Vibali vya kusafiri nje nchi toka Ikulu viwe vya kielectroniki

nyamagaro

JF-Expert Member
Feb 25, 2010
394
102
Kuna minongono mingi sana juu ya vibali hivi vya kusafiri nje nchi vinavyotolewa na ikulu vinachelewa sana au pengine havitoki.Unakuta mtu umeomba kibali mwezi mzima, lakini mpaka siku ya safari kibali hakitoki. Kwa dhana JPM ya kupunguza urasimu, hii ya vibali toka ikulu haijakaa vizuri.

Watanzania wengi kwa sasa wanakosa fursa muhimu sana za nje ya nchi kwa sababu ya kuchelewa au ktotoka kwa vibali hivi. Kuna jamaa yangu (Researcher) ameniambia kuwa alikuwa asafiri tarehe moja lakini hadi leo kibali hakijatoka.

Napendekeza, huu mpango fanyike electronically ili kupunguza huu urasimu wa mafile.Applicant akishajaza form na kupitishwa wizarani, anaweza kufanya scanning na kutuma kwa njia ya mtandao.
 
Kwani huyo rafiki yako alijaza kile kipengele cha kama usipoenda nchi inapata hasara gani? unaweza kutujilisha ili tuanze kulalamika hiyo hasara tuliyopata kutokana na huyo rafiki yako kutokwenda.
 
Napendekeza, huu mpango fanyike electronically ili kupunguza huu urasimu wa mafile...Applicant akishajaza form na kupitishwa wizarani, anaweza kufanya scanning na kutuma kwa njia ya mtandao.

Nadhani wazo zuri na hili litasaidia Ikulu kufanya maamuzi kwa wakati !
Hata fomu inaweza kutengenezewa utaratibu wa njia ya mtandao isipokuwa viambatanisho vingine vya mwaliko na mazagazaga mengine kuhusu Safari inkuwa scanned na kutumwa na original inabaki kwenye Taasisi au Ofisi ya Muombaji kwa matumizi ya uhakiki wa baadaye wakati wa ukaguzi.
 
ukiona hakijatoka labda kile kipengele cha kama taifa tunafaidikaje au tutapata hasara gani hawajakuelewa... halafu ukiomba si lazima kupata .. sema wajitahidi waseme hatutoi
 
Back
Top Bottom