Vibaka wapora, wabaka Chuo Kikuu Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vibaka wapora, wabaka Chuo Kikuu Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BabuK, Apr 28, 2012.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]WAKAZI na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John mjini Dodoma, wako katika hofu kubwa kutokana na kuibuka kwa makundi ya vibaka ambayo licha ya uporaji, yamekuwa yakijihusisha na ubakaji na ulawiti, hasa usiku.

  Kutokana na hofu hiyo, wanachuo wameshauriwa kutembea kwa makundi kwa lengo la kujihami na wahuni hao.

  Hayo yamethibitishwa na Msemaji wa Chuo hicho, Karim Meshack, aliyekiri kuwa waporaji hao ni tishio katika eneo hilo, kiasi cha kushauri wanafunzi kutembea kwa makundi ya watu watano hadi sita.

  Meshack alikuwa anathibitisha habari ambazo gazeti hili lilizipata zikidai kuwa, kuna matukio kadhaa ya uporaji, huku baadhi ya wanafunzi wa kiume wakidaiwa kuporwa mali na kulawitiwa.

  “Ni kweli katika siku za katikati kulikuwa na matukio ya wanafunzi kupigwa na kuporwa vitu kama simu, lakini hayo mengine nami nayasikia juu juu,” alisema.

  Hata hivyo, mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho alidokeza kuwa, kutokana na hofu ya vibaka na matukio mengine wa makundi ya watu wasiofahamika, kasi ya mahudhurio ya watu wanaojisomea nyakati za jioni imepungua

  “Zamani ikifika saa moja au mbili wanafunzi kibao wanajazana kwenye ‘mdigrii’, lakini sasa ikifika saa mbili wanafunzi wanakuwa wa kuhesabu kutokana na kila mmoja kuwahi kurudi anakoishi kwa kuogopa vibaka,” alisema.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, alipoulizwa juu ya matukio hayo, alisema hana taarifa kwa kuwa hakuna tukio lililoripotiwa.

  “Kama kuna matukio yaripotiwe ili uchunguzi ufanyike na wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua,” alisema huku akiwataka wananchi kuwa na tabia ya kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu ili wahusika wabainike na kukamatwa na si kukaa kimya.

  Diwani wa Kikuyu Kaskazini, Johnick Kisasi, alisema kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi kushindwa kutoa taarifa za vitendo kwa kihalifu katika Serikali za Mitaa hali ambayo inafanya wahusika washindwe kuchukuliwa hatua.

  “Matukio yapo, lakini hakuna taarifa rasmi kuwa wamefanyiwa vitendo hivyo, ila ni kweli tunasikia wanafunzi walilawitiwa na mwingine kuvuliwa nguo, sasa kama waliofanyiwa vitendo hivyo wameamua kuwa kimya, sisi hatutakuwa na taarifa rasmi,” alisema.

  Alikiri kuwa vitendo vya kihalifu vimekithiri katika kata hiyo na juhudi zinahitajika ili kufanya eneo hilo kuwa salama kama ilivyokuwa siku za nyuma.

  Imeelezwa kuwa, moja ya mbinu zinazotumiwa na vibaka hao nyakati za usiku ni kupanda juu ya miti kwa lengo la kuwavizia wapita njia na pindi wanapokaribia maficho yao, hushuka na kudhuru watu wasio na hatia.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  He kajipange urudi tena maada maana kichwa cha habari hakiendani na maelezo ya mada...pole nitarudi tena kuangalia
   
 3. t

  thengoshahimself Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huwa inachanganya sana ukisema chuo kikuu dodoma unavuta attntn ya watu kuwa ni udom.change headng plz
   
 4. r

  rchaga Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Badilisha kichwa cha habar yako!
   
 5. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  haki ya nani huku siku izi hapafai, wanafunzi wanaogopa kutembea na laptop usiku, au kurudi peke yako kuanzia saa nne usiku, maana hawa vibaka wanakula tigo,
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Hao wanafunz nao mayai tu,inabidi wauwe kibaka mmoja ili iwe fundsho.
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,492
  Trophy Points: 280
  Poleni.
   
 8. Mfarisayomtata

  Mfarisayomtata JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 417
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Tuigeni SAUT mwanza, vibaka wa mwanza wanapaita huku machinjioni hawafiki kabisa. Kazi yetu kuua tu.
   
 9. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  cant imagne cku wakikukamata na unavyopendaga kutembea na vikorokoro vyote simu, kamera, laptop...teh! Watakufilisije?
   
 10. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  si ndo hapo sasa!!!! wao wanaleta woga
   
 11. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,471
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
   
 12. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  rekebisha kichwa cha habari
   
 13. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Chuo cha dini bana usiue ni dhambi.
   
 14. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Lakini c ushaelewa bana na wewe!
   
 15. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hata mimi nimepata taarifa ya kama watu sita hivi kufanyiwa unyama huo.poleni sana
   
 16. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,318
  Trophy Points: 280
  Mtoa maada inaelekea umevutiwa na KULATIWA.
   
Loading...