20.

..kuna mamia ya nafasi za kazi ktk SECRETARIAT za SADC na EAC ambazo kujua KIINGEREZA ni moja ya requirements. Vijana wetu hawataajiriwa huko kama Kiingereza chao ni kama kile tulichokishuhudia bungeni.
 
Ndo mshindwe kutaja neno "I will not let you down" au "Front page?"
Be serious
Hiyo sentensi imemsumbua mheshimiwa hadi nimemuonea huruma. Pale mwanzo alianza vizuri sasa sjui alikariri vikatoka
 
Back
Top Bottom