vichwa vya viongozi vimejaa viroboto-Antony Lusekelo

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
hebu tujikumbushe maneno ya mzee wa upako halafu tujadili
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo, amesema kuwa serikali imejaa viroboto, ndiyo maana wameweza kuruhusu usafirishaji wa wanyama nje ya nchi bila kujua kuwa hatua hiyo ni kuliangamiza taifa.Kauli hiyo, inaweza kufananishwa na ile ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, aliyedai kuwa baadhi ya wabunge wa mkoa huu wanaomwandama kuhusu sakata kwa uuzwaji wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) wanawaza kwa kutumia makalio badala ya ubongo.Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya kumaliza ibada ya Jumapili iliyofanyika kanisani hapo, Mchungaji Lusekelo alisema kuwa jambo hilo ni kashfa kubwa kwa serikali kuliko zile zilizowahi kutokea za Richmond pamoja na Fedha za Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).Alisema hatua ya ndege ya kijeshi kuingia nchini na kisha kuchukua wanyama zaidi ya 160 na kuondoka nao huku vyombo vya dola vikiwa havifahamu, ni hatari kwa taifa.Mchungaji Lusekelo aliwataka watumishi wa Mungu kuhakikisha wanafanya maombi kwa ajili ya taifa kutokana na kuonekana kama limelogwa; kwamba ndiyo maana viongozi wanakosa maarifa.“Hivi tunaweza kusema tuna viongozi kweli katika nchi hii…uko wapi usalama wa taifa, serikali, uhamiaji na mawaziri wenye dhamana wa utalii hadi hawajui juu ya kuingia kwa ndege na kubeba wanyama kisha kutoweka nao,” alihoji Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako.Alisema kuwa kutokana na kashfa hiyo kubwa, Watanzania hawatasahau kwa miaka yote, jambo ambalo linazidisha chuki kwa serikali.“Tunapozungumzia nchi ni lazima tuzungumzie na vizazi vijavyo, hivi tufikirie kama leo wazee wetu wangeuza wanyama je sisi tungeikuta hiyo rasilimali ya utalii ambayo tunaitegemea?” alihoji.Akizungumzia kuhusu ajali ya meli ya Spice Slanders iliyoua zaidi ya watu 200, alisema jambo hilo linatokana na nchi kugumbikwa na rushwa ndiyo maana hata wasimamizi wa bandari walishindwa kudhibiti tukio la kujazwa kwa abiria na mizigo.Alisema serikali imekuwa ikifanya vitu vya kujenga ukuta hasa pale yanapotokea matatizo kama ambavyo imeamua kuunda tume katika suala la ajali hiyo jambo ambalo haliwezi kusaidia kitu chochote.“Serikali yenye akili timamu haiwezi kuacha tatizo litokee ndiyo ije kuunda tume, kufanya hivyo hakuwezi kufuta machungu ya waliofiwa na wala haitaweza kufufua wale waliokufa,” alisisitiza.Alisema kuwa kama serikali ingekuwa imejijenga katika mfumo wa kuwajibika basi mpaka sasa wasimamizi wa mamlaka za bandari wangewajibika kutokana na kuguswa na suala hilo na kwa heshima kwani huo ndiyo uadilifu.Mch. Lusekelo alisema kuwa viongozi wa mamlaka hizo wakubali kubeba dhambi hiyo kutokana na kuzembea kuchukua hatua na kusababisha vifo vya mamia ya watu wasio na hatia.“Nimeamua kusema ukweli sijutii suala hili hata kama itatokea urafiki wangu na Chama cha Mapinduzi (CCM) utaisha kwa ajili ya kusema ukweli basi katika hilo niko tayari…siwezi kumuona kiongozi wa nchi hajachana nywele nikaacha kumwambia kwa vile atakasirika!” alisemaTanzania daima
 
Back
Top Bottom