Wakuu tayari video clips kwa ajili yakuonesha namana mbalimbali za kuweka picha hapa JF zimekamilika. Ziko tatu
Ya kwanza inaonesha jinsi ya kuweka picha kama attachment. Hii ndo imekua ikitumiwa na watu wengi lkn sio nzuri hasa ukizingatia kiwango cha JF kutokana na kwamba picha zake zinakua ni ndogo.
Clip ya pili inaonesha jinsi ya kuweka picha pasipo kutumia njia ya attachment. Pia hii imekuwa ikitumiwa na wengi ingawaje picha bado zinabakia ndogo ingawaje kunakuwa na kaunafuu tofauti na mfumo wa kwanza wa attachment.
Clip ya tatu inaonesha jinsi ya kuweka picha ikawa kubwa. Hii ndo inayotakiwa/pendekezwa (most recommended).
Hi Jing ni software kwaajili ya kutengenezea video na pia unapo upload video huhifadhiwa kwenye sever ya Jing. Jing haihusiani na kuweka ama kukuza picha.
Sasa? Kwanini kusiwe na namna moja tu ya kuweka picha, yaani hiyo ambayo picha itakuwa kubwa kwa vile kila mtu anapenda picha kubwa.
Iwe kama facebook vile...