Elections 2010 Video: Alichosema Marando Jangwani

Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
124

Naona mpaka Judge Mkuu kaingia mkenge akizani video wanayo TBC peke yake. Sasa kwenye hii vieo kuna matusi gani jamani Wewe Tido Mhando ebu angalia? Makamba tuambie ni kipande ipi hapo ni matusi?
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Shalom kwa kiunganishi hicho!

Hakika watawala wetu walijisahau sana... Wengi wao wamesahau hata ule usemi kwamba, kila jambo lina mwisho. Wengi wao wamejisahau kuwa ulimwengu unabadilika na uwazi kuongezeka. Pamoja na teknolojia zote zilizopo za mawasiliano naona bado walidhania kuwa kuna maovu wanaweza kufanya na Watanzania kamwe wasiyajue.

Wengi wa viongozi wetu hawajasoma alama za nyakati. Wengi wanaaibika kwa kuenguliwa kwenye chaguzi na maovu yao kufichuka moja baada ya jingine. Na kwa Chama cha mapinduzi ni aibu kuona kwamba karibia viongozi wake wote wa ngazi za juu wameishia kuwa waropokaji au wasahaulifu, au wamehusika katika kashfa kubwa katika Taifa letu. Bila shaka kwa yale yaliyojiri kwenye uchaguzi huu mpaka hivi sasa na hata hapo 31 Oktoba yatawafanya viongozi wengi walio madarakani hivi sasa kuachia ngazi wao wenyewe kwa kuhofia yatakayowakumba mbeleni, haswa 2015.
 
Shalom,

asante sana, unaweza kuendeleza hii hotuba? maana mpaka hapo tuliona walio wengi ila complete speech ingekuwa bora. Asante sana
 
Bora hata ya Jaji mkuu kuliko Mwanasheria mkuu wa serikali. Maana ukisikia kuna viraka vimewekwa madarakani basi ni pamoja na yule jamaa. Sijui inakuwaje mtu mpayukaji kama yule kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Nimeipenda sana hotuba ya Marando. Lakini watanzania ni vichwa ngumu. Pamoja na kujua haya yote bado utawaona wakiendelea kuibeba CCM.
 
Bado sijasikia tusi hata moja labda jamaa wanatumia filters tofauti...:becky:
 
Shalom,

Asante sana. Iko so clear, Studio Quality.

Una sehemu iliyoendelea mara baada ya TBC kukata matangazo au shughuli zilisimama?

Je, ile ya Shibuda aliyoongelea Kumtoa Mwali Ikulu unayo?

Thanks in advance.
 
Bora hata ya Jaji mkuu kuliko Mwanasheria mkuu wa serikali. Maana ukisikia kuna viraka vimewekwa madarakani basi ni pamoja na yule jamaa. Sijui inakuwaje mtu mpayukaji kama yule kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
Nimeipenda sana hotuba ya Marando. Lakini watanzania ni vichwa ngumu. Pamoja na kujua haya yote bado utawaona wakiendelea kuibeba CCM.

Nimepapenda
 
Jaji mkuu si mteule wa rais?? HAYUKO HURU!!! Naichukia sana katiba ya Mwaka 1977 (na viraka vyote vilivyowekwa baadaye). Mfumo wote hauko huru, ni CCM wote. Wasaka tonge. Akili weka pembeni.
 
Siasa za kudanganyana zinafika ukingoni. Sasa matusi hapa yako wapi? Au kuna jina likitajwa na Marando linageuka tusi?
 
Nilidhani huyu Mura alitukana kumbe hata tusi mmoja hakuna! Sana sana ametoa tuhuma, kwa nini TBC waslivyanya alichofanya? Na kama Kikwete na Mkapa hawakuiba, basi wamburuze Marando kortini.....hivi bado kuna watu wanaona kuna serikali hapa! Kwa nini uwatese wengine kwa sababu ya wizi wako, ewe Mkwere?????????
 
Wakuu ninayo nyingine ni kali sana ila ni kubwa sasa nashindwa kui upload kwa sababu ya hii mitambo yetu. Hii ni kiboko kwani inatoa ufafanuzi wa mambo mengi tu
 
Back
Top Bottom