Vibaka Stendi ya Ubungo, mamlaka ziko wapi?

Lambardi

Platinum Member
Feb 7, 2008
17,941
20,287
IMG_7101.jpg

Wanajamvi naomba kuweka wazi wizi uliokithiri ndani ya stand ya Ubungo! Kuanzia alfajiri hadi saa 5 usiku wasafiri, wasindikizaji wanakumbana na vibaka wakiwa kwa makundi.

Wanaiba vioo, side mirror na kuvunja magari yanayoegeshwa ndani ya stand. Wasafiri wanaporwa sana. Kuna tatizo la usalama na taa ndani ya stand!

Mamlaka ipo kweli ? RC yuko busy kwenye media na matamko yasiyotekelezeka!
 
Wanajamvi naomba kuweka wazi wizi uliokithiri ndani ya stand ya ubungo! Kuanzia alfajiri hadi saa 5 usiku wasafiri , wasindikizaji wanakumbana na vibaka wakiwa kwa makundi.....wanaiba vioo side mirror na kuvunja magari yanayoegeshwa ndani ya stand , wasafiri wanaporwa sana..........kuna tatizo la usalama na taa ndani ya stand ! Mamlaka ipo kweli ? RC yuko busy kwenye media na matamko yasiyotekelezeka!

Usijali, ngoja kwanza tuhakiki wakazi wa Dar na kazi zao, tumalizane na mashoga, ombaomba, bajaji na kuwapandisha walimu bure kwenye daladala, then tuitokomeze shisha kabla hatujavalia njuga hili tatizo lako dogo linalokusumbua. Polisi wetu wako bize na majukumu haya...

Ahsante kwa kutuelewa......
 
mule ndani kuna giza totoro, hakuna cha sungusungu wala mgambo, ni kama hakuna utawala. jambo wanaloweza simamia vizuri ni ukusanyaji wa zile 300.
 
Hiyo sio upcountry bus terminal ni chaka la mabasi na wasafiri, no proper service at all shida tupu,
 
Usijali, ngoja kwanza tuhakiki wakazi wa Dar na kazi zao, tumalizane na mashoga, ombaomba, bajaji na kuwapandisha walimu bure kwenye daladala, then tuitokomeze shisha kabla hatujavalia njuga hili tatizo lako dogo linalokusumbua. Polisi wetu wako bize na majukumu haya...

Ahsante kwa kutuelewa......
Hahaha hahaha hahaha dah umenichekesha sana mkuu wewe ni noumer
 
Wanajamvi naomba kuweka wazi wizi uliokithiri ndani ya stand ya ubungo! Kuanzia alfajiri hadi saa 5 usiku wasafiri , wasindikizaji wanakumbana na vibaka wakiwa kwa makundi.....wanaiba vioo side mirror na kuvunja magari yanayoegeshwa ndani ya stand , wasafiri wanaporwa sana..........kuna tatizo la usalama na taa ndani ya stand ! Mamlaka ipo kweli ? RC yuko busy kwenye media na matamko yasiyotekelezeka!
Kabla ya ujenzi wa ngazi za daraja palikuwa na kituo cha polisi pale stendi, cha msingi ni jeshi la kuimarisha polisi kuimarisha ulinzi na doria zifanyike pia taa ziwekwe mle ndani maana pana kiza sana hivyo kupelekea kushamiri vitendo vya kihalifu.
 
Wanajamvi naomba kuweka wazi wizi uliokithiri ndani ya stand ya ubungo! Kuanzia alfajiri hadi saa 5 usiku wasafiri , wasindikizaji wanakumbana na vibaka wakiwa kwa makundi.....wanaiba vioo side mirror na kuvunja magari yanayoegeshwa ndani ya stand , wasafiri wanaporwa sana..........kuna tatizo la usalama na taa ndani ya stand ! Mamlaka ipo kweli ? RC yuko busy kwenye media na matamko yasiyotekelezeka!
Mkuu nimetoka ubungo kumsindikiza ndugu yangu yaani Ubungo ni giza tororo hivi kweli wameshindwa kuweka taa pale aisee! RC Dar hebu vamia siku moja pale saa 11 asubuhi uone maajabu.
 
Kama wangedigitize mfumo wa ukusanyaji mapato na fedha yote ikaenda serikalini kwa miaka yote basi tungeweza kuwa na kituo kizuri cha kisasa, lakini hakuna mwenye uchungu na maboresho ya kituo hicho kila mmoja anaboresha tumbo lake
 
Eeeeh simu za tochi zitumike
Na ariyesema haya arete vithibitisho hapa sentero, kwa sasa tunashughulikia mapapa.
 
Hiko kituo kinatakiwa kivunjwe na kijengwe upya kwa mpangilio unaofaa.
Sasa hivi ni gofu.
 
Wanajamvi naomba kuweka wazi wizi uliokithiri ndani ya stand ya Ubungo! Kuanzia alfajiri hadi saa 5 usiku wasafiri, wasindikizaji wanakumbana na vibaka wakiwa kwa makundi.

Wanaiba vioo, side mirror na kuvunja magari yanayoegeshwa ndani ya stand. Wasafiri wanaporwa sana. Kuna tatizo la usalama na taa ndani ya stand!

Mamlaka ipo kweli ? RC yuko busy kwenye media na matamko yasiyotekelezeka!

Katika SEHEM ninayoichukia na naona mara nyingi inatengeneza wezi ,na mkusanyiko usioelewaka ni ubungo ,naomba makonda aanze na stendi ya ubungo
 
Vijana wale vibaka...wana vioo hasa rav4.......

Back
Top Bottom