Kwa Nchi kama Pakistan,IRAN ana Somalia Hukumu hiyo ni halali kutopkana na sheria zao walivyopanga. Kwa Nchi kama ya kwetu hakuna sheria hiyo.Hukumu ya hii ni halali? Nilishindwa kuangalia video yote.
Watch "18+ Stoning To Death Of Muslim Man Pakistan."
Najua Irani kuna mama mmoja anayetegema kupigwa mawe naye namna hii hadi afe. Je ni kweli kuwa tuwe tunahukumiana kinyama namna hii?
Kwa Nchi kama Pakistan,IRAN ana Somalia Hukumu hiyo ni halali kutopkana na sheria zao walivyopanga. Kwa Nchi kama ya kwetu hakuna sheria hiyo.
Kumbukumbu la Torati/ Chapter 22 22. Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli.
23. Pakiwa na kijana aliye mwanamwali ameposwa na mume, na mwanamume akimkuta mjini, akalala naye;
24. watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
...wokovu ukaletwa na Yesu Kristo, maandiko katika Agano Jipya yanaonyesha mabadiliko baada y akuja Yesu Kristo. Kundi lingine lilipotaka kumpiga mtu mawe Bwana akawaambia kati yenu asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe, hakubaki mtu!
Bwana Yesu Anasema tena soma hapa> / Mathayo/ Chapter 5-27. Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28. lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum
/ Mathayo/ Chapter 5 - 17. Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
Mkuu MNDEE Unamsikia BWANA YESU Anavyosema hapo juu? hakuja kuibadilisha TORATI Ya Manabii bali Kuitimiliza. Sasa Wewe unaifuata TORATI Ya Manabii? Au Unamfuata Mtume Paulo Asiyefuata TORATI YA Manabii?.....QUOTE]
Tatizo la kusoma Biblia bila kupitia mafundisho ndio hili, unakamata kimstari kimoja unakimbizana nacho, kesho utakamata tambiko la wanyama na kulibebea bango. Mkuu si wezi bishana na mtu anayesoma Biblia kama gazeti.