VIDEO - 17 Wafariki Papo hapo, 78 Wajeruhiwa Kwenye Ajali Tabora

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
6563878.jpg

Basi la Sebena lililopinduka na kuua jumla ya watu 17
Thursday, August 09, 2012 10:09 AM
WATU 17 wamefariki dunia na wengine 78 kujeruhiwa baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kupinduka eneo la Kitunda Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Basi hilo la Sabena aina ya Scania yenye namba za usajili T 570 AAM ndilo lililosababisha vifo hivyo majra ya jana mchana.

Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Tabora kuelekea mkoani Mbeya

Miongoni wa watu waliokufa walikuwemo watoto watano, wanawake sita na wanaume sita ambao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Kitete kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu na jamaa zao.

Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kugoma kwa usukani wakati dereva alipokuwa akijaribu kulikwepa Fuso lililokuwa limeegeshwa katika kona eneo hilo, hivyo basi hilo likaacha njia na kupinduka

<tbody>
</tbody>




VIDEO - 17 Wafariki Papo hapo, 78 Wajeruhiwa Kwenye Ajali Tabora
 
Last edited by a moderator:
Huyu mtangazaji mbona hata kiswahili chenyewe hajui. Ina maana bado Tanzania hakuna watu waliosomea utangazaji wanaojua kiswahili?
 
Back
Top Bottom