Vibaraka wa CCM ni kama mshumaa

kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
19,011
11,942
Unawamulikia wengine wakati huo wenyewe unateketea,
(1) yaani wako radhi kupinga kila hoja ya msingi ili kutetea ulaji wa wakubwa,

(2)Wanashinda kutwa na pengine kukesha ili kuhakikisha wanavuruga mawazo ya wapenda maendeleo.

(3) Wanajifanya vipofu au sijui ni vipofu? Hawaoni uchafu unaofanywa na viongozi wa CCM.

(4) Hawataki kabisa kusikia ukweli au kuambiwa ukweli,wao watakanusha na kupinga kabisa jambo lililo wazi kabisa.

(5)Kwa kuwa wao wako mjini wamewasahau kabisa ndugu zao walioko shamba ambao kwao kunywa chai tu ni anasa.

(6)Wao wenyewe wanajua kabisa ugumu wa maisha,ila kwa ujinga usiokuwa na faida wanaendelea kusifia na kuyatukuza mawazo potofu ya viongozi wa CCM.

(7) Hela ndogo wanazohongwa zinakuja kuwatesa miaka 5 wananyonywa mpaka damu bila huruma.

(8) Wengine ni masikini wa kutupwa lakini bado wanaipigania CCM kwa nguvu zao zote.

(9)Zawadi ndogo ndogo wanazopewa pamoja na ahadi feki wanazopewa zinawafanya kutotafakari juu ya unafiki wa viongozi wa CCM.

Amkeni jamani Mmewamulikia vya kutosha angalieni msije teketea na kutupwa kama mshumaa uliobakiza utambi 2015 haiko mbali.
Mungu ibariki Africa,Ibariki Tanzania.
Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom