Victor Ambrose ndie aliyerusha bomu kanisani !

Victor Ambrose ndie aliyerusha bomu kanisani !

Huenda waarabu wawatu wamekamatwa kwa sababu ni waarabu tu basin a si sababu nyingine. Jeshi letu la polisi lina matatizo mengi makubwa kwa sababu walioenda kule ni wale waliokuwa na uwezo mdogo kichwani na ndio mana wanatumiwa kisiasa bila kuonyesha resistance yoyote. Lakini bado ukweli unabaki, kushughulika na ugaidi ni jambo gumu sana. marekani yenyewe inapata shida sana kushughulika na tatizo la ugaidi nchini kwao. Leo hii naona kuna wasichana walikuwa wametekwa miaka karibia kumi wamefichwa tu kwenye nyumba huko marekani, lakini jeshi lao lilishindwa kutambua mpaka leo ndio wanaokolewa.
Suala la Ulimboka, ni tofauti sana. lile lilikuwa suala lingine kabisa na inaelekea serekali inahusika moja kwa moja.
 
Halafu mtu ananishawishi nijivunie utanzania na kua mzalendo,serukamba hii serikali
 
Baada ya Mkenya kuhusishwa na tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dr.Ulimboka katika mazingira ya utatanishi, sasa jeshi la polisi linawashikilia raia wa Saudi Arabia likiwatuhumu kuhusika na mlipuko wa bomu katika kanisa moja mjini Arusha.

Kwa mujibu wa maelezo ya waziri mkuu leo bungeni, raia hao walikamatwa walipokuwa wakitaka kuvuka mpaka wa Tanzania na kenya mpaka ambao ulifungwa kufuatia tukio hilo. Katika maelezo yake,Waziri Mkuu Pinda alisema polisi waliwashuku raia hao waliokuwa wakitaka kuvuka.

Kwa mazingara haya,ni wazi huenda raia hao wameshukiwa kama alivyoshukiwa yule Mkenya. Sitashangaa na wala haitakuwa ajabu kesho tukiambiwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuwahusisha raia hao na tukio hilo na hivyo polisi kulazimika kuwaachia huru.

Intelijensia ya polisi wetu iko chini sana na inaonekana kitengo husika hakina competent people!

Tusubiri tuone movie nyingine inayokuja.

kama hawa watu wa saudia hutaki kuamini kwamba wamehusika pamoja na hao watanzania wengine basi wewe na familia yako umehusika,huoni hata haya.
 
Hata mimi matusi nayajua ili sioni busara yeyote kukutukana.Tukirudu kwenye hoja mimi nasema "time will tell"

tangu lini umeanza kuw na busara muovu mkubwa unajenga hoja ya ajabu hivyo halafu unataka watu wakuchekee,akulehemu ee mungu kwa kuwa umetenda zambi
 
Tukio la ugaidi ni ugaidi, liwe limefanywa na mwarabu, mkristu, muislamu, Raisi, Waziri, mbunge ama raia yeyote yule. Leo Serikali ya chama cha mapinduzi chini ya waziri wa mambo ya ndani imeutangazia umma imekamata watu sita ambao wanashukiwa kujihusisha na tendo la kujipatia bomu, kulisafirisha na kulitupa katikati ya waumini wa kikakoliki kuuwa na kujeruhi watu vibaya.

Lengo lilikuwa ni kuuwa waumini, kuuwa Mwakilishi wa Papa Tanzania Askofu Padilla na Askofu mkuu wa kanisa katoliki Jimbo la Arusha.

Kinachoshangaza hata kilichoshangaza kanisa pamoja ni usiri wa watuhumiwa hawa wengine huku serikali ikiamua kutangaza jina moja na kuficha majina mengine. Kanisa wao wanadai swala la ugaidi ni ugaidi, Papa alipigwa risasi kanisani, kanisa limeshudia kuteswa na kuuwawa kwa waumini wake kuchomwa makanisa sehemu nyingi za dunia ila hawajawahi kukutana na serikali laghai kama ya tanzania, waliouwawa ni wananchi, walijeruhiwa ni raia pamoja na watoto kwa nini serikali inaogopa kutaja majina ya wote kama imeamua kuyataja?.

Wasi wasi uliopo ni kwamba Victor kama kweli ndio jina lake ananafasi ndogo sana kwenye njama na hujuma hizi zidi ya kanisa. Wanaamini kunakitu kikubwa kinafichwa na serikali ya Tanzania dhidi ya uhalifu huu wa kuuwa kanisa na watu wake.

Wanaendelea kusema hata kama majina mengine yanaonekana ni watu ambao serikali inayaogopa ama kwa rushwa ama kwa uswahiba mhalifu ni mhalifu kwanini alindwe hata jina lake, kwanini huyu mmoja aonekane kwamba ndiye mhalifu kuliko wote. Je nani alimpa bomu, nani alilitengeza au kununua nani alilifikisha arusha malengo yao yalikuwa nini.

Serikali yetu imeanza kucheza mchezo wa kujificha. Maoni yangu kwamba baada ya kutokuaminiana kidini ambako tayari kumejengeka ndani ya nchi, mara baada ya bomu kila raia alihisi ni swala la udini. Hali ya hamaki ni kubwa sana, serikali kupitia kwa Nchimbi wakaona watengeneze jina la haraka la Kikristu ili kuwafanya raia watulie. Mbinu hizi za kuzima moto haziwezi kumaliza matatizo. Mkristu anaweza kuwa gaidi, Muislamu anaweza kuwa gaidi, mpagani anaweza kuwa gaidi, mtanzania anaweza kuwa gaidi.

Serikali yetu inakumbatia udini ndio maana inafikiri kidini. Kwanini leo tuogope wahalifu kwa majina yao?? Imeanza lini hii??

Serikali iache kucheza na roho za watu, isifikiri kuwa inauwezo wa kuchezea maisha yetu siku zote.

Watu wa Arusha tuanze kufuatilia huyu Victor AMbrose ni nani? Je alikuwa na marafiki gani kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 6 may kurudi nyuma. Wapi analala, wapi anakula, wapi anapaki bodaboda yake , maisha yake kiuchumi ndani ya mwaka mmoja. Je alibadilika kimaisha within a month , week, or day prior to attack?

Je pikipiki anayoendesha ni ya kwake au yakukodi. Ni nini Tabia za waendesha bodaboda kuwajua abiria wao. Je anamarafiki kwenye kitua chake cha kazi? Je siku ya tukio alitokea kituoni ama hakuonekana kutwa??

Je hiyo bodaboda ilifika na abiria kanisani? Na kama alifika mwenyewe kuna mtu alimwona akirusha kitu kilicholipuka?? Je kulikuwa na ulinzi kiasi gani kanisani, Je polisi walikuwepo na kama walikuwepo walikuwa na usafiri gani au miguu?? Lazima alikuwa karibu na watu akirusha kitu hicho au alikuwa bado juu ya bodaboda?? Alilibeba bomu kwenye nini? Nani majirani zake?, wazazi wake? ndugu zake? ana mke au mchumba? Ni mzaliwa wa wapi mkoa gani, kijiji gani? Ni muumini wa dini gani? Je huwa anahudhuria nyumba za ibada?? Tabia yake kwa ujumla ikoje anavuta bangi? anakunywa pombe? anavuta sigara? Alisoma shule gani primary na je aliendelea na masomo wapi?? lets dig down then serikali ituletee na hao wengine tutampata tu mhalifu wetu. Citizen intelligence is better than a government one. Once we believe on ourselves we can solve all our miseries

Je alikamatwa muda gani baada ya tukio la kurushwa bomu?? Je ni taarifa gani kanisa la Olasit wanayo mpaka sasa?? Je serikali inashirikiana vipi na paroko wa kanisa, walei, askofu lebulu na Askofu padilla au na wao wako kwenye sintofahamu??

Je kuchomwa kuchomwa kwa makanisa mengine kuna uhusiano wowote wa ni la Arusha, Je kupigwa Risasi Mapadri Zanzibar kuna uhusiano wowote na hili hasa ikizingatia mpiga risasi na mrusha bomu wote walitumia pikipiki.

Kwanini Hawa wahalifu wote target yao ni kanisa? Ni nini chanzo cha uhalifu huu. Hata Magaidi ambao wanaogopwa sana duniani aghalabu sana kudhuru makanisa. Sehemu yeyote inayokuwa na uchoma au ulipuaji makanisa huwa ni chuki za ndani baina ya imani na imani. Ugaidi wa Kimataifa hauhusishi Kuchomwa nyumba za Ibada ila ugaidi wa Ndani.

Je Magaidi hawa kama ni wa Saudia walikuwa nia yao ni kumuuwa Askofu Padilla???

Serikali ijibu haya maswali, wananchi aanzeni utafiti wenu pekee, mkitegemea hii serikali isiyojiamini kesho tutaangamia wote.

Angalizo hili swala tusilaumiane kwa misingi ya dini, ila tukubali wapo wengi kati yetu wanachuki za kidini na wapo tayari kuuwa wenzao kwa chuki zao na hawa wapo kwenye imani zote.

Upendo na ukweli utatuweka huru.

Tusiogope tusibaguane huu ndio uwe wakati wa kuwa pamoja kuliko siku zote za maisha. Tuwakatae hawa wahalifu, na punguze hisia zetu za kiimani. Wote tuseme hatuwataki.
 
Nchimbi anasema Victor ndiye aliyerusha bomu wakati JK anasema hao ni watuhumiwa tu sasa cjui nani tumuelewe. serikali inataka kutuaminisha kuwa wakristo ndo wamehusika at the same time inasema tuache kuwa na fikra za kidini.

sasa inawezekaneje sisi tusifikirie kidini wakati serikali yenyewe ndo inafanya mambo kidini, inatoa taarifa za kidini na imetufanya tuamini kwa mitazmo ya kidini
 
Tuache mamlaka zinazohusika zifanye kazi maana hii issue ni nzito pia inahitaji umakini katika kuiangalia maana tukiangalia katika local context uta-link na matukio mbalimbali yaliyotokea katika nchi yetu kuhusu hizi dini mbili kubwa kama wengi tunavyohisi lakini kwa upande mwingine inaweza kuwa mlengwa labda alikuwa ni huyo balozi wa vatican kutokana na siasa za kimataifa na siku zote gaidi akikusudia kufanya tukio lazima kuna watu wengine wataathirika though hawapo kwenye huo mgogoro
 
Nimemkubali sana Kardinali Pengo this time kaja na hoja kama Mtu mzima na kuasa kuwa issue hii asisingiziwe mtu na dini ingine maana yeye ana taarifa zisizokuwa na shaka ndani yake kuwa ni " INSIDE JOB " ndani ya Kanisa kwenyewe hakuko sawaaaa...

Hii taarifa ya Kardinali Pengo wadau wenye Udini mwao vichwani hawaitaki kuisikia kabisaaa...sijui wao walitakaje ?
 
Watanzania kuna watu wanatuchonganisha maana wadau wengi hawakutaka kusubiri ukweli na walichotaka wao ni Sheikh Ilunga tu akamatwe kana kwamba Sheikh Ilunga ana ugomvi nao !!

Baada ya kusikia ni Victor wameshakaa kimyaaa !

Kwanini alivaa kanzu ? Ili iweje ?
Hapo huyo jamaa angejiita Khamisi au Jumaa! ungesikia meengi kuhusu waislamu,Ni Victor sasa! Hapo naingia mashaka na Chadema si walishasema nchi isitawalilke!
 
Yule mbunge wao machachari nina wasiwasi nae sana.alikua anafanya nini arusha wenzake wako bungeni.tukio lilifanywa ili waislamu ndo wabebe lawama,na jumatatu ndo alitakiwa kuwa dom kuwasilisha ushahidi wa jk kuwa mdini...je haiwezi kuwa huyu jamaa kaorganise falseflag ili kuitilia nguvu madai yake?
 
Nikikumbuka sarakasi zinazochezwa kwenye sakata Dr Uli, Mwangosi na hivi karibuni Kibanda, sina imani na jeshi letu la polisi wala UWT. Nahisi kuna "management" kubwa inafanyika katika sakata hili. Tuwape muda!
 
Nimemkubali sana Kardinali Pengo this time kaja na hoja kama Mtu mzima na kuasa kuwa issue hii asisingiziwe mtu na dini ingine maana yeye ana taarifa zisizokuwa na shaka ndani yake kuwa ni " INSIDE JOB " ndani ya Kanisa kwenyewe hakuko sawaaaa...

Hii taarifa ya Kardinali Pengo wadau wenye Udini mwao vichwani hawaitaki kuisikia kabisaaa...sijui wao walitakaje ?
si ndio maana kila thread kumhusu pengo na tamko lake ikiwekwa wanaichomoa zimefika thread kama 20 wanaziondoa cha ajabu mainstream media kama mwananchi newspaper wameiripoti ila hapa wanazinyofoa WHAY?Could it be that someone here has connection with what happen in arusha or someone,somewhere is trying to protect someone or he/she is in a coverup mission.
 
Taarifa zilizopatikana jana jioni, zilieleza kuwa raia hao wa Saudi Arabia, waliingia nchini Jumamosi usiku kwa ndege kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na baada ya tukio Jumapili, waliondoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.QUOTE]

Majasusi waliingia nchini wakafanya uharamia kwa kumtumia mtu anayeitwa Victor Ambrose na mara baada ya tukio wakaondoka nchini kupitia mpaka wa Namanga kwenda Kenya au kusikojulikana! Na hao waliokamatwa wametoka wapi? Manake tumeambiwa wahusika walishaondoka na siyo kutoroka wakipitia Namanga? Taarifa hii ina utata!
 
Tukio lenyewe linaweza lisiwe na udini lakini maswali ya kujiuliza je lengo lake ni lipi. Kwani waliolipua ubalozi wa Marekani walikuwa ni waislamu tu? Hapana. Lakini sponsor wao Al qaeda malengo yao ni yapi kama si ya kidini?
 
niliwahi kusema siku za nyuma kwamba hali si nzuri kama tunavyofikiria, na siku zote mti wenye matunda ndio unarushiwa mawe, kila mmoja wetu anajukumu la kulinda amani yetu, amani ni kitua adimu sana, ikikosekana ndio kama vile utu unapotea, watu wasio kuwa na hatia kuwawa na kukosa viungo, na wasiwasi kila mahali, jirani yangu moja kaniambia hata ukiwa kwenye watu wengi chunguza mwenzako anafanya nini, mmhh! usikute!!
 
Haswaa!
Ila kinachonishangaza hadi leo ni hiki, ni kweli serikali imeshindwa kumkamata sheikh ilunga na Askofu mmpenda au nini kipo nyuma ya hili pazia

Tutashuhudia mengi sana yaliyo nyuma ya pazia

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nadhani wakati wakusema mazingaombwe ulishapitwa na wakati. Kwa kawaida, mtu akisema wamemkamata Julie Jessy, au Yahaya Yahaya, au Peter Barnabas au Jacob John inakuwa ni usanii mtupu. Ingefaa zaidi kwa matukio haya kama wangetaja jina la tatu la mtuhumiwa na si hayo ya kizungu kwa vile kusema hivyo ni kupoliticise issues where politics is not required. Iwapo wamekamatwa 10, kwanini jina moja la Ambrose ndo linaibuka na kila kiongozi? Inamaana ni maarufu sana au profile yake ikoje hapa?
 
Huyo Victor Ambrose abanwe mazagazaga hadi awataje mabwana zake hao waliomtuma halafu wote wauwawe kwa kupigwa bomu hadharani. Ni maoni tu.

Huyo n ilunga tu maana amewaambia mtafute namna nzuuuri ya kushughulika
 
Back
Top Bottom