Vibaka Stendi ya Ubungo, mamlaka ziko wapi?

Vibaka Stendi ya Ubungo, mamlaka ziko wapi?

Na hizo mia mbili mbili sijui wanazionaje pale getini kama hamna taa
 
Hatari sana hapo Ubungo...Dsm siji tena;Juzi wamekwapua kamkoba ka bibi yangu kana Nokia ya Tochi,Chuo cha sala na dawa za Bibi ambazo mkoani hazipatikani zaidi ya Dar.Tulisafiri kuzifuata hizo dawa huku huku Dsm kila baada ya miezi6!!Ikabidi safari ihairishwe tujipange kununua tena dawa maana inakuwa haina maana kuendelea na safari.

Halafu unaibiwa na watu wanakuona tu,wanabaki kusema "Hao ndio ajira yao"...Yaani unaweza uwa mtu hivihivi,kwa kweli nikikuta kibaka anapigwa maeneo ya Ubungo hata kwenzi tu ntamtandika au kumfinya kabisaaaaa ili niridhike.Wanachaji 200 sijui 300 bila hata EFD,ndani hakuna hata Terminal Building kujikinga na jua wala mvua,unalipa mlangoni na bado ndani ukiingia inabidi ulipie na huduma ya choo.Giza totoro kama mapango ya Amboni
 
Kuna rafiki yangu aliibiwa walet ilikuwa na hela 120000 na vitambulisho,baada ya kuutangazia umma pale ubungo wengi walisikitisha sana wakamshauri aache namba yake ya simu.

Siku ya pili alipigiwa simu ya kumwambia vitambulisho vyako viko nyuma kabisa karibu na ukuta sehemu ya kukusanya takataka.

Yaani ubungo ni tatizo sana wahusika sijui wako wapi!?
 
Mamlaka hazihitaji kutumia nguvu nyingi kufukuza vibaka pale ubungo, au kwingineko nchini..
Only two things to be done out there,
1.modernise that old school terminal
2.Reform the system, ule mfumo mzima wa usafirishaji unahitaji kuboreshwa,


Watu bado mnachanganya mambo, pale Ubungo hakuna terminal , kuna eneo ambalo mabasi ya kwenda mikoani hujusanyika na serikali hukusanya pato toka kwa abiria na wasindikizaji..

Siku chache Baada ya UDART wapiga debe wengi wa daladala toka morogoro road wamehamia ubungo, hivyo kufanya idadi ya Vibaka kuongezeka pale.
Always nzi hufuata uchafu, huwezi kuwaondoa nzi kwa kuwaua au kuwafukuza, unless uondoe uchafu..
.. ule msongamano usio wa lazima unasababishwa pia na makampuni ya usafiri ambayo huwapa visenti Fulani kila wakileta abiria..that's uchafu nnaozungumzia..
Ndio maana kampuni standard kama shabiby huwezi ona mpiga debe, maana tayari wanajiamini na services zao hivyo wanajua hata bila mpigadebe abiria tutawafuata ofisini kufanya booking..na hivyo ndio inatokea yaani safari zangu za Dom naondokaga home nikijua naenda kusafiri na shabiby (Very comfortable)
Pale Ubungo hata kama husafiri ukipita tu wale wapigadebe ambao ni magenge kwa magenge watakusumbua sana, watakuzonga na usipokuwa makini watakuibia.
Ile terminal ikiwa modernized, na makampuni yakafanya some serious investment, na mamlaka husika zikasimamia mfumo vilivyo, haya mambo yatabaki historia.
 
Mhnnn.... I can imagine how hell it is for visitors.
Ndani ya stendi ubungo ni Kama ghetto au kichakaa cha wahalifu....abiria wanaibiwA,na ukiwa mnyonge utaonewa mfano ukikapaki gari watakuja watu watajifanya kukufungua Raimi na watataka hela.....ukiwa na mzigo watakuja watu wanajifNya maaskari na kukutishaaa wakukagueee....yaani mule ndani ni u.... Mtupu
 
IMG_7101.jpg

​
Wanajamvi naomba kuweka wazi wizi uliokithiri ndani ya stand ya Ubungo! Kuanzia alfajiri hadi saa 5 usiku wasafiri, wasindikizaji wanakumbana na vibaka wakiwa kwa makundi.

Wanaiba vioo, side mirror na kuvunja magari yanayoegeshwa ndani ya stand. Wasafiri wanaporwa sana. Kuna tatizo la usalama na taa ndani ya stand!

Mamlaka ipo kweli ? RC yuko busy kwenye media na matamko yasiyotekelezeka!
Hapo niyaona mabasi: Color Star, Champion, New force, Alsaedy,Hai, BM n.k,
 
Mnaona kituo cha mabasi pale msamvu Morogoro?chakwanza afrika mashariki,wenzenu wanawaza maendeleo nyinyi mnashinda kwenye Tv na Radio MAWINGU munajinadi,vipi bank ya NMB wamesha ludisha pesa za wafanyakazi hewa?
 
hahaaaa umenikumbusha mbali hawa abiria wanaochelewa kufika wanaibiwa sana maskini ila hata wa kumlalamikia hamna.
Kama mnavyoforce watu kutoa 300 simamieni na usalama pia
 
Huwa nikifika ubungo nashindwa kujua kama ni kituo cha mabasi au nice mipenyo ya vibaka
 
Vibaka hapo ubungo jiandaeni na muondoke haraka, hapa tukimalizana na wasafi records, kunaenda kwenye sensa ya jobless na kuwarudisha makwao na baada ya hapo tunatia timu hapo ubungo kituoni, watatutambuaje hao vibaka!
 
Natamani Mkuu wa mko@ au Mkuu wa wilayaaa itokeee siku waendeee Hapo alafu wapigweee kabal....... Ndiyo wafahamu hali Halisi ya Hapo
 
Kituo cha Ubungo ni International kwa kuwa kinaingiza mabasi toka nchi mbali mbali hivyo kuwa na giza na vibaka wengi ni aibu kwa uwongozi wa jiji. Meya na municipal husika fanyeni jitihada kuondoa kero hapo kituoni siyo kusubiri ushuru tu toka kwa mkandarasi
 
Ubungo Sasa ni Salama, na tumezindua Lango la kuingia na kutoka humo ndani kwa upande wa kanisa la Agape. Changia mapato.
 
Back
Top Bottom