VETA sijawahi kuwaelewa

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,034
2,000
Sina mengi zaidi, Mimi ni mmoja wa vijana wa ki-Tanzania, Hua natamani Tanzania iwe moja ya wagunduzi wa mitambo mbali mbali,
Watu ambao wangesaidia kugundua ni pamoja na watalam wa VETA cha ajabu mpaka leo hii sijawahi kuona mitambo ambayo imebuniwa na hawa watu wa VETA,
Mwenye uzoefu na product zao nijulishe mitambo ambayo imesha wahi kuvumbuliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,598
2,000
mkuu 'mitambo' hua inatengenezwa kutatua tatizo fulani au kurahisisha kazi fulani, lakini pia kuna swala la gharama za kutengeneza huo mtambo ukilinganisha na uhitaji/umuhimu wake, kwahiyo hao VETA hawawezi tu kuamka asubuhi na kuanza kuchoma mamilioni kutengeneza 'mtambo' ambao hata hakuna anaye uhitaji na wala hawajui unakwenda kutatua tatizo gani.
na pia huwezi ukatumia milioni 100 kutengeneza 'mtambo' ambao tayari unapatikana sokoni kwa milioni 5, kwenye nchi masikini hakuna hela za kuchezea kiasi hicho.
 

ArchAngel

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
4,447
2,000
VETA wafanye mpango wa pushback tractors ili siku nyingine tusisukume ndege kwa mikono.

Sent using Sukhoi Su-57
 

bbc swahili

Senior Member
Jul 17, 2017
175
250
aahh hawa jamaa utachoka mbona
niliingia katika banda lao la maoyesha hapa dar es salaam kipindi cha sikukuu za sabasaba
eennh eti wananionesha mashine ya kutengeneza vifungo vya sharti
moyoni iliniuma taasisi kubwa kama ile baada ya kutuonesha mamitambo makubwa au ugunduzi wa kaliba ya sasa


Sent using Jamii Forums mobile app
 

MfalmewaKiha

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
1,034
2,000
aahh hawa jamaa utachoka mbona
niliingia katika banda lao la maoyesha hapa dar es salaam kipindi cha sikukuu za sabasaba
eennh eti wananionesha mashine ya kutengeneza vifungo vya sharti
moyoni iliniuma taasisi kubwa kama ile baada ya kutuonesha mamitambo makubwa au ugunduzi wa kaliba ya sasa


Sent using Jamii Forums mobile app
Haaaaaaaaaaaaa eti mtambo wa vishikizo, Ayse ni hatari Sana, swali langu kwako ni kwamba, wakati wanakuonyesha walikua na ujasili kabisa Au walikua wanaona aibu kiasi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

BOB OS

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,320
2,000
VETA wagundua Dawa: Usipovaa Kofia ngumu Pikipiki haitawaka - JamiiForums

Mwalimu wa fani ya elektroniki kutoka Mamlaka ya elimu na mafunzi ya ufundi (Veta) kituo cha Kipawa jijini dar es Salaam, Aneth Mganga, amegundua teknolojia mpya ambayo itakuwa mwarobaini kwamadereba pikipiki ambao hawapendi kuvaa kofia ngumu.

Kwa kutumia teknolojia hiyo, mwendesha poikipiki asipovaa kofia ngumu, basi pikipiki anayotaka kuiendesha haitawaka.

Kwa mujibu wa mwalimu huyo, teknolojia hiyo mpya haipatikani mahali pengine popote duniani.

Akizungumza katika banda la veta katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi, mwalimu Aneth amesema mfumo huo ukianza kutumika utapunguza madhara yanayotokana na ajali za pikipiki.

“uzuri wa teknolojia hii ni kuwa hata anapokuwa katika mwendo, dereva akivua tu kofia ngumu, pikipiki inazima,” anafafanua mwalimu Aneth.

Amesema kwa upande mwingine teknolojia hiyo inazuia wizi wa pikipiki kwa sababu mwizi hatoweza kuiwasha pikipiki hiyo mpaka awe na kofua ngumu ambayo imeunganishwa kielektroniki na pikipiki husika.

Mwalimu Aneth ameiomba serikali na wadau mbalimbali kuunga mkono ili kueneza teknolojia hiyo na kusaidia kampeni zirtakazoifanya ikubalike katika miongoni mwa waendesha pikipiki katika maeneo mbalimbali nchini.

Akielezea juu ya gharama ya vifaa vinavyotumika kutengezeaa kifaa hicho, mwalimu Aneth alisema kuwa kwa sasa vifaa hivyo vinapatikana nje ya nchi na anatumia fedha nyingi kuviagiza kwa sababu huagiza vichache.

“Naamini kama utawekwa utaratibu utakaowezesha kuviagiza kwa wingi, bei yake itapungua sana,” amesema.
 

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,140
2,000
Hii mada yako (yenu) imekaa kishabiki au lah, una ugomvi na VETA.

Vocational Education & Training Authority SIO SEHEMU YA MAVUMBUZI. Pengine umekurupuka tu na lawama bila kutafakari hasa nini maudhui ya VYUO VYA UFUNDI STADI.

VETA kazi yake ni kuzalisha mafundi, sio WATAFITI. Entry Requirements za kozi nyingi za VETA ni CHETI CHA KUHITIMU ELIMU YA MSINGI, hakuna mtu atatoka VETA akaitwa ENGINEER. Je, ni hawa watu wa Darasa la Saba ndio umewafungulia uzi wa kuwalaumu hawajavumbua TREKTA?

Kama una hasira na nchi yetu kukosa wavumbuzi, hasira zako zielekeze VYUO VIKUU. Universities ndio hasa sehemu ya mavumbuzi. Research zinafanywa huko na Maprofesa na Madokta, tunapata chanjo na tiba, na Mainjinia watuvumbulie mitambo. VETA itazalisha mafundi wa kurekebisha hiyo mitambo.

Sitashangaa ukiniambia una degree.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom