Vibonge tambueni kuna tofauti ya kula chakula kingi na kula kula ovyo

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,165
2,000
Nimejaribu kuchunguza sana, vibonge kweli ubonge umekuja wenyewe au umejitakia au umerithi?

1. Kweli kuna unene wa kurithi lakini unue ni ugonjwa, lazma ufanye upasuaji au umtafute daktari kwa ushauri zaidi.

2. Ubonge wa kuja sababu ya maisha mazuri, kutokuwa na wasiwasi na maisha au kutojali chochote, yani unaishi wewe ilimradi mzima tu hutaki kuumiza kichwa kuhusu wengine au vingine. Unaridhika na chochote tu. Mlo wako wa kawaida ila kamili na wanga kwa sana bila kusahau 🍻, juisi matunda n.k.

3. Hawa watu, kwanza wana asili ya uchoyo na ubinafsi. Unakuta hana uwezo mkubwa wa kifedha lakini ni wa kula kula hovyo, kwenye daladala, njiani au popote alipo mwenyewe ana mishkaki ndizi mara anakunywa soda. Hapo anahesabu hajala, akishuka kwenye gari akiona duka atachukua biskuti,a kiona kitumbua kala, mara 🥜, hapo akifika nyumbani atasema hajala toka asubuhi. Atapika chakula atakula kidogo na kudai "chakula hakipandi" ataagiza chips na soda n.k

Hiyo no.3 watu hao wapo wengi sana, wakiambia punguza kula wanajua labda wanakula chakula kingi kumbe ni kula kula bila mpango. Afu ni wengine ni masikini wa kutupa kubajet pesa hawajui, pamoja na kula kula hovyo bila mpango bado atasema hajala kisa sio chakula rasmi.

Kila mtu naamini anaweza kuwa wa kawaida bila unene wa kupitiliza, kwa sababu hata zamani hakukuwa na unene huo, vyakula, milo tunayokula na aina ya kemikali tunazotumia ndio tatizo.
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
16,631
2,000
Unakuta mwanaume anakula hivi.
IMG-20210606-WA0008.jpg
 

new gal

JF-Expert Member
May 4, 2021
750
1,000
Mm binafsi nilikua na mwili nikajichukia nikapanga ratiba zangu vizuri nikaacha mazoea niliuotaja juu hapo kwa sasa,hata sihangaiki kutafuta nguo(suruali)
basi we una mwili wa kula, mimi kula yangu utacheka. Na ndo kwanza nachanika mtt wa kike. Kukonda ni mpaka niugue tena nilazwe kabisa
 

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,165
2,000
mi huwa sivai nguo fupi. na najtanda haswa na mtandio juu! nkivaa vimini au vibukta ujue nashinda ndani na sio sabb ya ubonge ni sabb am muslim
😁Kweli bonge nguo pekee inayoweza kukupendeza magauni tu nguo nyingine waachei mamodo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom