Nimesoma habari kwa makini sana nimegundua mambo makubwa machache 1. Vicky hakukamatwa na polisi wala hata wakti muandishi wa habari hiyo anamtafuta Vicky alikua hajui kinachoendelea na hata kamanda wa polisi mkoa hajui lolote kuhusu tukio hili 2. Catherine Magige na Mayenga wanabifu na Mh. Vicky la.muda mrefu tu nadhani wengi wanajua hilo 3. Katika habari hii wamewanukuu wadada hao wakisema kua wanatumiwa meseji na namba ambayo vicky amesajili kwa jina la Mdogo wake kwanini asikamatwe huyo mwenye jina la hiyo namba inayotukana kwanza au asitafutwe huyo kwanza?? 4. Wamedai kua wakiangalia location ya mtuma meseji anaonekana anakuaga maeneo ya Bungeni ama namu hotel ama airport je hizo meseji gani za text zinazoonyesha location?? Mbna hautjaona udhibitisho wa TCRA kwamba meseji hizo zimetumwa na mtu akiwa location gani?? Nijuavyo mm text meseji za kawaida huwa hazionyeshi location hata kwa android phone nk.. Lakini pia wamedai kuna kiongozi mkubwa anahusika na amekua akifatilia kwa hatua zote jinsi Vicky anavyowatukana na kwamba kiongozi huyo amekua akimsapoti Vicky anavyowatukana swali ni je wameonaje hizo meseji kwa mkuu huyo?? Maana wakisema location hapa napo walijuaje??
Hapa akili ndogo zinashindana na akili kubwa. Mm nasema hawa wadada wanalao jambo mkumbuke jinsi walivyokua wakimchafua Vicky katka ishu ya Ndoa yake nadhan waliona halikumtikisa na kumaliza kabsa kama walivyotaka na walivyodhani kua lingemmaliza kabisa sasa wamekuja kivingine kwakua ukisoma habari hii kwa makini utagundua kua ni habari ya Kupika haina ukweli na kama haina ukweli na wao wamehusishwa moja kwa moja ni dhahiri ni chuki tu tena zawazi wazi kabisa.
Kama mmepata fursa chunguza habari hii kwa makini sana fikiri mazingira yaliyotajwa kuna uongo mwingi sana.. mimi naamini wanamuonea tu dada wa watu mara waseme yupo karibu na mkubwa nk. kama nyinyi ni wadada kweli si mngekua nyie sasa au yeye kua karibu na wakubwa kinawauma nini?? Kipi alichonacho Vicky nyie Magige na Mayenga hamna?? Kuweni nyie karibu na wakubwa basi kama mnaweza kwa kutumia uwezo na njia alizotumia yeye ili muwe kama yeye..
kweli nimeamini wanawake hawapendani siku zote akiona mwenzake yupo alipotaka awe yeye lazima kitamuuma tu na mbaya zaidi wanawake wengi sana wakifika hapo wanakua wehu na hawana la kufanya kupambana kufika pale wanapambana kwa majungu fitna na kuchafuana.. kama mnayaweza pambaneni kimaendeleo pambaneni kwa mambo ya msingi sio kuchafuana katika mitandao na magazeti.
katika soma yangu ya magazeti sijawahi kuona hata siku moja Vicky kaandika habari akiwashutumu magige na mayenga kwa ubaya lakini pia kama mnakumbuka baada ya ndoa ya Vicky kutofungwa katika mahojiano na mwandishi Simon simalenga wa Clouds fm alimuuliza kama kuna mkono wa mtu ndani ya bunge aliyechangia ndoa kutofungwa Vicky alikataa akasema anaamini ni mpango wa Mungu na naamini vicky alikua anajua fika wadada hawa walikua wanaongoza kwa kutuma meseji kwa mwandishi mmoja wa magazeti ya udaku jina kapuni ambazo kwa taarifa ya mwandishi wa Vicky kamata blog aliwahi kukiri kuzinasa meseji hizo walizokua wanataka ziandikwe magazeti ya udaku zimchafue Vicky lakini alipojaribu kuzichapisha katka blog Vicky alikataa akaombwa zifutwe akisisitiza anamuachia Mungu, kama mlikua mnafatilia mkiyachanganya hayo yote mtagundua kua magige na mayenga ni waongo na wanapika habari ili kumchafua Vicky kwa wivu wa maendelea na hatua aliyopiga vicky ambayo wao hawana na wanaitamani sema akili zao zimegonga mwamba hawajui watafikaje sasa ndo wamekuja na mbinu ya kumchafua kwenye magazeti na mitandao.. upuuzi tu hamna jipya hapa..