TALAKA KATIKA UKRISTO (Mst. 6-8) Hakuna
talaka katika ukristo. Mwanadamu YEYOTE iwe ni
Mchungaji, Askofu, Jaji wa Mahakama Kuu ya
Rufaa au yoyote hana ruhusa kumtenganisha
mtu na mkewe, na cheti chochote cha talaka ni
batili, hakitambuliwi na Mungu. Mungu
alichukuliana na watu wa Agano la Kale kwa
ugumu wa mioyo yao, lakini hachukuliani na
yeyote katika Agano Jipya kwa suala la talaka.
Hata kama mke ameachwa kwa talaka potea,
hana ruhusa kuolewa na mwingine (1
WAKORINTHO 7:10-11).KUMWACHA MKE KWA
SABABU YA UASHERATI (Mst. 9) Hiki ni
kisingizio cha watu wengi wasio na maarifa
kuwaacha wake zao. Nyakati za Biblia mtu
alipotoa posa kwa mchumba wake, hata kabla
hawajaoana, waliitwa mtu na mkewe
(KUMBUKUMBU 22:23-24; MATHAYO 1:18-20).
Katika uchumba, kama mke huyo alithibitishwa
kuwa amefanya uasherati kwa kuwa na mimba
au vinginevyo ilikuwa ni halali kumwacha maana
ni dhahiri kwamba siyo mwaminifu. Ni kwa
sababu hiyo Yusufu alitaka kumwacha Mariamu
kwa kudhani alifanya uasherati. Vivyo hivyo,
katika Kanisa, watu ambao bado ni wachumba,
hata kama posa imekwisha kutolewa;
mmojawapo anapothibitika kuwa amefanya
uasherati, huyo mwenzake ana ruhusa ya
kumwacha kwa sababu inadhihirisha kwamba
hajaokoka. Lakini mtu na mkewe wakiisha
kuoana, uzinzi siyo sababu ya kuwaruhusu
kuachana. Mume anapaswa kumsamehe mkewe
mara saba mara sabini makosa YOTE kama
Mungu katika Kristo alivyotusamehe sisi. Je,
tulisamehewa dhambi zote kasoro uzinzi? Jibu ni
la! Basi uzinzi siyo kisingizio cha kumwacha mke
(WAEFESO 4:32).