Vibanda vya Machinga Complex vyabomolewa, Machinga wahaha

Tanzania ya viwanda ndo hii kweli?
 

Attachments

  • IMG-20170403-WA0022.jpg
    106.4 KB · Views: 40
  • IMG-20170403-WA0020.jpg
    61.9 KB · Views: 40
Gharama za pango zipo juu,machinga hawaimudu na ndiyo sababu ya kujenga vibanda nje..
Kweli kabisa, pia vilivyokuw vinagaiw walijipa wenyew wakubwa kwanza pia kod ni miezi 6 na mwaka. Kwa mmachinga inamuiwa vigum kumudu
 
Katika hili tuweke pembeni tofauti zetu za kisiasa,, nitashangaa sana kama kuna mwana CHADEMA mwenzangu eti atalipinga hili. Hapa halmashauri ya jiji wako sahihi kabisa, haiwezekani kwenye jengo zuri kama hilo nyie mnakuja kuweka uchafu wenu hapo. Jiji limefanya vizuri kuwafurusha,, waingie ndani tu hakuna namna na nitamshangaa sana Rais kama ataingilia hili eti waachwe kama alivyofanya Mwanza kipindi kile aache kutafuta kiki za kitoto!! Kama kodi ya jengo la Machinga complex ni kubwa Jiji liangalie utaratibu wa kupunguza gharama wasitafute utajiri wa haraka haraka! Na uzuri Jiji linaongozwa na UKAWA!!
 
jingo lina masharti makubwa na ni gharama ukilinganisha na uhalisia wa biashara. wale jamaaa wamekua mkombozi kwa mtanzania mwenye kipato cha chini. nimefikiria zaidi ya kile ninachokijua
Sasa mbona hawataki wenzao wakodishwe?
Wamegeuka joka la mdimu, ndimu hawali lakini hawataki wenzao kuzichuma
 
kwa hiyo walikataa kukaa ndani wakaweka vibanda nnje ya jengo la biashara ili watu wasiingie ndani wakija waishie hapo nnje, wao hawalipi kodi huku wanauza, walio ndani wanalipakodi lakini hawauzi.
Sasa uliza humo ndani nafasi ipo basi, ni majanga tu
 
Mazoe yanatabu.Wamachinga hawaabiwi ukweli kutoka kwa wanasiasa,imekuwa ni kawaida hata viongozi wajuu,kutoa matamshi kigeugeu kama mtaji wa siasa.
Mwisho wake ndio haya.Aliyaanza Mzee Ruksa kuwa wasibuguziwe,kayapalilia Mkapa na Kikwete na sasa Magufuri.Mmeyalea yamekuwa dawa ni kurudi kwenye drawing board Serikali,wamachinga na wadau wengine.
 
Ni Tanzania pekee unakuta mtu kaandaliwa sahani nzuri yeye anaamua kulia chini! Hili zoezi Liwe endelevu kariakoo imekuwa Kama gulio
 
Hili suala la daladala kuegesha nyuma ya kituo ni kero sana halafu anaacha mkia barabarani,tatizo waswahili kila kitu ni siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…