Delloite & Touche ndiyo wanafanya mchakato mzima wa ajira hizi za VETA. Nimechoka kabisa kusikia taasisi ya Umma inatafuta wafanyakazi katika middle level management na Junior staff kwa kutumia kampuni binafsi. Mamlaka yenye umri mkubwa kama hii, Mkurugenzi na idara ya human resources nchi nzima nk. kutumia kampuni aaagh. Siyo hivyo tu pia kuna Management ya ajira serikalini, japo inahusika na wafanyakazi wa idara na taasisi za serikali zilinazotegemea budget ya serikali lakini pia ni wakati muafaka kwa taasisi nyingine za serikali zisizo na uwezo wa kuajili kama VETA kutumia idara hii. Naomba kuwasilisha