MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,181
- 5,429
Habari zenu wakuu!.
Hakika duniani kuna zaidi ya mambo. Huwezi jua kwanini hufanikiwi, kwanini huolewi, kwanini una mali ila vitu vingine umeishia kuvitamani, kwa nini miaka mingi unafanya biashara ila ukifikisha mtaji kiasi fulani mambo yanaharibika.
Natoa kitu kidogo nilichokiona ktk ulimwengu mwingine ambao wengine tunaujua na wengine hatuujui.
Ukifanikiwa kuanza kusoma huu uzi basi hakikisha unaumaliza kwa faida yako na uzao wako pia na jamii yako.
Mimi mla panya wa sumbawanga nililala kama ilivyo ada kuwa tukichoka baada ya kazi za kutwa usiku tunalala kupumzika. Ilipofika usiku mnene alinijia mtu nisiye mjua mwanaume handsome aliyekuwa kavaa vazi refu jeupe.
Akaniita nikaitika akasema leo twende nikuzungushe uujue mji huu ulivyo. Basi nikaongozana naye ktk mji ambao ni moja kati ya majiji yetu hapa Tanzania.
Tukiwa njiani tulikuwa hatuongei mpaka alipotaka nione jambo fulani. Mara ya kwanza alinipitisha ktk makanisa mbalimbali. Ktk kanisa la kwanza niliona kibao chenye ratiba za ibada juu ya mlango wa kanisa.
Nikiwa namalizia kusoma kile kibao ghafla maneno yale yakapotea yote yakaja maneno mengine kama naona video yakasomeka, Ktk kanisa hili marufuku watu kuzidi mia tano arobaini ktk ibada moja.
Tulienda makanisa mengi tu niliona yale yale isipokuwa kilichotofautiana ni idadi makanisa mengine ilisomeka marufuku kuzidi 50.
Baada ya hapo tulienda mahali ambapo palikuwa na maduka mengi mno mithili kama sokoni. Nilipokuwa nasoma yale mabango yao juu ya milango juu ya bidhaa wanazouza ghafla maandishi yakapotea yakaja maandishi mengine yakasomeka, Marufuku kuuza zaidi ya milioni moja na nusu. Hii hali niliiona ktk premis nyingi ila ilitofautiana kiwango tu.
Ajabu zaidi lipo duka alikuwa anauza baba mmoja mtu mzima kibao kilisomeka Marufuku kununua sana hapa ni kuuliza bei tu. Hii ndiyo dunia tunayoishi ndugu. Endelea kufuatilia.
Baada ya hapo nilipelekwa nyumba moja ambayo nakiri hadi sasa sijawahi kuingia nyumba nzuri kama ile achilia ndotoni. Nyumba imesheni kila starehe nikaingia tukakakaa tukakaribishwa humo mama wa nyumba kashiba kwelikweli baba wa ukweli.
Tukiwa hapo ghafla juu ya meza kikaota kibao chenye maandishi yaliyosomeka, "Marufuku nyumba hii kuwa na amani kugombana sana ".
Hapo tena tuliondoka tukaenda sehemu nyingine ambayo tulikuta nyumba mbovu ukweli haielezeki vema. Upendo na jinsi tulivyopokelewa hakuna mfano. Yule mama wa nyumba alitukaribisha ktk vigoda vya kuchonga miguu mitatu vya zaman tukakaa. Tukiwa mle mimi yule mtu na baba wa nyumba ile na mkewe nikaona taratibu kibao kinachomoza ardhini Kama uyoga kikasomeka, "Marufuku nyumba hii kugombana ni amani tu na marufuku kuwa na mali iwe shida.
Mwisho tulienda eneo ambalo ni kama mnadani niliona watu wa aina mbali mbali. Zaidi mgongoni walikuwa wana maandishi yaliyosomeka tofauti tofauti. Siwezi kukumbuka wote ila nanukuu wachache.
"Marufuku kuzaa wewe ",Marufuku kumiliki pesa zaidi ya laki tatu na nusu ",Marufuku kuvuna mazao zaidi ya gunia 13 shambani kwa zao moja ".;Marufuku kununua kitu cha maana ununue pombe na wanawake".Marufuku kusoma.
Ukweli siwezi kueleza yote niliyoyaona, hapo nikageuka nikamtazama yule jamaa kwa mshangao naye akaniuliza akinitaja jina langu "Unasemaje"!.
Nikamuuliza nini maana ya hivi vitu nilivyoona?.
Akaanza kujibu, akaniambia ulimwengu huu unaongozwa na vitu vitatu. Wewe, ama shetani, ama Mungu, yaani unapofanya jambo waweza kulitimiza kwa ama nguvu yako, ama kwa nguvu ya shetani ama kwa nguvu ya Mungu.
Akianzia kwenye makanisa akasema makanisa mengi yanakuwa driven na shetani watu wakijitahidi kuhubiri wakapata waumini wengi idadi ikizidi ile ya marufuku basi shetani humuinua mmoja na kuwagawa watu na hivyo kuzaliwa kanisa jipya. Uthibitisho ongezeko la madhehebu na makanisa na hata mpasuko wa imani zote chanzo ni kuzidi idadi iliyopo kwenye marufuku.
Kuhusu yale maduka kuna watu wanauza pesa kidogo sana lakini idadi ya wanaouliza ni kubwa sana na wakijua bei hawarudi tena.
Watu wanaviwango walivyowekewa na shetani ktk biashara zao na ikitokea mwenye duka akauza zaidi ya kiwango kile basi akirudi nyumbani atakuta matatizo mengi yatakayomtafuna pesa zaidi. Mfano dada yako yuko hospitali hana hela, mdogo wako amefungwa kwa kosa la kusingiziwa kuua na mengine yafananayo na hayo ilimradi tu ile iliyozidi ipotee. Hii ndiyo dunia tuishimo.
Kuhusu ile nyumba ni kwamba wote unaowaona wamebarikiwa na mali wengi wao wana shida ndoa zao ni pasua kichwa full kugombana ilimradi tu wasifurahie zile mali zao.
Wale masikini uliowaona shetani kawaamrisha wasigombane na pesa mali wasipate. Lakini marufuku kugombana.
Vibao ulivyoviona kwa watu migongoni ndiyo laana walizopewa waishi nazo bila kuelewa. Mwingine alionekana malaya kupindukia kwa kuwa jini alilobebeshwa lilikula mbegu za wanaume tu kama chakula hivyo liliposikia njaa lilimtekenya akapandwa na hisia hadi anamtafuta mwanaume lengo tu lipate kushiba.
Nikaambiwa ili watu wafanikiwe hawana budi kujua vibao vyao vya marufuku vinavyozingira maisha yao. Imani za wanadamu ni za kivivu mno kutokana na hali hiyo wanatoa mwanya wa kudhibitiwa na shetani.
Wang'oe hivyo vibao vya marufuku ndipo watafika wanakotaka.
Baada ya hapo niliamka nikiwa natetemeka.
Ndugu zanguni unapolala ukaota tambua Mungu ana kusudi na ndoto hiyo. Mtambo wa ndoto saver zake hazipo duniani zipo kwa Mungu. Mungu hukuletea ndoto kulingana na majukumu uliyopewa hapa duniani.
Ndoto za baba hazifanani na za watoto. Ndoto za askofu mkuu wa kanisa lako ama shehe mkuu haziwezi fanana na za waumini wao.
Ndiyo maana ndoto ya farao kama raisi wa nchi tafsiri yake ililenga kuwaokoa wamisri wote na jamaa zao wengine.
Usidharau unachoota ndotoni kina maana kamili na halisi inayoreflect maisha yako. Ukiamua kuwa mchawi basi amua kwelikweli na ukiamua kuwa mcha Mungu pia amua na ondoa ubabaishaji.
Mfano waweza ota panzi wana kufuata au kuwaona tu panzi ama ukaona jangwa, ukame, jua kali ni ishara kuwa utapita kipindi kigumu maishani.
Ukaota umevaa shati bila suruali ni ishara kuwa msingi wako wa maisha ni mbovu tengeneza msingi imara.
Ninawatakia tafakuri njema ktk andiko hili mkaongozwe vyema kama nilivyoongozwa vyema nikiwa na baba yule. Mungu awafunulie mengi msiyoyajua kwa njia ya ndoto na maono.
Tunatumikishwa na shetani bila kujua siku zote.