Video: Hotuba ya Rais Magufuli uwekaji wa jiwe la msingi Kinyerezi II

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
Hotuba inayogusa mtazamo na mpango wa serikali katika Sera ya Nishati.

Hotuba anayogusia Sheria ya Umeme ya mwaka 2008 na pia mpango wa Mabadiliko ya Sekta ya Nishati (Electricity Sector Industry Reform) ya mwaka 2014.

Hotuba inayogusa matarajio ya serikali katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na Nishati.

Ni hotuba inayogusia hatima ya IPTL na wawekezaji wengine kwenye sekta ya Nishati.

Hotuba inayogusa sababu ya Rais Magufuli kumteua Prof. Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Hotuba inayogusa sababu ya kumteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

MITSUBISHI HITACHI H-25 Combined-cycle Power Plant
..Gas turbine/Steam Turbine..
h25_tab03_02.jpg

si mchezo..
Construction begins on Tanzania’s first natural gas-fired combined cycle power plant| Sumitomo Corporation

http://www.power-eng.com/articles/2...-for-tanzania-s-1st-combined-cycle-plant.html
 
Kama Rais yupo serious juu ya kumaliza tatizo la umeme, serikali iweke nguvu kule Stigler's Gorge. Kule kunaweza kuzalishwa Megawatts 2,000 zaidi ya mahitaji ya nchi kwa sasa. Baada ya hapo, apeleke nguvu kwenye wind turbines na solar power plants kanda ya kati. Kwa hii miradi mitatu, Tanzania itakuwa na umeme hadi wa kuuza nje kwa miaka michache ijayo, mpaka pale ujenzi wa viwanda utakapohitaji umeme zaidi. Hapo ndipo vyanzo vingine kama nuclear power plants vinaweza kutumika.
 
..mimi kanishangaza kuhusu vigezo anavyodai ametumia kuwateua Muhongo na Makonda.

..yaani ni as if lengo la Raisi kuwateua lilikuwa ni kuwakomoa wale wanaokosoa utendaji na mwenendo wa hao wawili.

..mimi nadhani Raisi yuko TOO CONFRONTATIONAL when dealing with wapinzani kitu ambacho siyo kizuri kwa demokrasia ya nchi yetu.
 
Uwekaji saini makubaliano ya awali ya ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania
 
..mimi kanishangaza kuhusu vigezo anavyodai ametumia kuwateua Muhongo na Makonda.

..yaani ni as if lengo la Raisi kuwateua lilikuwa ni kuwakomoa wale wanaokosoa utendaji na mwenendo wa hao wawili.

..mimi nadhani Raisi yuko TOO CONFRONTATIONAL when dealing with wapinzani kitu ambacho siyo kizuri kwa demokrasia ya nchi yetu.
Yes, Rais Magufuli is too emotional and impassioned. Vile vile ana soft touch.
 
Kama Rais yupo serious juu ya kumaliza tatizo la umeme, serikali iweke nguvu kule Stigler's Gorge. Kule kunaweza kuzalishwa Megawatts 2,000 zaidi ya mahitaji ya nchi kwa sasa. Baada ya hapo, apeleke nguvu kwenye wind turbines na solar power plants kanda ya kati. Kwa hii miradi mitatu, Tanzania itakuwa na umeme hadi wa kuuza nje kwa miaka michache ijayo, mpaka pale ujenzi wa viwanda utakapohitaji umeme zaidi. Hapo ndipo vyanzo vingine kama nuclear power plants vinaweza kutumika.
Yes, ushauri wako ni mzuri.

Sekta ya Nishati imechezewa sana nchini.

Nidhani baada ya uvumbuzi wa gas, huu mradi ulisahaulika au uliwekwa kando pamoja na kupata clearance zote za go ahead.
 
..mimi kanishangaza kuhusu vigezo anavyodai ametumia kuwateua Muhongo na Makonda.

..yaani ni as if lengo la Raisi kuwateua lilikuwa ni kuwakomoa wale wanaokosoa utendaji na mwenendo wa hao wawili.

..mimi nadhani Raisi yuko TOO CONFRONTATIONAL when dealing with wapinzani kitu ambacho siyo kizuri kwa demokrasia ya nchi yetu.
Is the opposition not too confrontational when dealing with the Government...!??
 
..mimi kanishangaza kuhusu vigezo anavyodai ametumia kuwateua Muhongo na Makonda.

..yaani ni as if lengo la Raisi kuwateua lilikuwa ni kuwakomoa wale wanaokosoa utendaji na mwenendo wa hao wawili.

..mimi nadhani Raisi yuko TOO CONFRONTATIONAL when dealing with wapinzani kitu ambacho siyo kizuri kwa demokrasia ya nchi yetu.
Ume overunderstand rafiki. Alitaja kabisa (waweza rejea tazama tena) kwamba yeye alikuwa haangalii maneno BALI utendaji KAZI tu. Kwani hatuwateua kufanya siasa ila kuleta maendeleo.
 
Ngoja tumpe Shule huyu mwenzetu anaetaka kuturudisha nyuma na Miradi hewa ya World Bank ya Stigler's Gorge,
Licha ya Mradi huo Kuwa na MW 2000. Muhongo alituma Elimu hii' tuna mabwawa 5 ya kuzalisha umeme Tanzania, ambayo yote yanategemea Mvua ili yajae na kuzalisha umeme. Licha ya Kuwa na mabwawa Haya matano, yote tatizo kubwa maji hayatoshi Kwa Kuwa Watanzania wengine wanayatumia kwa ajili ya kilimo. Kwa akili ya kuzaliwa tungetegemea mtushauri kutafuta Miradi mingine ya ambayo itatuletea maendelea, tusifanywe kichwa Cha wendawazimu Kwa kutuletea miradi mibovu
 
..hivi unaamini kwamba hakuna siasa?

..mahali ambapo viongozi wana mahusiano mabaya, na hawashirikiani, kazi za kuleta maendeleo inakuwa ngumu.

..sasa ukimsiliza Raisi wetu utaona kwamba yeye haamini ktk dhana ya viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa kusikilizana na kushirikiana.

..Makonda anaweza kuwa ni mchapa kazi mzuri, lakini kama hana mahusiano mazuri na wabunge na madiwani ktk mkoa wa Dsm, then sidhani kama ana fit kuwa mkuu wa mkoa huu. Ningemuelewa Raisi kama angemteua kuwa mkuu wa mkoa sehemu nyingine lakini siyo Dsm.

..Mimi nilitegemea Raisi angezungumza lugha ya kuwaunganisha wabunge, madiwani, na mkuu wa mkoa. Badala yake anazungumza lugha ya KIBURI na kutokujali.
 
Kaka, you are too lightweight to engage with...unafikiri na kusema simplistically...na kama hiyo ni quote ya Muhongo, basi tuna kazi sana. Wakati mimi nawaza maji katika upana wake (hydrological cycle), wewe (au Muhongo kama umem-quote) unawaza/anawaza maji ya mvua! Besides, EIA ya Stigler's Gorge ilifanyika miaka ya 1980 na ikaona mradi ni feasible. Sasa wewe unasema tu kwa wepesi na mzaha mzaha. Kuhusu maji ya kilimo, mimi nimeshaondoka na dunia ya kuwaza kilimo cha kutegemea mvua. Ndiyo maana nimesema awali kwamba wewe ni lightweight katika huu mjadala.
 
Magufuli kapoteza fursa nzuri ya kuwaunganisha Watanzania wawe wamoja, walompa kura na walomnyima kura. Ni wazi Dar es Salaam waliikataa CCM na mgombea wake na hii ilikuwa nafasi nzuri kwa Rais kuonesha yeye ni kongozi mkuu wa Watanzania wote bila kujali itikadi. Yeye kakamata makali, vyombo vyote vya dola viko chini yake na kauli yake kulingana na katiba ya sasa ni agizo kwa watendaji wa serikali bila kujali sheria inasemaje.

Hapo palikuwepo na pande mbili, wawakilishi wa wananchi na wawakilishi wa serikali na ilikuwa ni nafasi nzuri ya kuwaleta pamojaa kwa lugha ya upatanishi, lugha ya kiungwana. Badala yake kaamua kuwa confrontational huku akijua wapinzani hata kama hawaafiki hawana uwezo wa kushindana naye. Kwa wastaarabu wanaoheshimu utawala wa sheria na kidemokrasia, wawakilishi wa wananchi ndio huwawajibisha wawakilishi wa serikali na si vinginevyo.

Magufuli ana mengi ya kujifunza na tuombe Mungu amfunulie mbinu ya uongozi uliojaaa hekima unaoendana na nafasi yake katika jamii. Nina hakika akiwa kiongozi mpatanishi, hata walio na mashaka naye kama mimi nitamwangalia katika jicho tofauti na mwanga mpya. Kulikuwa na taabu gani hao kuwatambulisha wawakilishi wa wananchi kama Meya? Kulikuwa na haja gani kuongea kwa lugha ya maudhi kama ya mitaani iliyojaa vijembe kwao? Really?
 
..hivi unaamini kwamba hakuna siasa?

..mahali ambapo viongozi wana mahusiano mabaya, na hawashirikiani, kazi za kuleta maendeleo inakuwa ngumu.

..sasa ukimsiliza Raisi wetu utaona kwamba yeye haamini ktk dhana ya viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa kusikilizana na kushirikiana.

..Makonda anaweza kuwa ni mchapa kazi mzuri, lakini kama hana mahusiano mazuri na wabunge na madiwani ktk mkoa wa Dsm, then sidhani kama ana fit kuwa mkuu wa mkoa huu. Ningemuelewa Raisi kama angemteua kuwa mkuu wa mkoa sehemu nyingine lakini siyo Dsm.

..Mimi nilitegemea Raisi angezungumza lugha ya kuwaunganisha wabunge, madiwani, na mkuu wa mkoa. Badala yake anazungumza lugha ya KIBURI na kutokujali.
Ni mbunge gani hana uhusiano naye mzuri, Kubenea? Hao ni wanasiasa don't take them too serious man. Wataelewana tu katika ujenzi wa taifa na cha msingi hapa watuletee maendeleo na si kuweka vyama mbele.
 
Kaka, you are too lightweight to engage with...unafikiri na kusema simplistically...na kama hiyo ni quote ya Muhongo, basi tuna kazi sana. Wakati mimi nawaza maji katika upana wake (hydrological cycle), wewe (au Muhongo kama umem-quote) unawaza/anawaza maji ya mvua! Besides, EIA ya Stigler's Gorge ilifanyika miaka ya 1980 na ikaona mradi ni feasible. Sasa wewe unasema tu kwa wepesi na mzaha mzaha. Kuhusu maji ya kilimo, mimi nimeshaondoka na dunia ya kuwaza kilimo cha kutegemea mvua. Ndiyo maana nimesema awali kwamba wewe ni lightweight katika huu mjadala.
Bahati mbaya wewe ndie usiyejua. Mradi unaoupigia debe ulikuwa ufadhiliwe na Norwegians lakini baada ya kutambua athari yake down river wakautema. Miradi kama hii ni antiquated, msitake kuturudisha nyuma.

Amandla........
 
Tatizo la Stiegler's Gorge siyo athari kwenye mazingira brah! EIA na SEA zilifanyika na mwishowe UNESCO na World Heritage Centre wakatoa 'kibali'. Jambo moja ambalo limekuwa likileta mvutano ni siasa za RUBADA na TANESCO. RUBADA anataka umiliki kwa kuwa gorge ipo kwenye eneo lililo chini ya RUBADA. TANESCO hawataki hilo kwani wanasema wao ndiyo wenye mamlaka ya kuzalisha na kusambaza umeme. Miaka kama mitano (kama nakumbuka vizuri) iliyopita wabrazil na wachina walikuja na kutaka kuendeleza mradi, lakini siasa zimekwamisha. Hadi MoU ilisainiwa; lakini siasa inakwamisha, na ilisemwa mwaka 2015 mradi ungekuwa umekamilika, lakini bila bila. Ndiyo maana katika post yangu ya kwanza, nilisema kama Rais ana nia ya kweli kumaliza tatizo la umeme, huo mradi upewe msukumo mzito. Kama mradi ulipata clearance na MoU ilisainiwa, Rais aweke msukumo sasa, ili tuzalishe umeme hadi wa kuuza.

Angalia hapa habari za hivi karibuni kwa mradi unaouita 'antiquated':

http://allafrica.com/stories/201207060460.html

STIEGLER'S GORGE ENERGY PROJECT SECURES INTERNATIONAL CLEARANCE

Stiegler’s Gorge hydroelectric project would have regional advantage

Home

Home

Tanzania plans $2 bln hydro plant with Brazil | Reuters

Na hapa ni mjadala JF: Stiegler's gorge hydropower project

Brah, kuhusu huo mradi bado una taarifa za miaka ya 1980. Ebu jaribu kuwa up-to-date kidogo. Yaani bado unaongelea habari za miaka ya 1980 kwa jambo ambalo hata Kikwete alikuwa akilipigia chapuo kwenye safari zake za kitalii?!?
 
Back
Top Bottom