VIDEO - Ajaribu Kuliiba Kombe la Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Ajaribu Kuliiba Kombe la Dunia

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Jul 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">VIDEO - Ajaribu Kuliiba Kombe la Dunia</td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Jimmy Jump akipewa konde lililomwangusha chini</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Monday, July 12, 2010 9:36 PM
  Mwanaume ambaye aliingia uwanjani na kujaribu kulivalisha kofia kombe la dunia kabla ya mechi ya fainali kati ya Uholanzi na Hispania atafikishwa mahakamani jumatatu kwa kosa la kujaribu kuliiba kombe la dunia.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Mwanaume huyo ambaye ni raia wa Hispania anashtakiwa kwa makosa ya kuviruka vizuizi vya ulinzi na kujaribu kuliiba kombe la dunia.

  Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 34 anayeitwa Jaume Marquet i Cot ambaye ni maarufu kwa jina la "Jimmy Jump" ni maarufu kwa kuzamia kwenye viwanja na majukwaa kwenye matukio mbalimbali makubwa duniani.

  Miongoni mwa matukio ambayo Jimmy Jump alizamia ni mechi ya fainali ya Euro 2004 kati ya Ugiriki na Ureno, mechi ya nusu fainali ya klabu bingwa ulaya mwaka 2005 kati ya Liverpool na Chelsea, mechi ya nusu fainali ya Euro 2008 kati ya Ujerumani na Uturuki na mechi zingine kadhaa kubwa duniani.

  Jimmy Jump pia ametia maguu maguu yake kwenye mechi kubwa za basketball, rugby na hata kwenye mashindano ya muziki ya Eurovision mwaka huu.

  Katika tukio la nchini Afrika Kusini, Jimmy alikimbia kuingia uwanjani akitaka kulivalisha kombe la dunia kofia yake nyekundu lakini kabla ya kutimiza azma yake alipigwa ngumi na mlinzi na kuanguka chari kabla ya kubebwa msobe msobe na kupelekwa mahabusu.

  Chini ni VIDEO ya tukio hilo lililotokea kabla ya kuanza kwa mechi ya fainali ambapo Hispania ilishinda 1-0 na kutawazwa mabingwa wa dunia.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;">

  VIDEO - Ajaribu Kuliiba Kombe la Dunia
  <object height="385" width="640">


  <embed src="http://www.youtube.com/v/2BjJTYldyGQ&hl=en_GB&fs=1?rel=0" type="application/x-shockwave-flash" allowscriptaccess="always" allowfullscreen="true" height="385" width="640"></object>


  Chanzo NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.


  </td> </tr> </tbody></table> <table style="width: 488px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td style="width: 429px;">
  </td> <td style="width: 249px;"> Mwizi huyo waKombe la dunia ama kweli Miafrika Bwana Ndivyo ilivyo
  </td></tr></tbody></table>
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Duniani kuna Vituko vya kila aina na watu aina na tabia mbalimbali
   
 3. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Duh! Hii njemba bwana. Hata hofu hamna?
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 394
  Trophy Points: 180
  Ingekuwa Bongo hilo lilikuwa limekwenda ati
   
Loading...