Mkuu Research ni muhimu sana kabla ya kuanza biashara yoyote:-Je ni watu gani watanunua hizo games na kwa bei gani na ni wangapi wenye games?Je hao watu wenye Games Console huwa games zao wanazipata wapi na je unaweza ukacompete nao bei?Hizo Games utazipata wapi na kwa bei gani, na Je unaweza kuuza kwa faidi baada ya kuziingiza nchini na Je price haitakuwa kubwa sana?Baada ya kujibu hayo maswali hapo juu naona utapata jibu kuwa market sio kubwa sana kwa kuuza labda ufanye Games Library ambapo watu wanaazima games, cause itakuwa cheaper au uanzishe games cafe, ambapo unaweza consoles zako za kutosha na unacharge watu per hour kwa kucheza games, ukifanya cafe ikawa nzuri na ukaweka na viburudisha (drinks etc) nadhani faida itakuwa nzuri na utapata watu zaidi ya kuuza games peke yake