Viatu vya mitumba toka canada

Viatu vya mitumba toka canada

Incredible

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,031
Reaction score
1,603
Nipo Canada na kampuni yangu inasupply viatu vya mitumba grade A. Viatu hivi ni vya kike na kiume. Majina ni kama Nike, Naturizer, Jessica, American Eagles, 725, n.k.

Tunauza kwa 40ft container, au 20ft container. Bei ya hapa Canada ni $ 79 kwa balo. Freight charges ni $ 4,250 kwa 40ft na $ 2,950 kwa 20ft. Kwenye 40ft zinaingia balo 730, na 20ft zaingia balo 360. Pia kuna gharama ya $ 550 kwa ajili ya Inspection fees.

Mix ya viatu katika balo ni pair 8 raba, 6 viatu vya kiume, 5 viatu vya watoto, na pair 21 vya kike ambavyo ni simple shoes na high hills na sandals za kike. Idadi ya viatu ni 40 kwa balo.

Mawasiliano ni faoincredible@yahoo.ca
 
Mkuu nina mil 5,tu vp huu mtaji unatosha!! Au ni mdogo sana!
 
Mil 5 ndogo rafiki, sababu natuma container zima.
 
Milioni tano ndogo? Unachekesha sana, you have to think outside the box ili ufanye international business na third world countries ambazo ndo wateja wakubwa wa mitumba.
Fikiri namna gani utawa accomodate hata wenye mitaji pungufu ya kuweza kuagiza container zima. Nitaweka hapa contact details za kampuni moja ya namna hii ambayo inauza viatu na grade A na B, na si lazima mtu anunue container zima.
Hivi jiulize kwanini kampuni zinakubali letters of credit? Zinatuma mzigo kwanza kabla ya kulipwa pesa?
Mil 5 ndogo rafiki, sababu natuma container zima.
 
Mkuu nina mil 5,tu vp huu mtaji unatosha!! Au ni mdogo sana!

just an advice

kama mnaweza kujipanga watu wanne wenye 5M mnaweza kuweka umoja mkachangia na kuleta container nzima, baada ya mafanikio kila mtu akaendelea kivyake
 
mkuu tafadhali tupia picha za viatu vyenu mnavyouza tuone muonekano wake
 
Ndugu wana JF. Ninaishi Canada na ninasupply viatu vya mitumba grade A toka hapa Canada. Jana niliweka tangazo langu kwenye jamvi hapa na nilipata some few enquries, leo nimekuta halipo. Nimeamua kuamini kwamba siyo hujuma bali ni hitilafu za mtandao.

Viatu hivi ni grade A. Kila balo twaweka pair 40 yaani raba 8, viatu vya jiume vya ngozi pair 6, vya watoto pair 5, pair 21 vya kike ambavyo ni mchanganyiko wa( simple shoes, sandals, high hills).

Bei ya balo ni $ 79. Tunauza kwa 40ft au 20ft. Kontainer la 40ft yanakaa mabalo 730, na 20ft mabalo 360. Aina ya viatu ni kama American eagles, Naturizer, 725, Jessica, Alado n.k.

Freight charges zina range $ 4,150 kwa 40ft, na 20ft $ 2,950.

Kwa mawasiliano zaidi ni faoincredible@yahoo.ca

N.B
Kama itatokea tangazo likapotea tena kwa itilafu za mtandao basi nitaweka tena na tena.
 
Mkuu nashukuru kwa moyo na nia yako njema. Lakini niwajuavyo waTz wenzangu, first atalinganisha "mimi nifanye biashara ya mitumba wakati nina degree..."
Mtu yuko lazi atembee mjini na baasha kama mwendawazimu, kuliko kufanya biashara hiyo...
 
Ninaishi Canada na tuna supply viatu vya mitumba (gently used shoes) kwa kiwango cha konteina la 40ft au 20ft.

Ni viatu vya kike na vya kiume, baadhi ya majina ni American Eagles, Naturizer, Jessica, Nike, 725, n.k.

Bei kwa balo ni $ 79. Kwenye 40ft yanakaa mabalo 730, na kwenye 20ft mabalo 360. Hatuuzi kwa uzito bali kwa idadi ya viatu. Kila balo tunaweka pair 40 ambazo ni raba 8, viatu vya kiume vya ngozi 6, watoto pair 5, vya kike pair 21 amabavyo ni simple shoes, sandals, high heels n.k.

Hutuweki winter boots wala kiatu ambacho utakitupa.

Freight charges ni $ 4,150 kwa 40ft, na $ 2,950 kwa 20ft.

Kwa mawasiliano niandikie email faoincredible@yahoo.ca
 
belo chache inakuwa ngumu maana freight charges ni kubwa, na kwa ndege gharama ni kubwa pia.
 
Hiyzo bei siyo sawa!!!nikiwa arusha naweza kwenda kuchukulia nairobi kwa bei pungufu ya hiyo.
 
kwani lazima usafirishe kwenye ndege?hata kwa meli ni poa tu japo kutakua na some sort of delay,mil 5 sio ndogo blaza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom