Video: Huyu dada ambaye ni mlinzi binafsi wa Tundu Lissu nimetokea kumfikiria sana. Hapa ni Chato anataka kumkunja askari wa FFU

Awali nilitangaza kumchagua Magufuli kwa hoja hizi:-
1. SGR
2. Nyerere dam
3. Barabara za mikoa iliyotengwa kama kigoma kwetu ambapo bado km 180 hivi kuunganishwa na lami
4. Kuhamia dodoma

Miradi yote hii mikubwa naamini ni Magufuli pekee ameianzisha na naamini ndiye ataikamilisha kwa ufanisi.

Hata hivyo, kwa kuwa Magufuri ni muumini wa siasa za fujo ama kwa kujua au kutokujua na kupelekea yafuatayo:-

1. Misafara ya Lissu kukosa coverage kama Magufuli
2. Misafara ya Lissu kunyimwa fursa sawa na Magufuli. Magufuli anasimama popote, bila kujali ratiba, Lisu kajaribu kafungiwa
3. Misafara ya Lissu kupigwa mawe, wagombea ubunge kupigwa mawe na wengine kuumizwa, mara nyingi vurugu hizi huratibiwa na ma DC
4. Na manyanyaso yote wanayofanyiwa wasio wa CCM.

Nimeghairi sasa ntawachagua hawa watu. Lengo ni:-
1. Tuone sera zao kwa miaka mitano
2. Katiba mpya
3. CCM na wao wawe chama cha upinzani waone taabu za kuwa wapinzani. Najua chadema wametangaza kutolipiza kisasi.
5. Serikali kamili za majimbo, zinazopatikana kwa ridhaa ya wanachi na siyo maamuzi ya mtu mmoja

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Huyu dada nimekuwa namfuatilia kila alipo Tundu Lissu kwenye hii mikutano ya kampeni inayoendelea.

1. Anaonekana ni mtu jasiri sana kila anakopita.
2. Anaonekana ni mtu mwenye mafunzo hodari ya ukakamavu.
3. Anaonekana kuwa very loyal. Yeye ndiye anakaa upande wa kushoto wa Tundu Lissu pamoja na yule kijana anayekaa upande wa kulia.
4. Hataki na hapendi mzaha.

Kwenye video hapa anataka kumkunja askari wa FFU huko Chato jana kabla hajatulizwa na mwanamama wa BAWACHA.

Kweli nyakati zimebadilika
View attachment 1599502
Alichofanya huyu dada ni kazi nzuri sana. KEEP IT UP LADY!
 
Mbona mnashabikia upumbavu sana.

Hivi kuzuia jeshi la polisi na kutaka kumpiga askali nowdays imekuwa sifa.

Sema serikali ya Tanzania inahuruma sana,Ingekuwa sehemu nyingine huyu bibie angepatikana na shtaka la kujibu mahakamani.

Acheni kushabikia ujinga buana.

Mpumbavu utakuwa ni wewe Mkuu ,Askari yeyote hatakiwi kuvunja Sheria anapokuwa ana tekeleza wajibu wake kinyume na hapo ni vurugu.

Kwenye Red unatakiwa kuwa na Ushahidi wa kutosha kuthibitisha Mahakamani ,Askari ni Raia kama sisi kila mmoja ana wajibu wa kumshughulikia yeyote anae vunja Sheria.Usiwatetee sana na wao huwa wana kosea sana sana mno.
 
Mbona mnashabikia upumbavu sana.

Hivi kuzuia jeshi la polisi na kutaka kumpiga askali nowdays imekuwa sifa.

Sema serikali ya Tanzania inahuruma sana,Ingekuwa sehemu nyingine huyu bibie angepatikana na shtaka la kujibu mahakamani.

Acheni kushabikia ujinga buana.

Lakini kwako ni sifa kwa Askari kuvunja amani? Kuonyesha upendeleo kwako hio ndo sifa eti😁
 
Hizo mbwembwe tu angejaribu kumkunja huyo askari halafu ungeona show yake hapo mbona huyo dada angesarenda na kuolewa kabisa na huyo police
 
Huyo mwanamke Ana power au kelele?

Huyo FFU angeamua kufanya kweli angeyaweza? Real power iko kwa huyo askari

Usicho kijua kama huyo Askari ange mshambulia unafikiri Raia wange muangalia tu ,hata kama ni mimi ninge mfanya kitu mbaya sana huyo Poti.
 
Lakini kwako ni sifa kwa Askari kuvunja amani? Kuonyesha upendeleo kwako hio ndo sifa eti😁
Popote linapotokea public interest(Manufaa kwa umma). Police atalazimika kuhakikisha jambo lolote linakwenda sawa kwa ajili ya umma kwa ujumla lakini sio kikundi kidogo cha watu.

Mmoja afe, ili watu mia waishi salama.(Hii kauli usiichukulie juu juu tu,tafakari then reply).
 
Askari Polisi asipo fuata misingi ya kazi yake na kushirikiana na wahalifu tayari sifa za kuwa askari zinaishia hapo hapo zinabaki nguo tuu alizovaa ndio za polisi.
Umeona Nigeria nin kimetokea kwa SARS?

Mkuu tatizo hapa Tanzania Watawala (wana Siasa) huwa wana wapa ulinzi wa kisheria Askari wetu ,nna kumbuka kipindi flani Mkuu wa Nchi nae aliagiza Askari kuua Majambazi.Yani kwa namna Askari wanavyo bebwa ni rahisi kufanya jambo baya na waka pongezwa.Ya Akwilina (R.I.P.) yame tufunza mengi sana.
 
Hapana anatoka mwenyewe baada yakuona hawezi bishana na mwanamke! Huyo ndiyo mwanaume halisi unaanzaje kubishana na mwanamke? Ndiyo wanaume wa Kanda ya Ziwa walivyo hawabishani na wanawake ila akileta cha kuleta anapata kibano cha kiume full stop.
We matope, nani kakwambia kuwa huyo ni "mwanume wa kanda ya ziwa'? Ulivyo chenga, unafikiri hayo ni mabishano baina ya mwanaume na mwanamke?-hayo ni mabishano ya kikazi..
 
Huyo mayala ana mazoezi gani?? labda ya kukung'utwa tu

Una weza kusema chochote ,nikwambie tu nime kutana na hawa Viumbe kwenye mafunzo makali na huonyesha weledi wa hali ya juu.Yani hizi dharau zako hizi ndio zitakufanya uumizwe au uuliwe na hawa viumbe ..

Nna kumbuka kuna Jamaa mmoja mwenye mdomo mdomo kama wewe aliwahi mchomokea Msichana flani hivi Jamaa akiwa la Lori la Mchanga,Msichana alie chomekewa alijitahidi kulihimili Gari lake lakini aling'oa baadhi ya mabambari.Jamaa walipofika Site kumwaga Mchanga wakashangaa kuona Gari imepaki nyuma yao akashuka huyo Binti na kuwa uliza kistaarabu ,wakamjibu vibaya na Matusi kibao.

Hakuna alie amini Dereva alipigwa kama Mtoto mdogo Sehemu za Kichwa tu mpaka Jamaa akadondoka.Ni kitendo cha haraka yule Binti akaondoka zake na hakuna alie kumbuka hata ku'notice namba za Gari la yule binti.Jamaa wa Lori mpaka leo Akili hazipo sawa Ndugu wame tumia Pesa nyingi kumtibu Muhimbili bila ya mafanikio ,Mke kamkimbia na Watoto pia sababu ya shida ya Ubongo aliyo ipata..

Hichi ni kisa cha kweli ,hivyo nna kuomba Ndugu yangu usimdharau Mtu yeyote na ukamchulia poa tu jifunze sana namna ya kuishi na Binadamu wengine hapa Duniani.
 
Polisi wa Tanzania unaweza fananisha na kikundi cha SARS.

Hivi unajua kweli kipi kilikuwa kinafanywa na SARS pale Nigeria??

Huu ni Mfano Mfu kabisa katika muktadha huu.

Kwani hao SARS majukumu yao yalikuwa ni yapi Mkuu kama sio kupambana na Wahalifu !?..

Yaliyo tokea kwenye Msafara wa Lissu ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine ,au ulitamani mpaka afe Mtu ndio utaona huo kweli ulikuwa ni uhalifu ?
 
Popote linapotokea public interest(Manufaa kwa umma). Police atalazimika kuhakikisha jambo lolote linakwenda sawa kwa ajili ya umma kwa ujumla lakini sio kikundi kidogo cha watu.

Mmoja afe, ili watu mia waishi salama.(Hii kauli usiichukulie juu juu tu,tafakari then reply).

Sio mbaya Police kufanya Ghasia ili kuleta Amani , si ndivyo Mkuu ?
 
Back
Top Bottom