Vibaraka waandamana kupinga mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vibaraka waandamana kupinga mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miela, Mar 9, 2012.

 1. M

  Miela Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilisikia jana kuwa wanahakati binafsi wataandamana kupinga mgoma wa madaktari nikawa na shauku ya kujua wanaharakati hawa wazalendo. Nilipowa kwenye taaarifa ya habari chanel 10, nimeishiwa pozi. Kiongozi woa Salumu tunamjua kuwa ni kibaraka anaefata upepo wa iliko pesa. Ni dhahiri haitoki rohoni mwake. Pia nikamwona Matefu anaeyejitambulishaga ni mwanasheria wa UDSM na hali hajawahi somi pale bali hupita akienda Changanyikeni. Huyu Matefu aliwahi kula hela ya vijana wa shule za sekondari akiwa Kiongozi akapotelea Kenya. Akarudi anajifanya mana CCM. Hawa vijana CCM iwe makini nao ndo watakuja kukijeruhi chama chetu, wana tamaa tu hawana lolote. Nimecheka, nimedharau, hawana Mashiko.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  waache waandae halafu wanaharakati wa kweli washiriki,watajuta kuandaa.shime shime wale wanaharakati wa kweli nafasi hadimu ndio hizoooo!!
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha! Hao sio wanaharakati binafsi bali ni UV-CCM, shame on them
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wananikumbusha Gadaffi alivyokuwa anaandaa watu wake na bendera zao za kijani.

  Lakini mbona hata humu wako wengi tu wanaoandamana???
   
 5. L

  Luluka JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nani asiyemjua salum Aly?ni mtu anayependa kuonekana kwenye tv.tokea amalize chuo alimiss kuongea kwenye media thats why akaona avamie uharakati bila hata kufikiria.
   
 6. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  mwanaharakati gani wewe unamuona wa ukweli? Wote matumbo ndio isue. Na mumshukuru sana Rais wa sasa kwani amewaachia mno,sasa hivi kila mtu anatanua kinywa vile apendavyo. Hakika hii hali kwa taifa sio mwelekeo mzuri.
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Huyo Salumu na vijana wengine wale waliokuwa kwenye kipindi cha Je Tutafika kinachorushwa na channel tenkwenye maada ya CCM waitakayo nimeshangaa sana kuwaona ndio wanaharakati. Nimejiuliza maswali mengi kama UVCCM imeamua kuwaanza harakati? na Harakati za nini hasa? huku ni kutapatapa na kuchezea akili za watu. Niliowaona kwenye taarifa ya habari ni wale wana ccm. Kweli usipokuwa na akili kwa maswala kama haya ni shida tupu na kama huyo Salumu ni mwanasheria basi CCM ndio inaenda kwenye kifo chake
   
 8. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Si warudi shule wakasomee udaktari ili wafanye kazi kwa uzalendo. Wanapiga kelele nyingi ukiwauliza wana-belong kwenye kingdom gani hawajui.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wapigine picha hao vibaraka, na zibandikwe kwenye hospitali zote Dar.
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Thanks to the constitution not an individual you dummy, umuhimu wa kutoa shule ya katiba unazidi kujionyesha.

  Back to the strike, wananchi wanapaswa kuandamana kumshinikiza incompetent Prez. kuwaondoa wanasiasa wawili kati
  maelfu ya wanasiasa tusiowaitaji anyway.
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wewe unaona kabisa dereva analielekeza gari kwenye korongo halafu bado unamshukuru dereva..ziko sawasawa kweli. Ajabu mtu anayekuambia shuka humo unamona mjinga.
   
 12. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Maandamano ya hawa matapeli na wachumia tumbo ni janja ya kitoto ya Kikwete kutaka kuzima madai halali ya madaktari. Je atafanikiwa? Hawa wanaoandamana ni waroho kama fisi wanaoweza kuwauza hata mama zao ili mradi tonge liende kinywani. Kwao taifa ni matumbo yao na njaa zao. Yeyote awezaye kuwatumia hata kama ni shetani watamtumikia ili mradi wapata mabaki ya mafisadi na kujaza matumbo yao yasiyo na shukrani. Wanatumia utumbo kufikiri badala ya ubongo. Wanangu, walaani wezi hawa wa mchana. Kesho utawasikia mzee wa Upako na Kalokola na baadhi ya mashehe wakimwaga sumu. Nadhani mtasikia wazee wa Dar es salaam wakiunga mkono ***** wa Kikwete muda si mrefu.
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Aisee wakati serikali ya sisiem inapingana na maandamano hata kwa kuwapiga risasi za moto waandamanaji, safari hii ndio wao wamekimbilia kuandamana? Ama kweli simba akizidiwa hula majani. Wamekimbilia pia mahakamani lakini kwa kiwewe kilichowashika hawakuona kama hukumu ya mahakama itawanusuru. Ndipo wakawaomba madaktari waende ikulu ili wafanye majadiliano. Sasa sijajua kama kikao cha ikulu kinajadili hukumu ya mahakama au vipi. Na kufanya hivyo sijui kama hawaoni kuwa wanaingilia uhuru wa mahakama.
  Lets wait and see.
  .
   
 14. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hiyo move nzuri tunataka maandamano ya wanaharakati wanaounga mgomo yaitishwe haraka na Kikwete avumilie.Hayo yafanyike haraka ili kujua ukweli
   
 15. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kumbe ndiye yule nilimsikiliza hamna kitu kumkichwa walikuwa wanatema pumba hadi aibu.
   
 16. vimon

  vimon Senior Member

  #16
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  kwenye maandamano kesho kila mtu aje na bango llake lakuiponda serikali tuone kama hawataishia kumwaga maji washa
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu umefanya vibaya kuwataja maana wanajitengenezea uadui na madaktari wakati hawana uwezo wa kutibiwa nje ya nchi. Ni mwendawazimu pekee atakayekubali kushawishiwa kuwapinga madaktari. Kwanza ukiangalia madai yao ni kwa faida ya wagonjwa. Kama watakuwa na capacity ya kutambua magonjwa (ie kuwa na vifaa vya kisasa na mazingira bora) vifo vingi visivyo vya lazima vitaepukika.
   
 18. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  nimewaona itv na wale ndugu zetu wa ubwabwa...eti serikali iagize madaktari kutoka nchi marafiki na tanzania...yaani hii nchi bila 'vikofia' nadhani tungekuwa tumepiga hatua japo ndogo ya maendeleo maana watu wengi wameshaamka ila hawa wenzetu wengi wao ni ma nincompoop kwa hiyo wanatumika kirahisi kuturudisha nyuma...!
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Mar 9, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe unaishi sayari gani maana kwa vyovyote vile huwezi kuwa unaishi dunia hii tunayoishi. Tuko karne ya 21 na imebaki tu miaka 88 na siku 297 tuingie karne ya 22, please grow up dude!
   
 20. L

  LISAH Senior Member

  #20
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wao wataruhusiwa kuandamana?
  Hapa ndipo tutaona double standard za hawa jeshi la polisi kwa raia wake
   
Loading...